Baadhi ya wananchi wa Kata ya Dumila, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro wakiangalia maji yaliyojaa kwenye mto Mkundi na kusambaa kwenye mashamba ya wakulima wa Tarafa ya Magole, kama walivyokutwa darajani hapo na mpiga picha wetu.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh. Adam Malima ( kulia) akijadiliana na msajiliamali,Adam Masemo,( aliyenyoosha mikono miwili mbele ) anayefanya biashara ya kuuza mafuta ya petroli kwenye chupa za plastiki kwa madereva wa Pikipiki ‘ Bodaboda’ eneo la Magubike, Wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro.
Mkulima wa Kata ya Dumila, Tarafa ya Magole, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, Mariam Kisongela, akitoka shambani kwake baada ya kuona maji yamezingira mashamba yao wakati wakiwa mashambani,kama alivyokutwa eneo hilo.Picha zote na John Nditi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Dah!

    Huyo Mama anarisk sana. Hakuna mamba hapo kweli jamani?!

    ReplyDelete
  2. Waziri wa maji na wadau wengine wangetauta njia ya kuyahifadhi maji haya yanapokuwa mengi kwani mara nyingi mvua za msimu zikianza kwa mafuriki basi ujue fika ukame utakuwepo,tujipange ili tuyazuie maji haya ili yatusaidie baadae.Wenzetu kenya wameanza kilimo cha umwagiliaji kwa kasi nasi twangoja nini????,tujumuike na wenzetu wanapokimbia nasi tukimbie tusitambae.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...