Msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka matatu yakiwamo ya kutakatisha fedha haramu kosa ambalo halina dhamana kisheria na hivyo kurudishwa lupango.

Katika kesi hiyo, Kajala anashitakiwa pamoja na mumewe Faraji Mchambo ambapo makosa mengine ni kula njama na kubadilisha umiliki wa nyumba.

Wakili wa serikali Leonard Shayo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo alidai kuwa Kajala na mumewe wameshitakiwa kwa kosa la kwanza la kula njama kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 ambapo washtakiwa wote walitenda kosa hilo la kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam.

Shtaka la pili walidaiwa kuwa mnamo Aprili 14 2010 walihamisha umiliki wa nyumba hiyo kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.

Ambapo shtaka la tatu walidaiwa Aprili 14 2010 huku wakijua ni kinyume na sheria walifanya kosa la kutakatisha fedha haram ambapo ni kosa lisilo na dhamana kisheria .

Chambo hakuwepo mahakamani kwasababu yupo gerezani mahabusu kwa makosa mengine ambayo hayana dhamana yanayomkabili ya utakatishaji fedha.

Kajala alikana mashtaka hayo na kurudishwa rumande kwa uchungu mkubwa huku akilia pamoja na ndugu zake akiwamo mama yake aliyekuwepo mahakamani hapo.

hakimu Fimbo aliarisha kesi hiyo mpaka Aprili 20 mwaka huu ili kesi ije kwaajili ya kutajwa na pia kutolea maamuzi,maombi yaliyotolewa na wakili wa Alex Mgongolwa anayemtetea kajala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. KUTAKATISHA PESA NDIO NINI?MIMI MSHAMBA SIELEWI MAANA YAKE KWA KWELI.

    ReplyDelete
  2. kutakatisha hela maanake ni nini?

    ReplyDelete
  3. KUTAKATISHA FEDHA NDIO NINI?



    PIA MBONA MREMBO WA WATU YANAMKUTA MAKUBWA HIVYO?

    ReplyDelete
  4. Kutakatisha pesa ni money laundering kwa lugha ya kiingereza.

    ReplyDelete
  5. mtu anauliza kutakatisha fedha maana yake nini,jitu linasema Money laundering sasa ndo nini?
    Ila wabongo bwana sasa hapo tena anataka tuulize maana ya money laundering si ndio?
    Mpe jibu sahihi (wao mbona hawakusema money laundering?) ebo!

    ReplyDelete
  6. kwa kiswahili ndio nini hiyo "kutakatisha"

    ReplyDelete
  7. Sasa ametakatisha vipi? Mbona haijafafanuliwa?

    ReplyDelete
  8. Nielewavyo mimi, Kutakatisha fedha kwa lugha ya kiingereza (money laundering), ni kuchukua au kutumia fedha iliyopatikana kwa njia haramu (kwa mfano iliyopatikana kutokana na uuzaji wa madawa ya kulevya, uharamia n.k. kwa lugha nyepesi fedha chafu) na kuiingiza kwenye mfumo rasmi wa kibenki ili zionekane zimepatikana kihalali.

    Mara nyingi watu hao wenye mtandao mkubwa huwa na akaunti benki, pia biashara za kupotezea malengo kwa lugha ya watoto wa mjini (biashara za kuzuga); unaweza kuta anafanya biashara halali na biashara haramu (kisiri) kwa wakati mmoja bila watu kujua. unaweza kuta watu hao wanabiashara Fulani inayofahamika lakini

    Kwa vile nchi yetu tunatumia cash zaidi, hapa ndipo huchukua fedha ile iliyopatikana kwa njia halali (yaani biashara inayoonekana machoni mwa watu lakini anakuwa na biashara nyingine nyuma ya hiyo huionayo) na kuichanganya ile fedha iliyopatikana kwa njia haramu na kuzitakatisha (kuzisafisha) kwa kuziingiza kwenye mzunguko yaani mfumo rasmi, inaweza kuwa benki, kununua magari, nyumba n.k.

    Somo hili nilisoma zamani nakumbuka kwa mujibu wa sheria za wenzetu hakuna dhamana hapo. Kwani biashara hii haramu hasa ya madawa ya kulevya wana network (kama ile ya buibui) sasa hao wakitoka ina maana ushahidi wote utavurugwa ikumbukwe huo mtandao wa fedha chafu.

    Haya ni maoni yangu, kama kuna mtu anaelewa zaidi naomba atujuze.

    ReplyDelete
  9. Nielewavyo mimi, Kutakatisha fedha kwa lugha ya kiingereza (money laundering), ni kuchukua au kutumia fedha iliyopatikana kwa njia haramu (kwa mfano iliyopatikana kutokana na uuzaji wa madawa ya kulevya, uharamia n.k. kwa lugha nyepesi fedha chafu) na kuiingiza kwenye mfumo rasmi wa kibenki ili zionekane zimepatikana kihalali.

    Mara nyingi watu hao wenye mtandao mkubwa huwa na akaunti benki, pia biashara za kupotezea malengo kwa lugha ya watoto wa mjini (biashara za kuzuga); unaweza kuta anafanya biashara halali na biashara haramu (kisiri) kwa wakati mmoja bila watu kujua. unaweza kuta watu hao wanabiashara Fulani inayofahamika lakini

    Kwa vile nchi yetu tunatumia cash zaidi, hapa ndipo huchukua fedha ile iliyopatikana kwa njia halali (yaani biashara inayoonekana machoni mwa watu lakini anakuwa na biashara nyingine nyuma ya hiyo huionayo) na kuichanganya ile fedha iliyopatikana kwa njia haramu na kuzitakatisha (kuzisafisha) kwa kuziingiza kwenye mzunguko yaani mfumo rasmi, inaweza kuwa benki, kununua magari, nyumba n.k.

    Somo hili nilisoma zamani nakumbuka kwa mujibu wa sheria za wenzetu hakuna dhamana hapo. Kwani biashara hii haramu hasa ya madawa ya kulevya wana network (kama ile ya buibui) sasa hao wakitoka ina maana ushahidi wote utavurugwa ikumbukwe huo mtandao wa fedha chafu.

    Haya ni maoni yangu, kama kuna mtu anaelewa zaidi naomba atujuze.

    ReplyDelete
  10. mnafunga kisa kaafisha pesa jamani kama aliziona chafu ? kiswahili tabu kweli ,,, mithupu si ungesema tena anachapisha pesa bandia ...

    ReplyDelete
  11. safi sana ,hii iwe fundisho kwa wengine mjini mmnao fanya mambo kama hayo ma office , mwache ale rumande ya miaka hapo akitoka tuone hata hayo ma party ya kula bata kama atakuwa anauthuria tena,MUNGU IBARIKI TANZANIA
    MDAU PARIS

    ReplyDelete
  12. to make dirty money( drugs money, stolen in large quantities) clean, this is normally done by purchasing land, house etc and selling or renting.

    ReplyDelete
  13. ni kuchukua pesa bandia ukaanza kuzibadirisha na pesa halali,yaani hizo bandia ziingie kwenye mzunguko wa pesa nchini, jamani mambo mengini na nyie tumieni komoni sense zenu- sisi humu kwenye bloga siyo watoto wadogo wa chekechea -kamoni now !! Please. Zebedayo

    ReplyDelete
  14. Anonymous Fri16, 11.07:AM 2012

    Hata naona hatuelewani SI HELA BANDIA!!! Ni fedha halali ya Tanzania lakini inapatikana kwa kufanya biashara HARAMU. Naona nitumie mfano rahisi kama huu, wewe una biashara yako ya halali na umeisajili kisheria au duka lako la unauza bidhaa mbalimbali na inatambulika KISHERIA na tukija eneo lako tuona unaifanya ile biashara na imeshamiri kwelikweli KUMBE nyuma ya pazia si ile biashara kuna mambo mengine yanayoendelea ambayo yaweza kuwa ni biashara ya madawa ya kulevya, fedha haramu ulizozipa kwa njia za mishemishe, utapeli, fedha za wizi n.k. Sasa kwa kuwa ni nyingi unaogopa ukikutwa nazo ni SOO; unazichukua hela zako za haramu unachanganya na zile fedha ulizozipata kwa njia haramu unapeleka kwenye mfumo rasmi benki. Ukishaziingiza benki unaanza kutoa (kuwithdraw) kama fedha halali kwa mzunguko na wakati mwengine henda kununua madawa ya kulevya au kutoka kwenye ujambazi, utapeli, uharamia n.k. na mzunguko huo unaendelea kwa mtindo huo na kusafishwa kwa kuingizwa benki.

    ReplyDelete
  15. Tatizo la tafsiri za lugha, sidhani kama BAKITA wameshayasanifu na kuyapitisha maneno haya mawili ya kutakatisha fedha yakiwa na maana ya 'money loundering". Si kila tafsiri lazima iende sambamba na maneno ya lugha nyingine. Tafsiri sahihi ya money loundering nadhani ingekuwa 'pesa zipatikanazo kwa vyanzo haramu'
    lakini kutakatisha fedha haipendezi hata kidogo

    ReplyDelete
  16. kutakatisha fedha ni kujaribu kuzifanya za bandia ziweze kutumika kwenye mzunguko wa fedha halali wanatumia mpaka chemicals (not money laundering)

    ReplyDelete
  17. Ni kuchukua fedha iliyopatikana in a illegay ways like drug busnec,ufisadi,uhujumu,uharamia n etc then hiyo pasa unaamua kuiinvest like kujenga nyumba,kununua magari n etc ili ionekana ni legal!thats z a clear meaning ya hiyo kusafisha fedha chafu!

    ReplyDelete
  18. Mademu wa design hii wanaponzwa na waume zao, masikini. Hii kama ile ya Whitney Houston na Bobby Brown

    ReplyDelete
  19. Tamaa ya Utajiri, Maisha ya juu, Umaarufu na FEDHA INAWAPONZA WENGI DUNIANI!

    ReplyDelete
  20. huh! sasa wewe nawe ya Whitney Houston na Bobby Brown yanahusiana nini na hiyo story hapo juu...jamani huna cha kusema soma tu comments za wengine upite dont make fool of urself

    ReplyDelete
  21. Hivi kweli utamudu kujisaidia kwenye debe au ndoo?

    Badala ya kupanda juu ulikotegemea unajikuta unashushwa chini!

    Demu mzuri unakuwa na haraka na tamaa ya Utajiri,,,matokeo yake unapata Makazi ya bure Lupango!

    ReplyDelete
  22. Ni Bora kuwa Masikini Huru ukiwa Uraiani:::::KULIKO:::::kuwa Tajiri Mfungwa ukiwa Lupango!

    ReplyDelete
  23. Mkifuatwa kutaka Kuolewa na watu wenye Heshima zao mnakataa, mnaweka mapozi matokeo yake mnaangukia kwa Magalacha wa Magerezani!

    Afadhali yeye Mwanamke ana msala mmoja tu huu jamaa mumewe ana kesi juu ya kesi, sijui atachomoka vipi hapo?

    Eeee Mungu amsaidie!

    ReplyDelete
  24. Mbingwa wa Lupango wanamatumizi kama watoto wa Mabilionea!

    Utafikiri wana maghala ya Noti, au kama vile fedha haziishagi!

    Hawajui kuweka akiba kwa vile Bwana M-Pesa Vodacom ni watu wengine wanaotembea na hela zao kuwabebea wao, na muda wowote wakizitaka wanachukua!

    Hawa jamaa kwa Matanuzi yao, Ujiko ,kujiamini kupita kiasi na Maisha, maisha ya juu na matumizi makubwa,,,,na tamaa iliowajaa Mademu huwa hawakataliwi na Mademu!

    ReplyDelete
  25. Mademu wengi huwa wanaingia mitegoni mwa Mabingwa wa Misala kwa tamaa ya maisha ya juu, raha na starehe!

    Demu anakuja mtambua jamaa baadae mambo yamefyatuka anashangaa RB inatua na Pingu mkononi!

    ReplyDelete
  26. wengine mnachonga pumba tu ili mradi muonekane mmeongea....chuki binafsi zitawakondesha...na wengine hata kajala hamumjui....haya maisha bwana linalomkuta mwenzio leo... usijishaue kesho litakukuta ww hata kwa namna nyingine tofauti.Cha muhimu ni kuombeana dua tu....kila mtu ana maovu yake bwana...na sio wote wanaoenda jela wana hatia as a lawyer i know so......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...