Mkuu wa mkoa wa Tanga, luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa akifungua mkutano wa wadau wa mkonge uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa ambao ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wabunge wa mkoa wa Tanga.
Dkt Abdallah Kigoda mbunge wa Handeni ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Uchumi na fedha, akichangia kwenye mkutano huo ambapo alisema suala la wawekezaji waliochukua mashamba hayo serikali inatakiwa kuangalia kwa kina uwezo wao wa kuyaendeleza mashamba hayo ambapo tangu, wabinafsishiwe hadi leo wameweza kulima sehemu ya mashamba hayo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Katani Limited Bw. Salum Shamte akijaribu moja wa maswali yaliyokuwa yakiulizwa kwenye mkutano huo
Mbunge wa Korogwe Vijijini,Stephen Ngonyani 'Almaarufu Profesa Majimarefu' akirejea hoja yake aliyoisema bungeni Februari 3 mwaka huu wakati wa kikao cha 10 cha bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiitaka serikali kuwapa wananchi mashamba yaliyokuwa yakilimwa mkonge lakini wawekezaji hao kushindwa kuyaendeleza na kubaki pori hasa katika wilaya yake.
Wadau waliohudhuria mkutano huo kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Tanga, wakisikiliza kwa makini namna wajumbe wakichangia hoja za wawekezaji kuhusu zao hilo licha ya jitihada kubwa za serikali kuwawekea mazingira mazuri ya kilimo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...