Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmshauri kuu ya CCM ikulu jijini Dare s Salaam leo mchana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Sielewi maana ya Mhe. Kikwete kufanyia kikao cha chama Ikulu, sehemu ambayo ni ya umma na Rais siyo wa Chama bali wa Watanzania wote. Je, Chadema wakiomba ukumbi kufanya kikao chao Ikulu watapewa?, Je CUF, SAU, NCCR-Mageuzi nao watapewa nafasi hiyo ya kufanyia kikao IKULU?

    Natafakari ila sielewi kabisa. Hivi CCM wamefikia hatua ya kufanyia vikao vya chama IKULU?

    ReplyDelete
  2. Ni haki kuendesha vikao vya chama Ikulu!! Gharama hizo nani analipia au ni hela kutoka serikalini!! Ufisadi wa mali za walipa kodi ambazo zinatokana na wananchi wenye itikadi tofauti!!

    ReplyDelete
  3. mimi sijswahi kusikia conservative wala labour kufannya kufanya vikao vyao downing street. ikulu si sehemu ya ushabiki wa vyama. ni ofisi ya serikali.

    ReplyDelete
  4. chadema au nccr na wao wakitaka wafanyie vikao vyao ikulu mtasema nini? vyama vya siasa hukutana katika ofisi za vyama. ikulu ni ofisi ya watanzania wote, wenye vyama na wasiokuwa na vyama.

    ReplyDelete
  5. ..sasa mlitaka kifanyike kwenu..!

    ReplyDelete
  6. Unajua mm huwa nashangaa sana hii nchi inavyoendeshwa.Hivi hawajamaa hawaelewi au ni viburi tu?

    ReplyDelete
  7. Public fund wanatumia ,

    ReplyDelete
  8. Hata mm niliwahi kujiulza kuhusu jambo hili katika habari kama hii iliyopita majuma kadhaa.

    Nadhani ipo haja ya kurejesha ofisi au matawi ya chama katika taasisi za serikali. Na tukirejesha taasisi zitatenda kazi zake ama uchama ndio kazi.

    ReplyDelete
  9. CCM ni chama tawala. Kina wajibu wa kuisimamia serikali. Ikulu ni sehemu ya serikali. Sasa sioni tatizo kufanyia vikao ikulu, kwani CCM ni watawala. Ikulu wanaisimamia wao. CHADEMA, CUF na vinginevyo, vitaweza kufanyia vikao ikulu kama tu vitashika dola. Maana kamati kuu itaenda ikulu kuweka mikakati ya kiuongozi ili kutekeleza sera kwa mjibu wa ilani ya uchaguzi

    ReplyDelete
  10. Kuna baadhi ya malalamiko yakiendekezwa Rais atakuwa hafanyi kazi.
    Rais akifanyia vikao Ikulu, oooooh mbona kafanyia Ikulu; akienda kufanyia vikao Lumumba, ooooooooh mbona Rais anasababisha foleni.
    Ni vigumu sana kujua mnachotaka.
    Kumbukeni kuwa Ikulu ni ofisi na makazi ya Rais, kipindi cha urais siyo kwamba maisha yanasimama. Halafu kumbukeni pia kuwa chuki binafsi siyo lazima kila wakati meiexpress...Zemarcopolo!

    ReplyDelete
  11. issue hapa sio CCM kuwa chama tawala bali ni kutumia pesa za walipa kodi wa Tanzania kuendeshea mikutano yao.ikulu nimakao makuu ya serikali na SIO ukumbi wa CCM wakufanyia mikutano.

    ReplyDelete
  12. issue hapa sio CCM kuwa chama tawala bali ni kutumia pesa za walipa kodi wa Tanzania kuendeshea mikutano yao.ikulu nimakao makuu ya serikali na SIO ukumbi wa CCM wakufanyia mikutano.

    ReplyDelete
  13. Kidumu Chama Cha Mapinduzi..!!

    ReplyDelete
  14. Siyo suala la chuki binafsi ni suala la makazi ya nchi ( state house) kutumiwa vibaya na viongozi wa chama...hakuna sheria yoyote duniani labda TZ inayoruhusu mambo ya chama kujadiliwa state house. Ikulu ni jumba la watanzania wote ambao wana itikadi tofauti za kisiasa. Viongozi wa vyama vyote including mwenyekiti wa chama wanatakiwa wafanye vikao vyao kwenye ofisi zao siyo kwenye nyumba ya serikali.

    ReplyDelete
  15. mimi sijswahi kusikia conservative wala labour kufannya kufanya vikao vyao downing street. ikulu si sehemu ya ushabiki wa vyama. ni ofisi ya serikali.

    Mdau uliondika hivyo.....wewe mambo ya number ya namba 10 atakwambia nani? Ulaya hawana siasa za kishabiki na kitu kama hicho ni very trivial it won't even be written on the papers, kwa hiyo usilinganishe nchi zilizoendelea ambapo kwao everything is in place hawana kingine cha kufanya wanafikiria ni jinsi gani mume na mume wakaona au mke kwa mke vitu ambavyo kwetu sisi havina tija.

    ReplyDelete
  16. Lazima tutofautishe 'chama' na 'serikali'. Raisi ameapishwa kytumikia serikali na sio chama chake. Mikutano ya chama ifanyike katika ofisi za chama, ikulu iwe ni sehemu ya serikali. Mbona Watanzania wengine inawawia vigumu kuelewa hicho? Au bado ni ile kasumba ya 'chama kushika hatamu' bado imewajaa vichwani. Katiba mpya lazima iweke bayana mipaka ya chama na serikali. Vilevile elimu ya uraia iboreshwe ili kila mwananchi ajue nchi yake inavyotakiwa kuendeshwa. Kukazania kufanyia mikutano ya chama ikulu ni jeuri dhahiri ya viongozi hao. Tabia hii inahitajiwa kukomeshwa mara moja!

    ReplyDelete
  17. Jamani provided kwamba CCM ndio chama kilichoshika dola basi they are absolutely correct kufanyia vikao vyao humo. Sasa cha msingi sisi wananchi tusubiri muda wa CHADEMA au ADC or any other opposition parties to win the election ili nao waonje upepo wa kutokea baharini hapo ikulu. Labda pengine muda huu utakapofika kwao(though not in my lifetime)hili zogo litamalizika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...