Siku za hivi karibuni kumejitokeza tabia si ya uanamichezo kwa baadhi ya mashabiki wa soka kurushiana viti uwanjani pale Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Naomba hili niliweke sawa kama mchango wangu kwa taasisi husika,ili iwe changamoto na pengine suluhisho la tatizo zima.Nadhani baadhi ya mashabiki mtakubaliana na mimi kabisa kwamba pale uwanjani kuna idadi ya viti vingi sana havina NATI za kushikia yaani viti viko loose.
NINI CHANZO?
Kwa macho yangu niliwahi kushuhudia kwenye mechi moja kijana mmoja akiwa na kiroba kimejaa CLAMPS (Clamp ni chuma kinachoshikilia kiti kwa chini kisha kinafungwa kwa nati.) Nilichofanya niliripoti kwa askari yule kijana akakamatwa na alipoulizwa alisema anaenda kuuza vyuma chakavu.
Hata hivyo,pamoja na hayo sikubaliana na upuuzi unaofanywa na baadhi ya mashabiki kurusha viti.Lakini kwa upande mwingine hoja ya kwamba viti vinang’olewa mimi siafikiani nayo kabisa.Vile viti vimefungwa kwa uimara mkubwa sana, hakuna mtu anaweza kung’oa kwa kutingisha tu,lazima kwanza awe na spana kisha ainame chini kufungua kiti (Inahitaji time).
Nini maana yake sasa? Ni kwamba,vile viti vinavyorushwa uwanjani mashabiki wanavikuta vikiwa havijafungwa yaani viko loose na ndipo matatizo yanapoanzia.
MAONI YANGU!
Wenye mamlaka na usimamizi wa Uwanja wa Taifa wachukue hatua za maksudi kufanya ukaguzi na kurudishia nati katika viti vyote.Pili,uwepo usimamizi wa kutosha na hasa kwa watoto wadogo ambao wanakua na viroba uwanjani kwa kisingizio cha kuokota chupa kumbe wanafungua nati.Na tatu,tuwe na ulinzi shirikishi kwa kila mtu pale uwanjani kuwa mlinzi wa mwenzake kwa kutangaza motisha ya pesa taslimu kwa mtoa habari yeyote (Kama manispaa ya mji wa Moshi inavyofanya) juu ya uharibifu wa mali kuanzia viti,switch,taa,koki,na wanaokojolea katika masinki ya maji.
Huu ni mtazamo wangu,
Furaha “Mkatakona”
Nashukuru mdau kwa kuleta mada hii mezani.Wiki iliyopita nilishuhudia mechi kati ya Simba na Toto African.
ReplyDeleteNilikuwa nimekaa sehemu moja hivi utaona viti vimeandikwa nembo ya NSSF.Kwa upande wa juu mkono wa kulia wa sehemu hiyo ninayoisema, nilishuhudia mwenzangu mwingine aliyetaka kukaa kwenye kiti akataka kuanguka kwani kiti kilikuwa ni kibovu. Nikashangaa hiki kiti kimeharibiwa saa ngapi kwani watu ndio kwaanza tulikuwa tunaingia uwanjani.
Hili suala la kwamba watu wanang'oa viti kwa makusudi haliniingi akilini kama mdau anavyosema vile viti vimefungwa na nati hata ukisimama juu yake huwezi kukiharibu kirahisi.
Nina wasi wasi zile pesa vilabu vinavyopigwa faini ni uonevu mkubwa kabisa!
DAWA YA UHARIBIFU WA VITI UWANJANI:
ReplyDelete1.Viti vyenyewe inaonekana havijapachikwa madhubuti, inatakiwa viwekwe madhubuti ili kuhimili mikimi mikiki mfano hata ktk kipindi cha Ushangiliaji kwa wenye Midadi wanaweza wakang'oka navyo ni vile vipo legelege.
2.Kila 'Mwana Mayoka Manungu adhibiti majoka yake' kwa wale watu wa kule Tabora Wamanungu wanaocheza na Nyoka hivyo kila Mchezea Majoka adhibiti majoka yake nikimaanisha kila Kilabu cha Michzo kidhibiti Mashabiki wake huku TFF ikisimamia msisitizo huu.
Kamera za usalama zipo kila kona uwanjani,kwa nini wakati wa mechi zisitumike? au tunaogopa gharama za umeme zitapunguza mapato?
ReplyDeleteUdhibiti wa uwanja na vifaa vyake upo ndani ya uwezo wa mamlaka inayosimamia uwanja huo.
ReplyDeleteNinashauri,
kwanza, mamlaka husika ziongeze idadi ya walinzi majukwaani.
Pili, sekyuriti kamera ziwekwe wazi wakati wote.
Gharama zote hizi za ongezeko la ulinzi lifidiwe na watazamaji wenyewe, kwa maana ongeza kiwango fulani kwa kila tiketi.
adri tiketi itakavyokuwa ghali basi na uwanja utazidi kusalimika.
binadamu hachungwi !! ila busara na hekima ndiyo dawa pekee ya uharifu huu,bado mbongo hajawa mzalendo na waelimishaji hawajaenda mbali kutusaidia katika kutujenga. waelimishaji ni wazazi na waalimu na pia vyombo vya habari ikiwemo serikali. kisha namalizia kwa kusema kwamba ,sehemu zote za mashabiki wa kipato cha chini, VITI vibadilishwe kwa kujenga viti vya simenti (concreate). Zebedayo mna Nasa.
ReplyDelete