"Jamii ijenge utaratibu wa kuchunguza afya zao kila mara, kama ambavyo wengi wenye magari wafanyavyo, kwa kupeleka ‘service’ magari yao ....... Mbona tunajali zaidi magari yetu? Utasikia mtu anasema napeleka gari ‘service’ limeshatembea kilomita 3,000, lakini mtu huyu hajawahi kwenda ‘service’ ya afya yake” 
Dk. Mzige - HabariLeo 16 March 2012.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. watanzania wengi hatuna utamaduni wa kuchek afya zetu na ndio maana mtu anaugua gfla na kupoteza maisha. inabidi watu wapewe elimu ya kutosha kuhusu kuchek afya zao mara kwa mara. kwa upande mwingine uchumi sio mzuri kiasi kwamba watu hawana kipato cha kutosheleza kufanya chek up ya afya zao

    ReplyDelete
  2. Kufanya checkup ya afya ndiyo kufanya nini?

    ReplyDelete
  3. check up ya afya,shinikizo la damu, uzito na Body Mass Index, kupima damu- sukari(Glucose), cholesterol,haemoglobin, mafigo(U&E), ini(LFT), elimu ya afya kama una vuta sigara au unafakamika mapombe,mazoezi, elimu ya mlo- siyo kiti moto tu,kula pia matunda, mboga za majani nk, aka balanced diet, etc.
    "prevention is better, and indeed cheaper than cure"

    ReplyDelete
  4. Mdau wa kwanza Anonymous wa Fri Mar 16, 01:38:00 PM 2012

    Uchumi sio mzuri ku chek afya?

    1.Mbona Mabaa na Pubs yanajaa?
    2.Gharama ya Ku service gari na gharama ya ku check afya ipi zaidi ni ghali?

    UJAMAA ULITULEMAZA KWA MATIBABU YA BURE MPAKA SASA WATU KILA KITU WANANGOJA WAFANYIWE NA SERIKALI.

    HII NI HULKA YA UZEMBE NA KUTOKUWA MAKINI KTK MUDA TULIKUWA NAO TU!

    ReplyDelete
  5. Ohhh

    Vipimo vyote watu wapo tayari ila kipimo cha Ukimwi wachache ndio wapo tayari kupima na pia utayari wa kupokea majibu.

    Rekodi inaonyesha kati ya waliopima waliochukua majibu yao hasa ya Ukimwi ni wachache sana wengi wamekula kona!

    Wengi wanaishi kwa 'matarajio' kama sio 'matumaini' wanaogopa kupima kwa kuhofia wasiwasi kama tayari wameshaumia!

    ReplyDelete
  6. Hofu ya maisha ndio tatizo!

    ReplyDelete
  7. Ahhh ni Hulka mbaya na mazoea mabaya sisi watu kutojali na kutazamia mara kwa mara afya zetu.

    Unakuta Gharama za upuuzi afanyazo mtu ni nyingi kuliko Gharama za kutazamia afya yako na familia yako.

    Huku unakuta watu wanatumia gharama kubwa sana kwa starehe za ajabu na anasa zisizokuwa na maana kama Ulevi, Matumizi mabovu, Sherehe zisizo na mpango wowote, Nyumba ndogo na Mahawara kwa upande wa Wanawake wapo wanaoacha kuhudumia familia zao na kujijali wao kiafya wanahonga Mabwana!

    ReplyDelete
  8. Mtanzania 'nyoko' sana unakuta mtu analewa malaki kwa mamilioni ya Shilingi tena na watu baki sio na familia yake, lakini kutazama afya yake au ya familia yake kwa elfu 30 au 40 anaona ghali sana!

    ReplyDelete
  9. Wabongo ni bahili sana wa masuala muhimu ya maisha zaidi ya kucheki Afya zao!

    Mfano :

    -Unakuta mtu ana gari la mamilioni lakini Bima imekufa muda mrefu tu yeye anaendesha gari kwa bahati bahati tu,

    -Unakuta mtu ananunua gari kwa mamilioni ya pesa, wakati akiwa hata akiba Benki hana wala hela ya mafuta kwa gari lake pia mgogoro!,

    -Unakuta mtu anamiliki gari la maana kabisa lakini muda wa Lunch (chakula cha Mchana) anabonyea/ anakula kwa Mama ntilie!

    ReplyDelete
  10. Wabongo ni bahili sana wa masuala muhimu ya maisha zaidi ya kucheki Afya zao!

    Mfano :

    -Unakuta mtu ana gari la mamilioni lakini Bima imekufa muda mrefu tu yeye anaendesha gari kwa bahati bahati tu,

    -Unakuta mtu ananunua gari kwa mamilioni ya pesa, wakati akiwa hata akiba Benki hana wala hela ya mafuta kwa gari lake pia mgogoro!,

    -Unakuta mtu anamiliki gari la maana kabisa lakini muda wa Lunch (chakula cha Mchana) anabonyea/ anakula kwa Mama ntilie!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...