Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akiweka jiwe la msingi katika Jengo jipya la Machinjio lililojengwa katika Kijiji cha Ngelewala mkoani Iringa wakati akimalizia ziara yake katika mkoa huo jana. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, C. Ishengoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Kilimo na Mifugo wa Manispaa ya Mafinga, Augustino Nyenza, wakati akitoa maelezo kuhusu jengo jipya la Machinjio lililojengwa katika Kijiji cha Ngelewela mkoani Iringa, jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wachungaji wa mkoani Iringa, baada ya kumaliza majumuisho ya ziara yake katika mkoa huo jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, kupitia tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa, wakati akiwa Uwanja wa Ndege wa mkoani Iringa jana akirejea jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara yake ya mkoani humo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huyu waziri ofisi yake iko wapi maana kwa ziara anaongoza je bajeti yake ikoje

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...