Mchoro unaoonesha jinsi daraja la Kigamboni jijini Dar es salaam litavyokuwa baada ya kukamilika. Daraja hili, ambalo linajengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) linatarajiwa kuleta chachu kubwa katika ujenzi wa mji mpya wa Dar upande wa pili wa ghuba ya Kigamboni.

China Railways Construction Engineering Group kwa ushirikiano na China Major Bridges ndio walioshinda zabuni ya kujenga daraja hili lenye urefu wa mita 680 lenye njia sita kwa gharama za TSh 214.6. 
Ujenzi utachukuwa miezi thelathini na sita.
Kukamilika kwa barabara hii kutaleta maendeleo na kwa kiasi kikubwa litapunguza gharama za maisha kwa wakaazi wa Kigamboni. Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile ametoa pongezi kwa Wizara ya Ujenzi kufanya shughuli zake za msingi kwa vitendo. 
Pia ameipongeza  NSSF kwa kufanikisha mchakato huu kuanza kwa kutoa asilimia 60 ya gharama hizi, akisema ushiriki wa NSSF ni mfano mzuri wa ushirikishaji wa sekta binafsi (PPP).

Wadau wakiwa karibu na bango la mchoro wa daraja la Kigamboni wakati wa mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya kombe la NSSF 2012 uwanja wa TCC Chang'ombe ambako mfuko huo unaoongoza wa jamii umeandaa mashindano kwa timu za netiboli na soka za vyombo vya habari yanayotarajiwa kufikia kilele siku ya Jumamosi hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. This is exactly what kind of a bridge I was thinking of,Dr. Kikwete big-up, I love this, I love you, please make it happen.

    ReplyDelete
  2. Haya yote ni matunda ya Dr Dau. Sasa mimi nasubiri NSSF wafanye yafuatayo:

    1. Wamalizie zile slums za polisi pale Keko.

    2. Wavunje zile slums zote za Buguruni, Ilala, Magomeni na Temeke kisha wajenge social hosing zenye kuwapa watu staha ya maana na watu wapewe nafasi ya kuzinunua...

    3. Tanesco washashindwa kazi sasa NSSF wanunue Tanesco kisha Watupatie umeme wa Megawatt 10,000 kwa kuanza na baada ya miaka 10 watazame namna ya kutuletea nishati ya Nuclear (kama umeme mbadala wa upepo ukishindikana).

    4. Watujengee hospitali za maana ili tuondokane na adha ya kwenda India.

    5. Wamatuelee sisi watu wa disapora WESTADI ili tuondokane na adha ya kila kukicha kuomba michango michuzi blog.

    6. Watujengee nyuma za kuishi sie watu wa diaspora maana tushachoka kuibiwa na ndugu zetu.

    7. Wakishafanya yote hayo wapewe na Bandari waendeshe.


    - Mr NSSF aka Wimbi la Mbele

    (Ughaibuni)

    ReplyDelete
  3. Waanze kufikiria na high speed train network pamoja na METRO Dar

    ReplyDelete
  4. Mhhh watanzaniza vitu vizuri havitufai maana wafujaji na hatupendi maendeleo ya utanzania wetu sio watu wa maintanance tukishajenga na kukabidhiwa kwa sherehe kubwa basi mchezo umekwisha.kama tunapenda mali zetu je uwanja wa taifa tunaufanyeje? Ni watu wangapi wanajitolea kupanda miti mbele ya nyumba zao not even ndani kwao ndio kwanza tunatupa uchafu mbele ya nyumba zetu wengine kukojolea je ni nani wa kulaumiwa rais,waziri, mbunge,diwani au serikali ya mtaa.
    Yule yule
    Manka mushi muke ya mtu sasa

    ReplyDelete
  5. hizo si kama ile pesa aliyochukua liyumba kumbe ingeweza kujenga daraja ya kigamboni hahahahaha

    ReplyDelete
  6. Hilo daraja linajengwa kweli au wanambwelambwela kama kawaida ya wadanganyika? Tutaishia kuoneshwa michoro tuuuuuuu!

    ReplyDelete
  7. SIO DAR TU NI TANZANIA NZIMA NZIMA MPAKA KIGOMA NI CENTER KUBWA HIVI SASA YA BIASHARA KI NCHI KWA AJILI YA BURUBDI, ZAMBIA, KONGO, NA RWANDATUNATAKA HIGH WAY ZA KIKWELI.
    MDAU MTOTO WA UJIJI KGM.

    MKAZI WA LONDON

    ReplyDelete
  8. mie naona wakabidhiwe wiraza ya mipango maana hawa walau wana deliver

    mambo makuu mawili wayashughulikie

    Barabara/bandari/anga

    Nishati

    wakimashamliza huyo Dau wampe uwaziri mkuu kabisaa isiwe taabu

    maana ni dynamic na ni results oriented

    -mdau, Mbabane

    ReplyDelete
  9. big up NSSF, ongrats to Dr Dau, so when this project start?
    Bora mtujengee hilo daraja sie watu wa kigamboni nasi tujisikie maana panton uzushi mtupu!!!

    ReplyDelete
  10. WATENGENEZE WEBSITE AU BLOG YA KUHUSU HILI DARAJA MAENDELEO YAKE TUENDE NAYO MPAKA MUNGU AKIPENDA HIYO 2015 TUONE WAPI TUTAISHIA?

    ReplyDelete
  11. Uwaziri haumfai huyo bwana watamletea siasa nyingi,bora aendelee hapahapa NSSF ili angalau baadhi ya sehemu za nchi yetu zipendeze,jamaaa anakubalika CCM,CHADEMA,CUF,UDP,ADC,CHAUSTA,SAU,NCCR-MAGEUZI,TADEA,UMD,PONA,NRA,FORD,MAKINI,DP,JAHAZI ASILIA,UPDP,NLD, PPT-Maendeleo HIZB UT TAHRIR na MAKINI.

    ReplyDelete
  12. Did the designer of the bridge consider the fact that we Tanzanians are pretty good katika kuhujumu vitu vya umma hata kama vipo kwa ajili yetu wenyewwe? Tunaiba mafuta ya transformers; Live electricity wires; road signs; and anything worthy recycling. Those cables at the bridge are meant to support the weight load of the bridge. I don't doubt in a moment kwamba wapo watanzania wenzetu watakao tamani waziibe to make money kama sehemu ya mauzo yao ya vyuma chakavu. At the moment the bridge will be in really, really trouble. Hopefully I am just dreaming!

    ReplyDelete
  13. sijaona mchoro wa wananchi wakitembea hapo,au kutakuwa na shattle buses...? napatwa na wasiwasi kuwa kunaweza kukosekana usimamizi hapo baadae kama iliyo kwa TaZaRa.
    ila natakia ujenzi mwema,natamani lingekuwa linaisha kabla ya 2014

    mwana inji,
    China

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...