MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope (pichani) naye atakuwa miongoni mwa waimbaji watakaopamba tamasha la nyimbo za Injili litakalofanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu tamasha hilo chini ya Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam, Alex Msama, alisema Rebecca amethibitisha kushiriki tamasha hilo.

Msama alisema Rebecca ataungana na waimbaji wa muziki wa Injili kutoka nchi jirani za Zambia, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia na Congo (DRC), Rwanda na Uganda.

Malope atakuwa mmoja kati waimbaji siku hiyo wakiwemo Rose Muhando, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Ephraim Sekeleti, Anastazia Mukabwa, Atosha Kissava na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival inayotamba na albamu yao mpya ya Mtu wa Nne, inatarajia kutumbuiza katika tamasha la Pasaka na Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka DRC.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Baada ya kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu.

"Katika tamasha la Pasaka mwaka huu, Rebecca Malope atapata fursa ya kuimba nyimbo mbalimbali zilizomo kwenye albamu zake," alisema Msama.

Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).

"Bado tunaendelea na mazungumzo na waimbaji wengine mahiri wa muziki wa Injili, lakini Rebecca atakuwepo akishirikiana na wengine mahiri kama Rose Muhando, Solomon Mukubwa na wengineo," alisema Msama.

Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.

Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.

Rebecca Malope ni mwimbaji nguli wa Afrika Kusini aliyetamba zaidi kimataifa mwishoni mwa miaka ya 90.

Malope alizaliwa katika shamba la tumbaku Afrika Kusini. Akiwa mtoto, yeye na dada zake walikuwa wakiimba kwaya kanisani.

Alijiunga na kundi la muziki wa injili akiwa binti mwenye umri mdogo, jijini Johannesburg, chini ya mtozi, Zizwe Zakho.

Alianza kutoa albamu yake ya kwanza aliyoipeleka Marekani mwaka 1996 na mwaka uliofuata alisaini mkataba na EMI kisha akatoa albamu ya Free At Last. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. hayo matiti inakuwaje na kumsifia mungu? naona siku hizi kila mtu anaonesha matiti yake hata watu wa dini nao wameingia katika wimbi hili.

    ReplyDelete
  2. Karibu sana Rebeca TZ.

    ReplyDelete
  3. Sad!! what our kids are learning from this type of behaviour? this is not acceptable in society.

    ReplyDelete
  4. Mnaolalamika ndyo wenye matatizo. Hata anyevaa hijab na baibui bado mngeatafuta la kusema

    ReplyDelete
  5. Wabongo wana tabia ya kuhukumu watu, wanajiona kuwa wao wako sahihi sana na wasio na dhambi, kama hapa tayari wameona wengine wanadhambi.
    Siku ya kiama utashangaa hao mnaowahukumu kukwakuta mbinguni na ninyi.......
    Acheni mambo ya kuhukumu, kila jamii inautamaduni wake, na mavazi sio kigezo cha wema.
    Pia ikumbukwe muimbaji injili ni kama mtu mwingine tu, binadamu kama wewe.
    Be HUMBLE!!!

    ReplyDelete
  6. Ni kweli hatupaswi kuhukumu. Na ni kweli mwimbaji wa injili ni watu km wengine bt wanatakiwa kuonyesha mfano coz wao ni nuru ya ulimwengu. Na tuliambiwa wale tusifwatishe namana ya dunia hii. Watu wa duniani wavaa hivyo na wa Mungu pia?

    ReplyDelete
  7. Malope atakuja kweli jamani au maana Msama anatangazaga list ndefu halafu anaishia kutuletea watu hawaeleweki, any way tusiongee sana tusijeingia kwenye dhambi bure, sisi kama wapenda gospel Music hapa bongo tunaomba sana akija tumuone kwenye press conference ili tuwe na uhakika sio kutuambilia hewani, habari ndio hiyo Kaka Alex natumaini utapita kuona comments za wadau humu; tunaomba hayo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...