MAREHEMU MATHIAS TANGANYIKA NZWILA
Alizaliwa Amefariki
24/04/1964 08/03/2011
Familia ya Ndugu TANGANYIKA iliyopo calfonia Nyegezi Mwanza inapenda kutoa shukrani zao za dhati kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki na wale wote walioshirikiana nao katika kipindi chote cha majozi ya kufiwa na Baba yao mpendwa MATHIAS TANGANYIKA NZWILA aliyefariki tarehe 08/03/2011 huko BUGANDO – MWANZA na baadaye kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika Nyumbani kwao NYAMENGELE – KWIMBA.
Kwa vile siyo rahisi, kumshukuru kila mmoja, tunapenda mpokee shukrani zetu kwa moyo mkunjufu. Hatuna cha kuwalipa, ila Mungu awabariki na kuwazidishia moyo wa ushirikiano na upendo.
AMEN
Poleni sana, sasa hpa sijaelewa vizuri. Hii ni kumbukumbu ya baba yetu ama ni msiba? maana tarehe ya kuzikwa inanichanganya na maelezo ya shukrani.
ReplyDelete