Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo ameagana na mabalozi wapya watatu watakaoiwakilisha Tanzania nchi za nje.Mabalozi waliokwenda ikulu kumuaga Rais Kikwete ni pamoja na Dkt.James Msekela anayekwenda Italia, Dkt.Ladislaus Komba anayekwenda Uganda na Mhe.Bi.Shamim Nyanduga anayekwenda Msumbiji. Pichani Rais Kikwete akizungumza na Balozi Mpya wa Tanzania nchini Italia Dkt.James Msekela ikulu jijini Dar es Salaam leo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Uganda,Dkt.Ladislaus Komba ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi Mpya wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe. Shamim Nyanduga ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.
yaani siku hizi mtu akichaguliwa balozi then anaanza ziara ya miezi sita kuaga?? Guys, Serikali haina hela jamani hebu acheni kuleta mzaha!!
ReplyDeleteChe
Huyu Che katoka wapi? Anaonyesha ujinga wake wa diplomasia. Diplomasia lazima izingatie hali ya nyumbani anapotoka mwanadiplomasia, hivyo lazoma kumfunda kabla hajaenda huko anapotumwa ili akiongelea kilimo anajua hali yetu na mahitaji yake, akiongelea ajira anajua hali ya vijana wetu, vile vile utalii. Kila kitu sharti uwekeze kwanza ili wanadiplomasia wako wawe mahiri na makini!!
ReplyDeletebalozi hutumikia kipindi cha miaka 4.baada ya hapo anaweza kuongezewa. sasa hawa miezi 6 tayari wametumia hapa nyumbani. je, utumishi wao utahesabika tangu wameteuliwa au tangu wafike ktk vituo vya kazi?
ReplyDelete