Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kuwafahamisha Watanzania waliopo Mali kujiandikisha Wizarani kupitia email zifuatazo nje@foreign.go.tz au info@foreign.go.tz. Wakati wa kujiandisha, tafadhali toa taarifa muhimu kuhusu Jina kamili, Umri wako,namba ya hati yako ya Kusafilia,mahali ulipo nchini Mali pamoja na simu na barua pepe yako.
Aidha Wizara inapenda kuwashauri Watanzania popote walipo kutosafiri kwenda nchini Mali kwa kipindi hiki kutokana na kufungwa kwa mipaka ya nchi hiyo baada ya Kikundi cha Wanajeshi kupindua Serikali ya nchi hiyo na hivyo kusababisha mipaka yote pamoja na Viwanja vya ndege kufungwa.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
kama kweli hili tangazo ni la serikali basi pongezi sana sana sana kwa kuwajali raia wake.kwa kweli yahitajika pongezi kwa kuamua kuhakikisha raia wake wako salama..lakini nina wasiwasi kidogo na tangazo hili maana matangazo yote ya serikali yanakuwa na nembo ya taifa, vipi kuhusu hili na ukizingatia ni suala nyeti sana.
ReplyDeleteahsante
Wewe mtoa maoni wa kwanza usiwe kama wamasai ambao walikata-kataa kabisa kuokoka, kisa mchungaji aliwambia watakapokuwa walokole, siku watakapokufa hawataenda motoni, wataenda peponi ambako hakuna moto. Wao wakachukia, kwa kusema kama peponi hakuna moto, je, mahindi yao watachomea wapi??
ReplyDeleteSasa taarifa kukosa nembo si tatizo. Maana taarifa kamili inakuwepo, lakini uenda wakati wa kuingizwa kwenye blog, ikachukuliwa taarifa yenyewe, 'header' ikaachwa. Elewa unachokiona na kuambiwa, usihoji saana kwa usivyoviona
serikali yetu ina matatizo sana kuna watanzania wapo ugiriki wanaomba msaada wa kurudishwa nyumbani serikali ya bongo imekaa kimya sasa wanatangaza kuitoa msaada kwa watanzania wanaoishi Mali wakati wanajua kwamba hakuna mtanzania anayeishi MALI
ReplyDeleteMtoa maoni wa tatu unakosea sana!!! Nani kakuambia kuwa hakuna mtanzania anayeishi Mali? Tupo watanzania wengi sana huku ila tu ni kwamba nchi yetu haina ubalozi hapa bado.
ReplyDeleteTunashukuru sana brother Michuzi kwa kutuwekea tangazo hili; nimeshawaandikia e-mail wizara na kuwataarifu wenzangu wengi ili wajiandikishe pia.
Idumu Daima blogu yetu ya jamii; na tuzidi kuombeana ili turejee salam salmini nchini kwetu; Amina!!
Nawashukuru wote waliotoa mawazo yao kuhusu statement yetu ya kuwataka Watanzania walioko Mali wajiandikishe. Tumefanya hivyo kwa wenzetu waliokuwa Libya tukawarejesha Watanzania 9. Tulifanya pia kwa nchi za Egypt,Tunisia na tumefanya hivyohivyo Ugiriki.
ReplyDeletekwa taarifa yenu kuna Mtanzania ambaye tulipata taarifa zake kwamba amekwama hotelinu Mali tayari taratibu zimefanyika anatarajiwa kufika Nairobi leo.
Wizara inarejea Mwito wake kuwataka Watanzania kila wanaposafiri nje ya nchi kukumbuka kujiandikisaha kwenye ubalozi wetu wa karibu ili kurahisisha mipango ya kuwaokoa matatizo yanapotokea.
Assah Mwambene
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mdau ukitaka kuhakikisha kama ni e-mail ya Serikali wewe angalia 'Domain' yaani mwisho wake unaashiria ni taasisi ya Serikali tena ya Tanzania.
ReplyDeleteMfano hapo E-mail:nje@foreign.go.tz
Ukichukuwa baada ya alama @ hiyo foreign.go.tz anzia na www.foreign.go.tz utaona ni tovuti ya Wizara ya mambo ya nje Tanzania inafunguka.
Tumia mbinu hii kuzibaini hata tovuti za wajanja Matapeli utawabaini tu...hata siku moja Taasisi Makini au Mamlaka haiwezi kutumia e-mail ya biashara kama gmail ,hotmail au yahoo n.k.
Mdau ukitaka kuhakikisha kama ni e-mail ya Serikali wewe angalia 'Domain' yaani mwisho wake unaashiria ni taasisi ya Serikali tena ya Tanzania.
ReplyDeleteMfano hapo E-mail:nje@foreign.go.tz
Ukichukuwa baada ya alama @ hiyo foreign.go.tz anzia na www.foreign.go.tz utaona ni tovuti ya Wizara ya mambo ya nje Tanzania inafunguka.
Tumia mbinu hii kuzibaini hata tovuti za wajanja Matapeli utawabaini tu...hata siku moja Taasisi Makini au Mamlaka haiwezi kutumia e-mail ya biashara kama gmail ,hotmail au yahoo n.k.
Wadau Watanzania waliopo Uguriki ni ukaidi wao na kujifanya wanakufa na tai shingoni,,,wenyewe hawataki kurudi nyumbani kwa Ubwege wao pamoja na Uongozi wao wa Jumuia ya Watanzania unao kataa kukubali ukweli kuhusu Kiama ,njaa na Balaa la maisha yaliyopo huko.
ReplyDeleteUtafikiri kama vile waliopo huko waliondoka kwa shari nyumbani !