Mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joshua Nassari na Meneja wake wa Kampeni, Vincent Nyerere, wakiwalisha chakula watoto yatima wanaolelewa na Kituo cha Hospitali ya Nkoaranga ya KKKT iliyopo Kata ya Poli, walipotembelea katika hospitali hiyo
Mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joshua Nassari na Meneja wa kampeni wake, Vincent Nyerere, wakimfariji kijina Peter Gadiel, ambaye alipata ajali ya pikipiki akiwa katika msafara wa mgombea huyo juzi, ambaye amelazwa katika hospitali ya Nkoaranga inayomilikiwa na kanisa la KKKT.
Meneja wa kampeni wa mgombea wa ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chama cha Domokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mchungaji Israel Natse (kulia), akiongoza maombi ya kuwaombea wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Nkoaranga iliyopo Kata ya Poli, wakati mgombea na ujumbe wake walipotembelea hospitalini. Picha na mdau Joseph Senga
Nina wasiwasi sana jinsi viongozi wa kidini walivyojiingiza na kukamata nafasi nyeti katika Chama cha demokrasia na Maendeleo. Hali hii inaweza kuchangia kufifia kwa chama cha wananchi kwani waumini wa dini zingine walianza kuhisi udini katika chama hicho hali ambavyo chadema inakwenda nayo sasa.
ReplyDeleteSi dhambi kwa viongozi waandamizi wa dini kuingia katika duru za siasa, lakini si tutakuwa tunajikanganya? tulikuwa tukihubiri kutenganisha siasa na dini kwa miongo kadhaa, si tutakuwa tunataka kuyarejea matapishi?
Mimi nasema hii haijakaa sawa, inaonekana kuna ajenda ya siri ambayo ikija kudhihiri itakuwa imeutafuna umoja wa kitaifa tuliokuwa nao toka uhuru. Hali iliyoitafuna CUF itakuja kukitafuna CHADEMA ili kunusuru amani ya nchi kwa uwezo wa bwana.
KK
ZNZ
hivi CDM pekee ndo ina viongozi wa dini? Mchungaji Rwakatale naye ni CDM? sema viongozi wa kidini wanaingia kwa kasi kwenye siasa na siyo CDM
ReplyDeleteMtaji wa mwanasiasa ni umaskini wa mali na akili wa mpiga kura!
ReplyDeleteKK, hebu tulitazame hili kwa upande mwingine. Viongozi wetu wanakanywa kuwa ili waweze kuwa viongozi bora zaidi ni lazima wamuogope na kumcha Mungu. Kiongozi anayemuogopa Mungu pia ataogopa kufanya maovu akiwa madarakani. Hivyo kwa upande mmoja hili ni jambo zuri, na uzuri wake unaongezeka pale baadhi ya wacha Mungu wanapokuwa na wale wengine wasiomcha Mungu na hivyo kupelekea uwezekano wa kuwaambukiza na wao au kuwakumbusha kutenda mazuri kila wakati.
ReplyDeleteMimi binafsi, nitamsikiliza na kumuheshimu sana kiongozi mcha Mungu, bila ya kujali dini yake. Wacha Mungu huwa wapo katika levo moja, tofauti ni namna tu.
Hata nchini kwetu tumekuwa na historia ndefu ya viongozi wacha Mungu...kama vile Al haji fulani, sheikh fulani, mchungaji fulani, n.k. Kumbuka kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya kuwa mcha Mungu na kuwa mdini. Ukiambiwa leo hii uchague upande upi wa viongozi kati ya wale wanaomcha Mungu na wale wasiomcha Mungu, wewe utachagua upi ndugu yangu? Angalia mifano tuliyonayo leo hii.
Kumbuka pia binadamu wote chimbuko letu ni Mungu, na kumcha Yeye si ombi bali ni wajibu wetu. Hivyo tuna bahati ya kuwa na viongozi wanaotekeleza jukumu kuu kuliko yote (kuliko hata uongozi wenyewe) mbele ya muumba wetu.
Tatizo watu ni wanafiki wakutupwa,, CCM hakuna mchungaji? Au msanii? Vyama vingine vikiwa nawo ni kosa? Eti chama cha kidini na CMM na mama rwakatare je? CCM ndio mabingwa wa kusingizia vyama udini,, acheni unafiki huo!
ReplyDeletemchangiaji hapo juu,hatujawahi kusikia viongozi walio kwenye siasa wakizungumzia habari za Mungu hata baada ya vikao vyao saa za jioni,hivyo ni kwamba wakishachaguliwa tu wanaelemea kwenye siasa zaidi ya kazi waliyoitiwa ya kuhubiri injili.hawawezi kukemea hata maovu yanayofanyika mbele yao.ukweli utabaki pale pale huwezi kuchanganya dini na siasa chagua moja
ReplyDeleteChadema kweli mmejaliwa ! Mashekh na Wachungaji/Maaskofu wote wanawakubali.Mwenye akili anaona,kweli akili ni nywele .....Mh. Nassari swali la nyongeza ?
ReplyDeleteKwa maslahi ya umoja na amani ya nchi yetu hatunabudi kuepuka kuchanganya DINI NA SIASA.
ReplyDeleteHata hizo ULAYA na MAREKANI hazikuendelea kwasababu ya uongozi wa kidini na ndio maana leo hii wanabariki ndoa za mashoga, ni isimamizi mzuri wa sheria tuu!
Tusijidanganye kwamba viongozi wa dini wanamuogopa MUNGU, uchamungu ni tabia ya mtu, bila kujali Mwanasiasa, Kiongozi wa dini au Mpagani.
Hebu tujiulize, ni viongozi wangapi wa dini ktk nchi hii, wamebariki UFISADI kwa kupokea sadaka na ufadhili wa majengo ya ibada huku wakijua wazi kwamba hizo ni fedha haramu?
Eti leo hii wanachukia ufisadi, huu si unafki huu?
Inaonekana Imani hizi zimeshidwa kudhibiti waumini wao.
Tofauti zao ni ndogo tu kama vile;
wafuasi wa imani ipi wanaongoza kwa
UFISADI, UZINZI, ULEVI nk.
Heee,
ReplyDeleteInakuwa kama vile ni muda wa jioni usiku unaingia tupo safarini na sasa Kilometa chache kwa mbali mataa yanaonekana yanang'ara tunaukaribia Mji wa Ahadi wa Galilaya!
Uenezi huu wa Kiimani na Kihali kutoka vyama vya Siasa na uendelee hata baada ya Uchaguzi Arumeru Mashariki!
Chadema ypou have allowed yourself to fall so low by using cheap popularity of using even orphans for your own interest. Shame on you.
ReplyDeleteNamuunga mkono mchangiaji wa kwanza! lakini hii sio kwa CDM peke yake.
ReplyDeleteMm nadhani Watanzania sote tuache ushabiki wa dini kwani unaweza hata kupunguza uzalendo wa nchi yetu.
Kwa mfano siku za hivi karibuni kumezuka mtindo wa kushabikia taifa la Israeli kwa mabendera nk. sasa najiuliza siku ikitokea TZA kutofautiana na Israeli kisiasa ama kimaslahi, baadhi ya watanzania si watatusaliti?
Na kwa uzoefu Waisraeli hua hawampendi mtu, ukitaka kujua waulize Wakristo wa kipaletina.
Mimi naamini nchi hii inahitaji viongozi kama Kingunge au Dr. salim ambao dini kwao hazina nafasi.
Weweee Anony Sat Mar 17, 03:06:00 PM 2012.
ReplyDeleteSHAME ON UR SELF. Tatizo gani hapo kwa CHADEMA kuwatembelea yatima..ur so ST&@$#D!! Ulitaka na wao wagawe kagha na tishirt tu nod msaada, au wagawe ubwabwa na nyama ndio wapate kula. acha upuuzi! CHADEMA walichofanya ni bora zid ya kampeni zozote chama chochcote kilivyoawah kufanya. ukiangalia vizuri..walitembelewa nia watoto..hapoa CHADEMA haikutegemea kura zao bali mioyo yao..imefanya kuwarimu,kuwajali na kujenga kitu mioyoni mwao..kwamaba wanapendwa..japo hili llimtokea wakati wa kampeni lkn ni bora kuliko yoooote uliyowahi kusikia.Munu awabriki watoto hawa, na sara zao za kuiombea CHADEMA,Mungu mbariki Joshuo, Mungu ibarikia CHADEMA, Mungu ibariki Tz.
KAKA hongera kwa kutumia kichwa cha chin kufikiria, coz huna hoja ya kujadil CDM SHINE LIKE A STAR. unakandia had kusalimia wagonjwa/o laa mounsier
ReplyDeleteHURUMA ya CHADEMA:
ReplyDeleteAnonymous wa Sat Mar 17, 05:47:00 PM 2012
''SHAME ON YOUR SELF. Tatizo gani hapo kwa CHADEMA...
Wasiwasi wa watu ni kuwa HURUMA hiyo ya CHADEMA kwa ma Orhpans na Sick people inaweza kuwa ni ya muda tu zaidi zaidi ni ya kipindi hiki cha Kampeni za Uchaguzi!