Mwamuzi Israel Mkongo akipigwa na wachezaji wa Yanga  kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliokutanisha timu hiyo  ya Jangwani na timu ya Azam FC kutoka Chamazi ambapo Yanga ilikandamizwa magoli 3-1 na wauza Sembe hao wa Chamazi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


Mwanzo ulikuwa ni mchezo mzuri uliokuwa wa vuta nikuvute kwa kila upande lakini mambo yalibadilika mara baada ya Azam kuandika goli la kwanza, mchezaji Haruna Niyonzima wa Yanga alionekana kumlalamikia refa mara kwa mara jambo ambalo refa alimuonya mara kadhaa lakini, hata hivyo Niyonzima aliendelea baada ya muda, alitolewa nje kwa kadi nyekundu, jambo ambalo lilizua tafrani uwanjani huku makonde yakirushwa hovyo, baadae naye mchezaji Nadir Haroub Canavaro alipewa kadi nyekundu kutokana na vurugu hizo na kuzua tifu lingine uwanjani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Waamuzi kama hawa wasichezeshe mpira.

    ReplyDelete
  2. JAMUHURI INABIDI IWAFUNGULIE KESI WAJINGA HAWA.UTAPIGANAJE KWENYE KADAMNASI YA WATU KAMA MWEHU...YANGA MMETIA AIBU KWELI.

    ReplyDelete
  3. Ni aibu kubwa sana kwetu. Na adhabu za mwaka mmoja na faini isiyozidi hata dola 650 kwa Stephano Mwasika na wengine kupewa adhabu zisizoweza kuwafanya watu waogope kuleta upuzi kama huo.Pia: viongozi wa Yanga, walinzi na mapolisi wako wapi? Dakika kumi refa anashambuliwa na hakuna anayeingia kati kumlinda? Mapolisi hapo uwanjani ni wengi ila wanafanya nini? Anayeongoza ulinzi pamoja na team members nao waadhibiwe vikali.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  4. hawa ni wachezaj washenzi sijapata kuona.mpira sio boxing,fungia kabisa hawa wapuzi,nimfano mbaya kwa jamii,uongozi wa yanga pia unatakiwa kuwafukuza wachezaji wajinga kama hawa ili wasihribu jina la club.

    ReplyDelete
  5. Tupatie na stori ya upande mwingine, refa alifanya nini?

    ReplyDelete
  6. wachezaji pumbavu hao Marisa. Fungia hata miaka 4 ni sawa kabisa. Tunatoa hela zetu kuangalia kabumbu sio masumbwii.

    ReplyDelete
  7. The Referee should take to court these players, he was basically assaulted at work. Why 6 weeks or one year, in other countries they would have faced very heavy penalties it is illegal to come into contact with a referee at ny point in time. Wake up Tenaga!!

    ReplyDelete
  8. ndo maana soka la bongo haliendelei, kucheza hamjui mnaendeleza ubabe usio na mpango, sasa unampiga refa wa nini?

    ReplyDelete
  9. Bwana michuzi leo ndio mnasema tutapata timu ya taifa mmmmmmmm ni sawa sawa na simba kumuweka kwenye nyumba moja na mbuzi hawa wachezaji waliohusika wafunguliwe kesi pia wafunguwe ili liwe fundisho kwa hawa wajinga yanga na uongozi walikuwa wapi na police nii aibu subiri kidigo clip hii tuisukeme bbc utasikia

    ReplyDelete
  10. hii sio nidhamu kabisa wachezaji kama hawa wafutwe kabisa kucheza soka maana huu ni uhuni sasa

    ReplyDelete
  11. kila siku tunarudia maneno,naona tuache mipira ya ulaya tujenge ya kwetu tuige majirani zetu zambia,hali inazidi kuwa mbaya bongo ujinga haishi sheria hazifuatwi,nini tatizo?uwanja tunao mzuri kabisa

    ReplyDelete
  12. I can't believe these players have no date in the courts. That is a physical assault. Where are the police. The guy was running away from them and they still chased and flogged him. Can the IGP tell us what action is being taken regarding these hooligans, forget about soccer!!! It is an assault.

    ReplyDelete
  13. Inafahamika toka enzi na enzi kwamba Yanga hawajui mpira. Yaelekea na wao wameanza kujitambua na kuanza kujihusisha na masumbwi. Washukuru sio mechi zetu za Uswazi maana huko refa anakuchomolea nanga.

    ReplyDelete
  14. wachezaji wafungiwe na faini pia.POLISI mko wapIIIIIII! aibu.
    Kama refa anamakosa kun a utaratibu kabla na baada ya mechi. BONGO mpira haukui,wachezaji hawana NIDHAMU.

    ReplyDelete
  15. Jamaniii watanzania wenzangu tujaribu kubadilika ktk mchezo Wa mpira Wa miguu, maana kwakweli tanzania unapokua muhuni Wa mitaani ndo unajiona unajua mpiraaa kuwa mbabe kujipigia mabuti wachezaji wenye nidhamu, ss ona uhuni umeenda mpaka mechi kubwa kama hii tena timu kubwa kama yanga wanampiga refa alafu haitoshi hao washenzi baadhi yao wako taifa star ss tunatarajia nn sisi wtzania kutoka ktk hao wajinga ktk timu yetu ya taifa. Alafu sasa kibaya zaidi polisi wako wapi hapo? Je kama wangemtia huyo refa mtu kati siange aga dunia, yani polis wapo magetini tuu Co. Uwanjani IGP awajibike kwa vijana wake,, mulamba mwana Wa totoo

    ReplyDelete
  16. TZ ndio hiyo... kila sehemu vururuvururu.....Ukiona mtu anakimbilia kupigana ujue hamna kitu kichwani mwake... hiyo timu ni ya kuogopa kama ukoma...ikimbiwe.Si waliopiga tu ila ni wachezaji wote. Kama wangekuwa wachezaji wangekuwa waungwana, baadhi yao wangeonekana kuzuia vurumai hiyo. Lakini wote waliunga mkono upuuzi

    Hata polisi pia wachukuliwe hatua. Maana refa anapigwa mpaka anakimboa na wanamfuata kuendeleza kipigo polisi walikuwa wapi! hiyo jeuri ya kupigana hadharani na polisi wakiwepo waliipata wapi? ina maana walishapanga na polisi kumpiga refa.

    ReplyDelete
  17. Uhuni uhuni tu huu, inaonyesha ni jinsi gani timu zetu zinaundwa na wahuni huni tu. Soka la namna ya masumbwi badala ya soka lenyewe na kujituma ni upuuzi mtupu, hatufiki mbali. Hata makazini mabosi huwa wanauzi lakini huwa hatupigani. Kiliwashinda nini hawa wachezaji kutulia hata waamue kurusha makonde ya nguvu namna hiyo kwa refa. Refa Ndg Mkongo peleka mahakamani wajinga hao ili iwe fundisho.

    Chaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  18. TTTT FFFF FFFF mpo WAAAAAAAPI mbona hamtoi kauli yeyote. BONGO bwana tambarare.Shangilieni tu Arsenal n.k, ndiyo kazi yetu na kuvaa majezi ya nje.MPIRA bongo miujiza tu.

    ReplyDelete
  19. Refa kama ameboronga hilo ni jukumu la klabu sio mchezaji kuchukua hatua ya kumhukumu kwa masumbwi. Sheria zipo, na hatua za kuchukuliwa zipo. Hao wachezaji wa Yanga ni aibu kabsaaaa!!!

    Katika michezo matukio kama haya hayatakiwi kabisa, huu ni udhaifu mkubwa katika nidhamu.

    ReplyDelete
  20. Mi niko tofauti kwani sicomment kwa ushabiki.kuzongwa na wachezaji hata ulaya kupo na inatokea pale mwamuzi anapofanya maamuzi ya utata.Kwanini waamuzi wa Tanzania hata kwenye CECAFA wanakuwa ka si mmoja wawili - - - - - -Poor referiing .mi nilivyoona aliyempiga refa ni mtu mmoja tu na kutoka na upoor referiing anakuja kutoa nje mtu mwingine.Kitendo cha wachezaji kumzonga na mmoja wao kumpiga refa waziwazi mi kinanitia mashaka kwamba inawezekana hawa jamaa wamekula mlungula kwani wana njaa sana.Haingii akilini kwani siku Nsajigwa alipopewa red card mbona wachezaji walikuwa normal au siku ile walipata kijiti kikali? pia kitendo che Fab kulalamika kama msichana toka mwanzo inaweza kuwa ni njama ya kujtaftia red card ya kujitakia

    ReplyDelete
  21. Kama TFF wameshindwa kusimamia suala la rushwa michezoni unategemea nini?

    ReplyDelete
  22. hawa wachezaji hawana adabu kabisa. hiyo adhabu ni ndogo sana, mi nilitegemea angefungiwa kucheza soka maisha

    ReplyDelete
  23. We mpuuzi uliyepost hii hapa mbona hukupost clip zinazoonesha maamuzi ya refa yaliyozua sokomoko? Yaani wewe, refa na hao wachezaji lenu moja.

    ReplyDelete
  24. SAFI SANA ! waamuziwamezoea sana kupokea hongo ili wawakandamize upande ambao haukutoa fezwa! tena ningefurahi kama yule tegete angekuwa amevaa ile chuma mkononi ! puuzi mkubwa ! wanatia hasira hawa, kila siku huwa nashangaa watu kushadadia mipira ya nje kumbe matatizo kama haya ya waamuzi kuhongwa yanakatisha tamaa, mpia TAnzania hakuna sio kama enzi zile za miaka 70.

    NA wewe michzui mshambenga kweli kweli maana unairudia rudia ! mh!

    ReplyDelete
  25. Kupigana ni kitu mbaya sana na haikubaliki but chanzo cha yote ni nini?Refa lazima kuna kitu amefanya mpakahawa players wakawaka hivi they were provoked I m sure chanzo ni nn tusiishie ushabiki tuuu

    ReplyDelete
  26. Am a Yanga fan..but not this Yanga..
    Shame on you Yanga..Mwasika hovyo..Nadir hovyo..Yanga haina nidhani..haina uanamichezo..huo ni uhuni wa hali ya juu..inatia aibu kuona uongozi unakata rufaa..shame on you myopic Yanga leaders..mnakata rufaa kutetea ujinga ule..TFF rekebisheni miongozo..hapa ingefaa timu iporwe points za mechi kumi ilizoshinda na ifungwe goli 20 kama adhabu kwa timu..hao wachezaji wangefungiwa kujihusisha na soka for life...tatizo bangi..yaani its beyond repair..uuuf..

    Hivi sio Yanga hawa hawa waliogomea mechi na simba cecafa ya mwaka juzi..jamani..hii timu kuanzia viongozi hadi wachezaji bogus

    ReplyDelete
  27. Mwamuzi alifanya nini mpaka apigwe? Maana tusiwalaumi tu wachezaji kumpigia huyu jamaa unaweza kuta mwamuzi nae ni mjinga mmoja ambae anajiona kwa vile ye mwamuzi basi anaweza kuleta maamuzi ya mkewe nyumbani uwanjani; acha apigwe tu kama kaleta za kuleta hata hao wachezaji wakifungiwa poa tu ila jamaa kichapo cha wanaume kesha kachezea. Mpira Bongo nani kasema acha watwangane tu maswumbwi.

    ReplyDelete
  28. Yanga walishazidiwa walikua wanataka mechi ivunjike. duh aibu kweli!

    ReplyDelete
  29. Wakiona wanashindwa ndio hivyo, hii ni reflection kutoka katika maisha ya nyumbani, familia, society, siasa inaathiri hata katika mahusiano katika michezo na kadhalika. Hii ndio bongo. Umeona Arusha siasa ilivyoharibu ule mji wa Kimataifa.

    ReplyDelete
  30. Ile ngumi kapiga kijinga, angepiga 'upper cut' ili iwe fundisho kwa Mkongo na wengine wanaoleta unazi mpirani. Hii najua hutaitoa kwa kuwa wewe ni Simba, Mkongo Simba na aliyeweka clip hii pia ni Simba...wote waharibifu wa soka.

    ReplyDelete
  31. Uamuzi tete wa Mwamuzi siku ile Yanga V/S AZZAM pana uwezekano Mwamuzi alilipwa Mshahara maalum kutokea Chamazi au Msimbazi!

    ReplyDelete
  32. Acha kusema Tanzania au Watanzania na wewe.Hii ni tabia ya mtu,si tabia ya Taifa.Acha hoja za kipuuzi.

    Tushambulie tabia ya mtu,kweli huyu aliyempiga refa ni mjinga kabisa.Badala ya kujiunga na mchezo wa ngumi yeye kajiunga na mpira wa miguu.

    Anataka refa awapendelee tu hata kama hawawezi.Wenzenu MAN U wanapendelewa kila mara lakini na kakishawishi ka uwezo wanako.

    Hii ni tabia mbovu sana kumpiga mwamuzi na ikomeshwe kwa ukali zaidi.Huyu kawachafulia sana watani wetu.Si kweli kuwa Yanga wanapenda mambo haya bali ni kichwa mbovu ya mtu,ndo maana wapo na wachezaji wenzake wanamkataza.

    Hivi wachezaji wanao sajiliwa wanapimwa afya kweli ikiwa pamoja na akili!Si kama kuna malalamiko captain aseme na refa,kwani kila mchezaji lazima aongee na mwamuzi.

    Wenye akili mbovu si wachezaji wa bongo tu,hivyo kusema "wabongo bwana" ni maneno ya ovyo ovyo sana hayana nafasi katika mjadala huu.Hivi wakina Rooney,Gatuso,Gaza,kule Misri nako ni wabongo!Acheni hoja za vichochoroni.

    Lakini,na polisi jamani refa anakimbizwa umbali wa kilomita nzima bado hamtokezi kumwokoa.Au manaangalia mpira tu,au nainyi ni Yanga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...