Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Ofisi za Tawi la CCM Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja jana, Machi 30, 2012. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini Magharib, Mohammed Yussuf, wakati alipofika mkoa huo kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Ofisi za Tawi la CCM Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja jana, Machi 30, 2012. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na mmoja kati ya wazee wa eneo hilo ambaye ni kati ya wazee waliokuwa na kucheza ‘Chandim’ pamoja. Hapa ilikuwa ni baada ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Ofisi za Tawi la CCM Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja jana, Machi 30, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Marekebisho. Mh Shamsi Nahodha ni mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe na sio mbunge ila ni mbunge wa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri Ya Tanzania kwa uwezo aliopewa kikatiba. Mdau OU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...