Dr N T Jiwaji

Mandhari za kuvutia sana zitaonekana angani siku za Jumapili na Jumatatu tarehe 25 na 26 Machi, saa moja jioni baada tu ya Jua kuzama chini ya upeo wa Magharibi.

Sayari mbili zinazo n’gaa kwa ukali mkubwa, Zuhura na Sambula zitaungana na Mwezi mchanga hilali ambao utasogea kati ya sayari hizo mbili na kutoa maumbo ya kusisimua. Zuhuara inan’gaa mno wakati Sambula inan’gaa kwa ukali mdodo kidogo.

Picha inaonyesha Mwezi hilali ikiwa chini na kati ya sayari mbili hizo jioni ya siku hizo mbili. Siku inayofuata, Jumanne tarehe 27, Mwezi hilali utakuwa umepanda juu zaidi ya sayari mbili hizo.

Inafaa kukumbuka kwamba katika anga za juu, sayari na Mwezi zinakuwa na umbali mkubwa kati yao kwa hiyo hakuna uwezekano wa kuja jirani kiasi tunavyoziona kwa macho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Dr this is realy interesting I always love to see stars,so whenever you update us I make sure to spare some minutes and take tour of our beautiful gift from God.Thank you for your kind and free knowledge to us.

    ReplyDelete
  2. Daktari nashukuru sana kwa updates zako za kinajimu. Ningefurahi sana, kama ungekuwa na website ama blog yako, tuwe tunakutembelea kule ili kupata habari zaidi.

    ReplyDelete
  3. Nakushukuru sana kwa kutujuza hii habari,,kila ukituma mimi huwa nasubiri kwa hamu ili nikajifurahishe kuangalia mandhari hiyo nzuri kabisa,,
    Hivi na wanaokuwa katika mwezi Dunia huwa wanaiona kama tunavyoona mwezi na nyota angani?
    Kuliiza si ujinga.
    Na kama ndio,,kwa nini wanaosafiri kwenda mwezini wanasema Dunia wanaona ni giza tu,,Ila mama Mmmoja wa kihindi ndo alisema kuwa alipojaribu kuangalia Earth aliona,,Makkah sehemu ya Al-Qa'abah ndo inang'aa,lakini Dunia yote ilikuwa Darkness,,,(She is a christian)

    Ahlam,,,UK

    ReplyDelete
  4. Ninashukuru sana kwamba watu wana sisimuliwa na maelezo ya angani kwani ndiyo kivutio kimoja muhimu kwa watu kuelewa kwa undani na kisayansi hali ya Ulimwengu wetu.

    Ni kweli kwamba tutaiona Dunia kutoka Mwezini kama vile tunavyouona Mwezi kutoka hapa Duniani, ila Dunia itaonekana jibes mara karibu nne kuliko tunavyouona Mwezi kwa vile tufe ya Dunia ina upenyo mkubwa mara 3.6 kulko Mwezi.

    Kuna website ya Astronomia hapa Tanzania

    http://sites.google.com/site/astronomyintanzania/

    ambapo utapata maelezo mengi kuhusu maendeleo na taarifa kuhusu mambo ya angani hapa Tanzania.

    Dr N T Jiwaji

    ReplyDelete
  5. We mdau wa tatu acha udini wewe, umeanza kuandika vizuri mwishoni ukaboronga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...