Baadhi ya wagonjwa waliopo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili wakisubiri huduma katika Kitengo cha Mifupa (MOI), huku wakiwa hawajui hatma yao baada ya madaktari kuanza mgomo wao kwa mara nyingine tena leo. (Picha na Francis Dande)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. dah hii inasikitisha kweli ukiwaangalia wananchi wote wanaonesha wana huzuni .. sijui alaumiwe nani rais na baraza lake la mawaziri au madaktari maana suala la uzalendo tunasema mawaziri sio wazalendo maana wanapoonesha kufeli katika kazi hawataki kuwaachia wengine na waziri mkuu nae anasisitiza madaktari wawe wazalendo..

    ReplyDelete
  2. Inasikitisha sana kuona ndugu zetu (wagonjwa) wanateseka namna hii wakati kuna viongozi tuliowachagua kutatua matatizo kama haya.

    ReplyDelete
  3. Kwa kifupi madaktari wamefanya maisha ya watanzania Kama chambo cha kupata madai yao. Kwa staili hii basi wao ndio wenye mamlaka ya kuongoza nchi hii, maana leo watadai huyu ajiuzulu kesho yule keshokutwa yule! Hebu madaktari kuweni na aibu muone haya na mjue vibaya. Kama kuna jambo mmefanikiwa katika issue hii yote basi ni kudhalilisha fani yenu wenyewe na kujishushia hadhi. Hebu fikiria kesho wanajeshi nao wakiibuka na madai kama yenu hivi kweli patakalika? Kuweni na adabu japo kidogo kwa wananchi.Nyinyi sio miungu watu.

    ReplyDelete
  4. kwa nini uzalendo uwe kwa madaktari tu. nasio wale viongozi nao waonyeshe uzalenda kwa kuachia ngazi?.

    ReplyDelete
  5. madaktari ni watu ambao wanasikitisha sana, watu ambao ufikiri wao ni kama vikuku, hamuwezi na hamna haki ya kumfukuzisha kazi waziri mnachoweza ni kumshauri rais na sio kumpa mashart ya nini cha kufanya, na vilevile, nynyi mdai vitu ambavyo vinawahusu na sio otherwise, na vilevile mjue hammkomoi mtu but raia co pina na president wanamadaktari wao, so acheni mambo yenu ya kishenzi rudini kazini maana sasa hivi mmeanza kuboa, hebu jaribuni kukua na mrudi kuangalia sheria zinasemaje na mtoe madai bassed on employment law na kama hivyo vitu vipo kwenye mikataba yenu ndi mnahaki ya kudai na sio vinginevyo plse acheni huo utoto wenu.

    ReplyDelete
  6. Poleni wagonjwa wetu, ila msijali nendeni private. Mbona TRA wao hawagomi? heh heh, he, au mshiko ni mkubwa?

    ReplyDelete
  7. jaman hadi huruma tanzania imeozaa.... hawa maskini si watakufa tu hovyoo hee madaktari hv mlisomea kutibu au kuua?????

    ReplyDelete
  8. Wananchi wanabidi wawajibishe viongozi na sio Madaktari, suala la uzalendo lisiwe kigezo cha uzembe wa viongozi. Kama ni uzalendo basi wafuatilie majukumu yao kila siku sio wasubiri mpaka kufikia watu kuchoka na kero na wanyonge ndo wanaoumi.

    ReplyDelete
  9. Hapa ni suala la udini kwa ktk nchi hii...!chunguzeni mtagunduwa...!

    ReplyDelete
  10. endeleeni kushabikia kama mlivyozoea?

    ReplyDelete
  11. Kila mtu hata mijinga mjinga anaweza kuwa waziri katika nchi hii lakini si kila mtu anaweza kuwa daktari. Mponda na Nkya achieni ngazi maana ninyi damu za watu zi juu yenu! Tangazeni kujiuzulu. Rais na Waziri Mkuu hawatawazuia.

    ReplyDelete
  12. Mungu ibariki Tanzania, hivi kweli kazi za wito kama udaktari vinageuka kuwa kazi za kusababisha vifo vya watu wasio na hatia. Mko tayari kuona watu wanakufa kwajili ya kungangania kutolewa kwa Waziri. Hamjui nchi inaongozwa na sheria. Mwenyezi Mungu awahurumie, hamjui mtendalo.

    ReplyDelete
  13. uzalendo huku unaumwa njaa? sijaona!! hao walioshiba (wabunge, mawaziri) hawataki kugawa hata makombo yao kwa madaktari ili yaishe warudi kazini, wote tunakufa, wananchi tunakufa kwa kukosa huduma ya madaktari, madawa na vifaa vya tiba kutoka serikalini na madaktari wanakufa kwa mateso na njaa kwa mazingira duni ya kufanyia kazi na malipo kiduchu, kama na jeshi nalo litafikia hapo kama mchangiaji mmoja alivyouliza, hilo litakuwa si tatizo la madaktari bali serikali pumbavu, kama somo wamelipata kwa madaktari, kilichobaki ni kufaulu mtihani

    ReplyDelete
  14. KWELI HAWA MADAKTARI HATA AKIMALIZA MGOMO TUTAKUWA NA IMANI NAO HAPANA. KWELI MATAKWA YENU NI YA MSIGI LAKINI SI KUMUACHA MGONJWA ANATESEKA MPAKA KUFA ETI WAZIRI MPAKA AONDOKE MADARAKANI JE NI NANI MNAMTAKA AWE WAZIRI WENU? MUWE WASHAURI WA RAISI NI HAKI KWELI?

    ReplyDelete
  15. Eti kila mtu anaweza kuwa waziri lakini sio kila mtu anaweza kuwa Daktari...unachekesha kweli.

    Ujue kuwa kila mtu anaweza kuwa DOCTOR lakini sio kila Dokta anaweza kuwa Lawyer, Banker, Engineer, Accountant to mention a few.

    Msijifanye taaluma yenu ni bora kuliko za wengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...