Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Mh. Ally Hassan Mwinyi (kushoto) na Mkewe Mama Sitti Mwinyi (katikati) wakiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia) pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa (kulia) kabla ya kuanza safari ya kuelekea kwenye Sherehe ya Kuzinduliwa kwa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo,Muhashamu Salitaris Melchior Libena iliyofanyika leo Ifakara,Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara,Muhashamu Salitaris Melchior Libena akiongoza ibada yake ya kwanza akiwa ni Askofu wa Jimbo Jipya la Ifakara mara baada ya kusimikwa leo.Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara,Muhashamu Salitaris Melchior Libena akitoa baraka zake kwa Viongozi wa Serikali waliohudhulia Sherehe hizo za kusimikwa kwake leo. Picha zaidi BOFYA HAPA
Home
Unlabelled
Sherehe za Kusimikwa Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





Mola aendelee hivi hivi kutupa moyo wa kupendana wakristo na waislam Tanzania na yeyote asieelewa umuhimu wa upendo huu aiangalie Nigeria. Mimi ni mwislamu na nafurahi sana kumuona kiongozi wa zamani (MWISLAMU) akihudhuria shughuli kama hii.Naelewa vizuri kuna wenzangu wenye misimamo mikali wataniona mimi kama si mwislamu kamili lakini hivi ndivyo mafunzo halisi ya dini zote yanavyotwambia TUPENDANE NA KILA MMOJA AENDELEE KUAMINI DINI AITAKAYO. Narudia tena kama kuna mtu asiyeelewa umuhimu wa upendo kati ya dini zetu kuu mbili AIANGALIE NIGERIA WANAVYOUANA HOVYO KWA VISINGIZIO VYA DINI. Mola awe nasi daima na azidi kutufungua macho na kutulinda Amen
ReplyDeleteWaandishi wa habari kuweni wapembuzi wa kina katika kuandika habari. Jimbo jipya la Ifakara si jimbo kuu bali ni jimbo lililo ndani ya ukanda wa jimbo kuu la Dar es Salaam. kwa mantiki hiyo huyo Askofu mpya si Askofu Mkuu bali ni askofu. Katika hierarikia ya Kanisa tuna maaskofu wakuu watano ambao ni wasimamizi wa majimbo makuu matano ya Dar es Salaam, Tabora, Songea, Mwanza na Arusha.
ReplyDeleteMBONA KAMA KUNAMCHANGIAJI HAPO JUU,KAONGEA BUSARA ILIYOPITILIZA.NARUDIA.BUSARA ILIYOPITILIZA.NAMI MKRISTO NAKUUNGA 180 PERCENT.MOLA AKUZIDISJIE,KWANI HATUTAKUWA NA MUDA KAMA HUU WAKUTUMA HATA HAYA MAONI PAKINUKA!
ReplyDeletesimon
Hakika ni kwamba kuna mipaka ya upendo miongoni mwa watu wa dini na imani tofauti na si lazima ku'SHIRIKI' katika ibada. ndio maana huwezi hata siku moja kumuona asiyekuwa muislamu ndani ya msikiti, sababu ndio hiyo hiyo mipaka ya upendo. Uadui katika tofauti za kidini nakubali kwamba upo na si Nigeria tu bali hata hapa Tanzania, Ireland na mfano wa karibuni sana ni huko Ufaransa ambako wasiokuwa Wakatoliki hawatakiwi na kundi fulani hadi kusababisha kuuliwa kwa wale Wayahudi na kabla yake Wanajeshi Waafrika watatu ambao wameuawa kwa rangi na hisia za uislamu wao.
ReplyDeleteHata hivyo, bado kuna njia nyingi za kudumisha maelewano mbali na kuhudhuria katika matendo ya imani isiyokuwa ya mtu dini yake.
wewe mwislamu mwenzangu hongera sana watu kinacho wasumbua ni ulimbukeni dini sio kudharauliana dini ni kuheshimiana, kupendana,kusaidiana safi kabisa huyo atakaye kuona eti sio mwisilamu kamili yeye ndiye asiyekamili
ReplyDeleteMTOA MADA WA KWANZA,NAKUSHUKURU SANA KWA KULIONA HILO,HAINA HAJA YA KUGOMBANA WALA KUTUKANANA,SIE WOTE BINADAMU BALI DINI TOFAUTI,DINI ZETU ZITUSIFANYE KUTOPATANA.....
ReplyDeleteMiongoni mwa Ustaarabu ni Kuthamini Imani ya mwenzio na sio kuibeza na kuidharau.
ReplyDeleteMARA ZOTE MATATIZO KTK DUNIA NA MIFARAKANO KTK JAMII ZETU INATOKANA NA WATU WACHACHE (Mfano pana watakaoona picha hiyo na taarifa hii na kukurupuka kutoa Maoni potofu) WANAOTUMIA UTENGANISHI NA UCHOCHEZI KWA MISINGI YA IMANI / DINI ILI KUFIKIA LENGO LAO CHAFU.
LAKINI UKICHUNGUZA KWA MAKINI UTAONA KUNA DALILI YA SIASA FULANI NDANI YAKE AMBAZO NDIO UNAKUWA NDIO SIRI AU MHIMILI WA SUALA ZIMA.
SASA KTK HADITH NA HISTORIA YA UISLAMU TUNAONA MTUME MUHAMMAD S.A.W ALIWAHI KUISHI NA JAMII ZA WASIO WAISLAMU (MANASWARA NA MAYAHUDI) HUKU AKIWA YEYE NDIO MTAWALA WA DOLA KTK MIJI YA MAKKA NA MADINA HUKU AKIHESHIMIANA NAO, AKIHESHIMU IMANI ZAO NA KUSHIRIKIANA NAO KTK MAISHA!
DINI INATAKA BUSARA HEKIMA NA USTAARABU ZAIDI KULIKO JAZBA!
Mola ajalie tuendeleze umoja wetu ,undugu wetu,ujirani wetu.
ReplyDeleteWachangiaji wote Mungu awalinde na awape upendo zaidi baina yenu.
Tanzania ni moja ,watu wake wamoja,asili yetu moja,na tukigombana ujue tunagombana ndugu kwa ndugu.
Wazee wetu mnaowaona hapo wanatupa mifano hai.Dini zituunganishe na kamwe zisitugonganishe.
Mungu Ibariki Tanzania,Mungu wabariki Watanzania.
Wote sisi ni kitu kimoja...wenu mpenda amani kupitiliza.
ReplyDeleteNi vema wale waislam wenye msimamo mkali wanaotukana wasio waislam kwenye radio, wakajifunza hapa. Sisi sote ni ndugu hakuna haja ya matusi, binafsi naamini kuwa wanajiongezea uadui kati yao na mungu. Mungu anapenda upendo na ustaarabu.
ReplyDeleteNimempenda mdau wa kwanza Mungu akulinde na akuongezee na kukutimizia haja za moyo wako, kwa ushauri wa busara ulotupa wadau wenzako.
ReplyDelete