Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bwana Longinus Rutasitara akila kiapo mbele ya Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wapili kushoto anayeshuhudia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na watatu kushoto ni Karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimrekebisha koti Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bwana Longinus Rutasitara muda mfupi baada ya kumuapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi .Kulia ni Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal aliyehudhuria hafla hiyo.(picha na Freddy Maro).
Jamaa kanifundisha UD huyo, nafikiri amesoma in excessive mpaka ukikutana nae kwa mara ya kwanza kama humjui unaweza sema katoka kanyigo leo. Ila upstairs yupo makini sana hasa kwenye uchumi.
ReplyDeleteWaheshimiwa wanafundishwa utaratibu wa kuvaa suti. Ukisimama unafunga vifungo sio kuacha koti lina pepea. Ukikaa unafungua vifungo sio una acha koti lina kubana tumbo...
ReplyDeleteNimesha ona mara nyingi Mh Rais akiwasawazisha waheshimwa katika vazi la suti ama koti au tai...
Jamani ube harakisheni tupate vazi la Taifa, ya mambo ya kuiga yanatushinda.
Ni Dr. Longinus Rutasitara.
ReplyDeleteInapendeza sana kuona Mhe Rais anajali umakini wa kuvaa..
ReplyDeleteWith all due respect kwa kila mtu, nafikiri Ikulu yetu inatakiwa kuangalia tena ratiba ya Rais wetu.
ReplyDeleteHizi shughuli za kuapisha maafisa kama hawa zinatakiwa zifanywe na makamu wa Rais bwana. C'mon, this doesn't diminish the position or the person being appointed ila my view is the president should contentrate on policies implementation and not trivial issues.
Mara mkutano wa usafi wa vinywa, mara mkutano wa watu wenye uremavu wa masikio.. kweli kweli, barabara mbovu, hatuna maji, nchi giza, tax codes hazieleweki.
my 2 cents.
NI daktari PhD.Economics yupo fiti sana. AMENIFUNDISHA ECONOMICS UDSM.
ReplyDeleteHONGERA SANA DR.RUTA
barabara mbovu yeye akajenge??
ReplyDeleteDr. Jk usipate tabu kulazimisha kufunga vifungo vya hilo koti la Dr. Ruta kwani ni dogo.
ReplyDeleteCongratulations Dr. Kijana wangu. Uwaziri huo unakutembela. Ni kijana mzuri sana makini, sio mlevi kama walimu wengi vijana wa CKD.
ReplyDeleteNamuunga sana mkono anonymous wa Thu Mar 15, 06:16:00 PM 2012...
ReplyDeleteRais wetu stimes anaonekana kama vile hana cha kufanya kisera. Mara nyingi aonekana akifanya vitu ambavyo honestly havijengi kikazi.
We unayeuliza akajenge barabara mbovu, nafikiri unakuwa na ufinyu wa mawazo wa kushindwa kuunganisha hivyo vitu viwili.
I don't normally like JK, lakini hiyo picha ya tatu imenifanya nimeone ni mtu poa sana. That looks really original and makes him a caring guy. Big up JK!
ReplyDeleteHuyo ni DR. Longinus Rutasitara, siyo sahihi kumuita BWANA. Amewahi kuwa Mkuu wa Idara ya Uchumi UDSM na mwaka 2010 aliteuliwa kuwa Deputy Principal Academic, College of Arts and Social Sciences (CASS). MZEE Wa Ankali, badilisha hiyo title yake tafadhali.
ReplyDeleteOhhh Usomi sio mchezo Jamaa amepiga kitabu hadi kufunga Koti vizuri hana muda!
ReplyDeleteMara nyingi mtu akiwa Msomi wa kupindukia anakuwa hana muda wa Usmati akili yake anawaza Taaluma zaidi kuliko muonekano!
Kuitwa kuapishwa na Raisi sio Mchaezo Dr. amekurupuka nyumbani kwake Chuo Kikuu Dar Es Salaam bila kukumbuka kama Koti lake amefunga vifungo vizuri!
ReplyDeleteSawa Dr. L. Lutasitara kaa na Mkubwa JK na uhakikishe unatoa Ushauri mzuri kwake dhidi ya Wanasiasa waliomzunguka ili Uchumi wetu uimarike na kuwa nafasi nzuri ktk kipindi hiki cha Ushindani ktk Jumuia ya Afrika ya Mashariki na Duniani!
ReplyDeleteDr. Lutasitara,
ReplyDeleteJUKUMU NI LAKO SASA:
Mwelekeze Mhe. Raisi jinsi tutakavyotumia wingi wa Rasilimali zetu tulizojaaliwa ili kuunusuru Uchumi wetu.
Mweleze kitaalamu kuwa 'uchumi wa Mafuta na Utegemezi wa Kodi ya Mafuta' ndio Mchawi wetu mkubwa ktk maendeleo ya Kiuchumi.
Pana umuhimu tukabadili mwelekeo kama nchi moja ndogo sana jirani Rwanda ilivyofanya, imepunguza sana Kodi ya Mafuta na Kuimarisha sekta zingine za Pato la Taifa na sasa inaendelea vizuri sana.
Sasa sisi tuna uwezekano Mkubwa sana kwa mali NYINGI tulizo nazo:
-ALMASI
-GESI ASILIA
-DHAHABU
-TANZANITE, NA GEMS ZINGINE
-CHUMA NA MAKAA YA MAWE
-URANI
-MISITU NA MALIASILI
-BAHARI NA MAZAO YAKE
-ARDHI
-RASILIMALI WATU (MAELFU YA WATAALAMU WA KILA KADA MADIASPORA WAKIWA UGHAIBUNI)
Tukafikia lengo la ''MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA KABLA YA 2015 MHE. JK ATAKAPOTUAGA NA KUTIMIZA AHADI NA ZAWADI YAKE KWETU TUKAMKUMBUKA DAIMA!