Kuna Mdau wa ugiriki aliandika 12/03/2012 ‘Kilio cha watanzania ugiriki” na kulikuwa na maoni tofauti yasiyopungua 25.
Kwanza kabla ya yote kichwa chake cha habari kingependeza kiwe “KILIO CHA MTANZANIA” na siyo “KILIO CHA WATANZANIA”
Pili ,kwa kuwa mtandao umeleta usawa wa mtu au watu kueleza chochote wakitakacho,imekuwa ni ada kwa baadhi ya watu kuelezea fikra zao kwa kutumia ANONYMOYS na wengine wakidai wapo nchi fulani kumbe hawapo kabisa katika nchi hiyo.
Mimi niandikae maelezo haya naitwa KAYU LIGOPORA mkaazi wa Athens ni Katibu wa Jumuiya ya watanzania tuliopo hapa. Napatikana kirahisi kwa email tanzathens@yahoo.com.
Nimelazimika kuuandika ufafanuzi huu baada ya kuombwa na watanzania wengi wanaoishi hapa waliosoma “KILIO CHA WATANZANIA UGIRIKI”
Ni kweli kuna hali ngumu ya kiuchumi ugiriki ukilinganisha na ilivyokuwa zamani.Yeyote ataepinga hali hili hatokuwa mkweli wa maelezo(Na huu ni ukweli pekee katika maelezo ya kilio cha Mdau wa Ugiriki).Isipokuwa mdau aliyeelezea kilio chake ametumia maelezo mengi yasiyokuwa na ukweli ili aweze kuwakinaisha wasomaji wakubaliane na hoja zake.
Kwa mfano
Anadai kuna majina ya wageni zaidi ya milioni waliojiandikisha kurudi (akiwemo na yeye) .. Hakuna ukweli wa idadi hiyo kulingana na takwimu za idara husika za hapa.
2. Anadai pa kulala wanashindwa kulipa hadi kuna wengine wanajipeleka hospitali ili walazwe wapate pa kulala!!!! Namnukuu “Imebidi baadhi yetu kuna ambao wamejipatisha vitanda hospitalini ili kuweza angalau kupata sehemu ya kuweka ubavu na chakula”…Hapa sina comment nawaachia wasomaji, ila tu nchi hii huwezi KUJIPATISHA KITANDA HOSPITALI KAMA HUUMWI na hasa ukiwa mgeni!!!
Inakuwa vigumu mno kuwakinaisha wasomaji wenye busara zao kwamba watanzania wa ugiriki kilio chao ni hicho kilichoelezwa na Mdau ANONYMOYS wakati kwamba juzi juzi watanzania haohao walikuwa wanajirusha na KHADIJA KOPA NA MATONYA na wanajiandaa kumleta mwimbaji mwingine katika kipindi cha Pasaka!!!!
Mwisho,inabidi wanaokuja Ughaibuni kutafuta maisha waelewe kuwa katika kutafuta kuna tabu tofauti ambazo zitawakumba na wanabidi wazivumilie. Ingekuwa maisha ni rahisi kama wanavyodhani basi kila mmoja angekuja Ughaibuni na kurudi Afrika akiwa milionea.
Asante kwa ufafanuzi Bw.Ligopora. Binafsi sijaona alichokosea Mdau kuandika Kilio cha WAtanzania Ugiriki, kwani kiukweli ni kwamba dunia inatawaliwa na MATABAKA ya rangi..
ReplyDeleteHivyo hata uwe BILIONEA lakini tu ukisha kuwa mweusi wa kutoka Afrika, huwezi heshimika even na wazungu walio omba omba wa mitaani kutokana na ukweli uliopo kuwa waafrika nao ni omba omba pia.
Kwa matiki hiyo Maoni ya MDAU aliyeleta hii hoja yata-sound zaidi na kuonekana ni ya UKWELI zaidi kuliko yako.
Hapa nimezingatia kuwa WAtanzania wanajirusha kwenye show za Khadija Kopa na Matonya then kesho yake MIHAYO mitupu kutafuta pa kwenda kukopa... maana HAWANA AKIBA.
Ukweli huu utajidhihirisha mtu AKIUMWA, AKIFARIKI au HARUSI utaona post za kuomba MICHANGO zinvyongozana humu kwenye blog ya Bw.Michuzi.
Tubadilike Watanzania wenzangu, maisha siyo SHOW-OFF bali ni UHALISIA wa akiba binafisi uliyojiwekea BANK kwa uwiano wa kipato cha jamii iliyokuzinguka.
Siyo kutesa na pesa za UFISADI ambazo hazina record ULIZIPA VIPI.
Naona kidogo tumeanza kupata maelezo yanayoingia akilini,maana hata Morogoro watu hawawezi kukimbilia hospitali ili wapate mahala pa kulala.Na nyie huko Ulaya ni ulaya gani hiyo watu wawe wanakimbilia kulala hospitali?
ReplyDeleteHalafu huyo katibu wenu ni mkali ile mbaya maana katoa vipande na hoja za maana haziwezi kupingika na yoyote. Of course maisha ya ugenini yanahitaji uvumilivu siyo lele mama.
ALUTA KONTIMNUA WADAU WA UGIRIKI NA HAO LELE MAMA WAAMBIENI WAACHE KULIALIA HOVYO.
kayu vijana wanajua ukija unapata na kukunja. hahahahha tulieni simnataka ulaya mbona mnalia sasa? ulikuja na nauliyako na utarudi na yako unaomba msaada wewe maiti?mnataka kuwapa msemo watu tuuu je mngeanzia huko tulipoanza kuyatafuta mh wacheni kupiga kelele kwani hamna ndugu?kama mwanaume kaza buti huu ni moto utapoa tuu vijana. KAZI KWENU
ReplyDeleteMdau No.1 hapo juu ni geneuos..
ReplyDeletemaana Amewachambua kama Karanga hao watu wa ulaya wanajifanya mambo safi kumbe Vumbi tu.
Magufuli alishasema.."PIGENI MBIZI" mrudi Bongo tuwape majembe ya Kilimo Kwanza tujenge Taifa.
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Ugiriki tunaona jinsi unavyosisitiza kuwa watu wako hawana shida na WANAJIRUSHA vilivyo.
ReplyDeleteSasa tusijekuona post za KUOMBA michango humu kwenye blog.
Mkipata matatizo tatueni wenyewe kwa hizo hizo pesa zenu.
very funny , kila mahali kuna watu mambo yao mazuri na wengine mambo ovyo ,hapa dar kuna watu wenye maisha mazuri na wengine wamechoka
ReplyDeletejamani, katibu hajakanusha kuwa hali si mbaya. kasema kweli hali ni mbaya lakini haijafikia kiwango cha kwenda kulazwa kisanii hospitali ili upate kula na kulala kwani haiwezekani...lakn kosa lake labda hilo la kutojali waTz wenzake wenye shida.kwa maana nyingine yeye kajiweka katika kundi la mafisadi wanaotesa ambao ni wachache huku zaidi ya 80% ya waTz hapa bongo wanalia njaa.
ReplyDeletekingine alichoweka wazi ni kuwa ngangari ktk maisha si huku ugiriki tu hata hapa bongo lazima ukaze buti ili angalau na wewe siku mojamoja ule nyama.
ni mtazamo tu
ahsante
hsm
enzi zetu walikuja jamaa kutuchafulia huko huko ugiriki eti tunaokota chakula kwenye mapipa,lakini hilo halikututisha wala kutushitua -tulikaza buti tena ndiyo tukakazana kweli kweli si machakoni hayo na kuvuna machungwa, yes wakati mwingine ponda ya namna hii inaongeza jaziba za kujitesa zaidi ili upate na yule bwana ponda yeye anabaki pale pale na suruali yake ya jeans-fainali nu uzeeni-kwa hiyi katibu ,usiudhike na hayo; Zebedayo
ReplyDeleteKayu Ligopotra,
ReplyDeleteKwanza, sawa kwa maneno yako isipokuwa kwa maisha ya popote kujipanga ni muhimu sana.
Pili wanaosafiri kwenda Ulaya wasifikiri huko kuna mafanikio ya rahisi rahisi.
Tatu licha ya Kujifanya wajuajai baadhi ya wanaoingia huko Wageni na kutokuonana na wenyeji lakini baada ya kukwama ndio wanatuma taarifa kama hizo, ninyi muwe mnafikika kwa wale wenye nia njema ilipindi mtu akikwama asaidiwe na Jumuia yenu huko Ugiriki ambayo lengo lake ni zuri tu, mfano tuliona mlivyofanikisha usafirishaji wa Mwili wa Marehemu Jamuhuri kuja kuzikwa Zanzibar mwezi uliopita.
Bw.Ligopora-Awijje..Ndugu zako wa mofu na mtimbala tunakusalimia.Mimi nimefika University of Athens na kutembea mitaani sana.Kweli shida kwa sasa Waafrika wanayo sanaaa na kweli hata wengine wanatamani kurudi lakini nauli hawana kabisaaaaa.Nakuomba labda wewe kama mambo safi poa baki lakini wachangie nauli wanaotaka kurudi Tz..Hapa mambo safi tunakula na kunywa.
ReplyDeleterumba limemchanginyi huyo....bado airport tax bongo dollar 50...awe nayo hiyo akikosa kalala segerea....umepata wp kibari cha muda cha kuasfiria ndio swali lao la kwanza....mi niliulizwa kwa nini umekaa sana....ujinga mtupu
ReplyDeleterumba limemchanginyi huyo....bado airport tax bongo dollar 50...awe nayo hiyo akikosa kalala segerea....umepata wp kibari cha muda cha kuasfiria ndio swali lao la kwanza....mi niliulizwa kwa nini umekaa sana....ujinga mtupu
ReplyDeleteUHALISIA NI KITU CHEMA ZAIDI:
ReplyDelete1.Kuwepo Ulaya sio kigezo kuwa utakuwa na maisha mazuri tu.
2.Kuwa na gari au Kuendesha Range Rover Vogue sio kigezo cha uwezo wa kifedha, mtu anaweza hata kumiliki ndege lakini akawa hana fedha au ana madeni lukuki!
SHIDA NI SHIDA NA NJAA HAINA KWAO!
Jamani kuomba msaada aidha wa mazishi n.k ni kawaida kwa tamaduni zetu,na especiaaly kwa mtu akifia nje ya nchi,kusafirisha maiti ni gharama sana,so msaada wa michango kwa ajili hiyo,sioni tatizo. Mbona hata hapa bongo tunachangiana kupeleka maiti moshi au mkoa wowote?
ReplyDeleteKuhusu mtu kujipeleka hosp kwa ulaya hicho kitu hakuna,hapoa ni uongo mtupu, ulaya hosp kwanza ili utibiwe kazima uwe na insurance, pili kama huna ugonjwa wa kukufanya ulazwe,hicho kitu sahau, huwezi kulazwa, walioishi ulaya wanaelewa, huwezi kwenda kuomba E.D ili utege class/office nini leo eti ujipeleke upewe kitanda!!! loh
Kwa ugumu wa maisha ulaya maisha ni magumu bse kule kila mtu ni independent,hakuna kukopana kule kama huku, kwanza pesa zenyewe huzioni kila mtu anatembea na card...
JAMANI WATANZANIA TUWASALIE MITUME, MCHANGO WA KIFO NI UTAMADUNI WETU SIS WOTE WATANZANIA SI NYUMBANI TU MPAKA POPOTE TUNAPOISHI WATANZANIA . SASA KIPI KIBAYA HAPO ETI WANACHANGISHANA? ELEWA NA GAHARAMA KWA MFIWA KUFANYA SHUGHULI ZOTE ZA MAZISHI BILA MSAADA WA NDUGU ,RAFIKI,JIRANI, NA WOTE WENYE MOYO WA KUFAHAMU HILO ,KWANI KIFO HAKINA MMOJA NI JUKUMU LETU SISI WOTE, NA KITATUFIKA! HATA HUKO BONGO AMBAKO KUNA MAFISADI WALIOKUBUHU WAKIFIKIWA NA MATATIZO HUWA KUNA MICHANGO YA MAZISHI, HATA MFANO TUNAMUONA RAIS WETU JK, MARA NYINGI KENDA TOA SALAAM ZA RAMBI RAMBI KWA WAFIWA NA KIBAHASHA CHA MCHANGO AMBACHO HUWA KAWAIDA HATUJUI NI NIASI GANI KACHANGIA ,LAKINI NI PESA ILI ZIWEZE KUWASIDIA WALIOFIWA HUSUSAN KWA KIPINDI KILE KIGUMU BAADA YA MEMBER WA FAMILI AKITANGULIA MBELE YA HAKI. SASA HUKO UGIRIKI NA POPOTE UGHAIBUNI KUMCHANGIA MTANZANIA MWENZETU ILI AKAHIFADHIWE NYUMBANI ILI BABA NA MAMA, NA NDUGU WOTE WAWE WANAWEZA KUONA KUMBUKUMBU YA KABURI LAKE NINYI MNAONA NI UJINGA? WAKE UP TANZANIA!!!MBONA MAREKANI KILA SIKU WANACHANGISHANA KULETA MAITI BONGO HAMSEMI KITU ? AU KWA SABABU NI MAREKANI? MSIFE MOYO WATU WA UGIRIKI MOYO WENU UWE HIVYO HIVYO MSIACHE UMOJA HUO NDIO USUKANI WETU LAZIMA MUISHI KWA UMOJA HUO NI UTAMADUNI WETU SISI WATANZANIA .SISI SI MAWEST AFRICA AU WARUNDI WA HUTU/TUTSI.
ReplyDeleteKUMBUKENI SI UGIRI TU NDIO KUNA MATATIZO YA UCHUMI NI DUNIA NZIMA KUANZIA MAREKANI,ULAYA YOTE MPAKA SCANDINAVIA,NA UJERUMANI PAMOJA NA UFARANSA NA WAO NDIO WANA TEKNOLOJIA YA HALI YA JUU LAKINI BADO MATATIZO NI HIVYO HIVYO KAMA UGIRIKI. WAZUNGU WOTE WAMEPAGAWA NA NDIO WAKO KWAO ITAKUWA SEMBUSE SISI WAGENI?
Bwana Kayu Ligopora, usipoteze muda kujibu hoja au maoni ya watu wengi wanaojiita anonymous. Yule bwana aliyeandka ile article ya "kilio cha watanzania ugiriki" ni mtu anayeonekana kwamba amechanganyikiwa. Na inawezekana ni baadhi ya wale ambao wameshindwa kuanzisha maisha ughaibuni na hasira zao ndiyo wazungu wanaita "sour grapes". Kila mtu mwenye akili timamu aliyeisoma habari ile alitambua kwamba ni habari ya kipumbavu iliyoandikwa na mpumbavu kufurahisha wapumbavu wenzake. Na matokeo yake kama ulivyoyaona, wapumbavu wenzake wengi tuu wamefurahi sana na kujipa moyo kwamba "labda maisha ya mtanzania wa Tanzania ni bora kuliko maisha ya mtanzania wa ugiriki".
ReplyDeleteMimi binafsi sijawahi kuishi Ugiriki, ingawa nimewahi kupita ugiriki na nimeishi nchi kadhaa za Ulaya.
Ujumbe kwa wale
watanzania "waliofanikiwa" kimaisha ndani ya Tanzania.
Mtanzania anayeishi ugiriki akiwa na vibali vya kuishi anakuzidi wewe katika mambo mengi sana ya kimaisha, kwa mfano yafuatayo.
1. Security. Ugiriki kuna polisi wanaowajibika kwa raia na watu wote wanaoishi ugiriki. Polisi wa Bongo wanaomba pesa raia, na kama huna cha kuwapa basi umekwisha.
2. Elimu. Ugiriki ina taasisi za kielimu, shule za watoto, na hata wakubwa ambazo Tanzania haina. Ndiyo maana mafisadi hupeleka watoto wao nje ya nchi kusoma. Wagiriki watoto wao wanasoma Ugiriki.
3. Chakula. Ugiriki hakuna njaa ya kula. Bongo njaa ya kula ipo.
4. Utandawazi. Ili sina hata haja ya kulizungumzia kwa sababu lipo wazi sana.
5. Usafiri. Bongo hata ukiweza kumiliki Lamborghini, bado utatumia masaa 3 kusafiri km 5. Ugiriki hakuna upumbavu huo.
6. Afya na michezo. Mtoto wa Mtanzania anayekulia ugiriki ana nafasi kubwa ya kushiriki kwenye michezo yote unayoijua wewe, na siyo football na basketball tuu kama watoto wa vibosile wa bongo.
7. Huduma za Afya. Hospitali za Muhimbili au Kairuki hazifikii kabisa viwango vya huduma za afya vinavyotolewa na hospitali za ugiriki.
8. Kuwa sehemu ya Dunia. Mtanzania mwenye pasipoti ya Ugiriki ana urahisi wa kusafiri na kutembelea sehemu kadhaa duniani kuliko hata mtanzania mwenye diplomatic passport ya Tanzania.
9. Usafi. Ugiriki neno "nguo ya mtumba" halipo kwenye lugha yao. Kwa ufupi, Mtanzania anayeishi ugiriki havai nguo ya Mtumba.
10. Usafi wa mazingira. Ugiriki hakuna mtaro wa maji machafu "open sewers" kukatiza mitaa wanayoishi wanadamu. Vipindupindu hakuna huku.
11. Sina haja ya kuongeza mengi kwa sababu hatutafikia mwisho. Ujumbe tuu kwa watanzania mlio ugiriki endeleeni kutafuta maisha na msikatishwe tamaa na baadhi ya watanzania waliopo hapa nyumbani.
bulshit rudini bongo mkajenge nchi kilimo kwanza
ReplyDeletewadau wa uholanzi tunapeta kila mtu mfukoni kumejaa mihela hihaaa hehe sio laziwa wote tuishi huku ukristoni wengine munaweza kurudi nyumbani mkaendelea na zile kazi zenu za kuuza vitumbua au wale ndugu zangu wahaya wasisahau kazi zao za asili. lol
Ughaibuni hakuna shida yoyote kwa mtu mwenye makaratasi maana kuna "social service" watakusaidia. Tatizo ni kwa ndugu zetu wanaohangaika na dunia hawana makaratasi na ili wasaidiwe inabidi wajulikane wao nani na kama ni wahamiaji haramu inabidi warudishwe kwao. Katibu inawezekana yeye ana makaratasi ndio maana anatoa maneno ya mtu asiye na wasiwasi na kuwatetea walioko ughaibuni. Hivi sasa huna ujanja maana wana "finger print" zako tayari.
ReplyDeletemimi naona maelezo ya huyo katibu wao yapo wazi na clear.hayana migonngano wala mizunguko.kasema wazi kuwa SHIDA IPO ila kafafanua kibusara na kiuwazi kuwa watanzania wake hawajafikia hali ya kukimbilia hospitali ili wapate pa kulala.Halafu inaonekana vijana wa sasa maisha ya bichi hawayawezi.je wangeweza vipi kuishi India enzi za kulala kwenye maboksi na kupigana vikumbo na mbuzi ? LIFE IS NOT LELEMAMA Kama hamwezi kustrago rudini mje kunywa maziwa na mtindi
ReplyDeleteHii mada ya ndugu Lingobora imeongeza utata badala ya kutatua.
ReplyDeleteNadhani badala ya kebehi za utajiri alizozionyesha, alitakiwa tu kuweka mkazo kwa Watanzania popote pale walipo iwe ni Ulaya au Africa, wajitahidi kwa kadiri ya uwezo wao kujitegemea wenyewe bila kumtegemea mtu mwingine katika maisha yao binafsi.
Beach Dume Mbona nyingi sana tokalini Nurs akapewa Bunduki aende Vitani kama wewe msafiri kweli huwezi kuanza ngonjera hapa nipo beach dume na nakomaa nao tu hakuna short cut hata cku moja komaa mwana au kama vp shuka kwa madevu buluza kiwanja kingine NO WAY BACK .Tanga/Dar Zenji /Mtwara.wanajua hio
ReplyDeleteWadau, kinachotokea ugiriki sasa ni kuanguka kwa uchumi, ambapo bwana katibu wa watanzania hajaongelea kabisa. uchumi ukianguka, (recession) maana yake, makampuni yanashindwa kulipa mikopo, uzalishaji unashuka, wafanyakazi wanachishwa kazi (Redundancy) na matokeo yake, mtu kibao zina kosa kazi. na kazi zikishakuwa haba, basi maisha yanakuwa magumu, hawezi lipa kodi ya pango mwishoe unatolewa kwenye nyumba, hela ya chakula hakuna na hivyo maisha yanakuwa magumu na hasa ukiwa ulaya ambao hakuna kupigana mizinga.
ReplyDeletehii si kwa wageni (watanzania) bali hata kwa wazawa wenyewe.
Kwahiyo bwana katibu kosa kubwa ulofanya kuonyesha kuwa watanzania ugiriki mambo safi kwa kigezo cha shoo za malkia wa mipasho Khadija kopa na Matonya, umepotoka big time.
ukweli uko pale pale ugiliki sasa inapita katika kipindi kigumu, na wengine ndo maana sasa wanaomba nauli warudi nyumbani, of course mdau alikosea kuwasemea na wengine japo yeye aliamini kuwa huu ndo ukweli.
katibu fanya utaratibu iliuweze kuratibu swala hili vizuri ili watanzania wenzetu wanaonataka kurudi nyumbani na hawana nauli, ili sisi tulioko huku nyumbani tuweze kusaidia.
Mdau,
Tegeta, Dar es salaam
Jamani naomba naomba ni muunge mkono kuna jamaa mmoja alisema kwenye Michuzi iliyopita, wabongo tunapenda kweli kuosha vinywa(na mie nimo). Wabongo tunaongea sana. 1.shida ni shida hata uwe wapi ni shida tu, uwe tajiri, masikini, mtoto, baba, mama,n.k.
ReplyDelete2.Hoja ya kuchangia kwenye vilio na harusi siyo kwamba jamaa wameshindwa binafsi lakini ni utamaduni wetu kuihusisha jamii kwani haiwezakani matukio makubwa kama hayo kuyafanya binafsi.(fikilia umbeya utakaosemwa kama una ndugu yako alifariki ukachimba kaburi na ukazika mwenyewe?)sipati picha.
3.Mie nawashangaa watu wanaowakatalia Wabongo walio ughabuni-si dada na kaka zetu? Jamani Wabongo unafiki, majungu, ushurikina mwingi mno. Mbona hatuwapigi vita watu toka nje' kama hao tunaiwata wawakezaji toka nje' au makocha wa Simba, Yanga na Taifa Stars? Lakini ndugu zetu kabisa walioenda nje'tunaosha vinywa. Na mbona wengi wanasadia sana kama kutuma pesa nyumbani, kutoa hujuma nyingi zinafanywa na serikali, au makapuni binafsi?.
Kayu Ligopora Mdau Kiongozi Katibu wa Umoja Ugiriki.
ReplyDeleteTumekuelewa vizuri licha ya sinto fahamu za baadhi yetu humu kama maoni yanvyoeleza.
Kwa kweli 'Uongozi ni Jaa' au 'Ukubwa ni jalala' huyo mtu mmoja liyekwama huko Ugiriki alitakiwa afanye ufuatiliaji kwanza kama kuwaona ninyi wana Jumuia huko kabla ya kumtumia Ankal Michuzi kilio cha msaada wa taarifa.
Ankal yeye kama Mdau mwezeshaji, Mzalendo halisi, mwana mapambano na ndugu wa Jamii yote ya Watanzania akafanya jukumu lake kama inavyostahili kwa vile utaratibu wake ni kutofungamana upande mmoja au kumbana yeyote,,,akairusha taarifa hewani!.
Kwa hivyo kama huyo mtu hatakuwa mwongo endapo yupo ndani ya Ugiriki kweli hivyo ugeni huo utakuwa ni wako kwa vile wewe ndio utafanya taratibu za kumfikishia lengo ili kama kweli amekwama arudi nyumbani kama anavyokusudia!
Ahhh inawezekana jamaa aliyekwama atakuwa Msumbiji akielekea Afrika ya Kusini na sio Ugiriki!
ReplyDeleteHaya ndio matokeo ya safari zisizokuwa na mipango.
Kwa nini asitoe namba ya simu au mawasiliano kuwa ni sehemu gani ktk Ugiriki yupo?
wewe unatia aibu eti aseme mtanzania kashasema wapo zaidi ya mmoja kwenye matatizo hayo sasa unaona aibu ya nini kuja humu kuandika mambo ya ajabu
ReplyDeletekwani wewe unajua watanzania wote? tena kaeleza vizuri sana kuwa ni wageni sasa wewe umeshakaa huko amekuongelea????
unaona aibu ya nini? mtu kasema kweli unaleta kutetea, kwani hospitali mtu aezi kujipeleka akadai anaumwa?
Unatia aibu wewe nyie ndio hampendi kusaidiana,
BADALA YA KUJA KUOMBA UWASILIANE HAE UWASAIDIE WALIO NA MATATIZO NA KUWASHAURI UNAKUJA KUTETEA PUMBA HUMU.
i hope wewe kama katibu ni unatia aibu chama chenu sana.
wewe umefatilia wapi kupata hizo point alizosema? idara gani umeulizia si utaje? mtetezi huwa anakuwa na info kajitayarisha sio kupinga bila kichwa.
hao waliokutuma ni wangapi acha hizo aibu ya nini. badala ya kukaa chini muongelee kusaidia wenzenu wanaoteseka mnakuja kupinga ukweli wanaoteseka huko
Acheni ubaili na ubinafsi saidieni wenzenu sio kuja kuandika story za kujitetea. Katibu umetia aibu kubwaaaaaaaaa
mtu zaidi ya mmoja ni WATANZANIA. period...do you get that????
Acha kutapa tapa Katibu, fanyeni mambo ya maana nyumbani. Mkija bongo hata pa kufikia hamna. Mnaanza kusumbua watu, ooh joto. Jenga nyumba weka AC. Tunamshukuru mdau aliyesema hali ni mbaya, na wengi mnajishughulisha na biashara ya unga. Mimi kaka yangu yupo huko miaka kiabao, hana kitu. Mwezi uliopita kafungwa huko Ugiriki kwa biashara ya madawa ya kulevya. Nisikilizie msiba utokee, hapo ndio utajua kama kweli upo majuu au chini. Mwezi mzima mnahangaika na michango kurudisha mwili nyumbani, hivi kwanini huwa hamziki huko huko? Mnasumbua hadi huku Bongo, nakumbuka mara ya mwisho wale wenzenu wa Italy wakaituma maiti ki aina. Niwaulize hivyo mkizeekea huko nanyi mtawekwa zile nyumba za wazee? Kama hivyo mna nguvu zenu mnadharaulika hivi, sasa huko kwenye nyumba za wazee nani atawhudumia?! Rudini nyumbani, acheni kupoteza nguvu kazi ya Taifa ulaya. Kuna wachache sana niliowatembelea unakuta wana maisha mazuri, lakini 90% ni msoto tu.
ReplyDeletewewe unatia aibu eti aseme mtanzania kashasema wapo zaidi ya mmoja kwenye matatizo hayo sasa unaona aibu ya nini kuja humu kuandika mambo ya ajabu
ReplyDeletekwani wewe unajua watanzania wote? tena kaeleza vizuri sana kuwa ni wageni sasa wewe umeshakaa huko amekuongelea????
unaona aibu ya nini? mtu kasema kweli unaleta kutetea, kwani hospitali mtu aezi kujipeleka akadai anaumwa?
Unatia aibu wewe nyie ndio hampendi kusaidiana,
BADALA YA KUJA KUOMBA UWASILIANE HAE UWASAIDIE WALIO NA MATATIZO NA KUWASHAURI UNAKUJA KUTETEA PUMBA HUMU.
i hope wewe kama katibu ni unatia aibu chama chenu sana.
wewe umefatilia wapi kupata hizo point alizosema? idara gani umeulizia si utaje? mtetezi huwa anakuwa na info kajitayarisha sio kupinga bila kichwa.
hao waliokutuma ni wangapi acha hizo aibu ya nini. badala ya kukaa chini muongelee kusaidia wenzenu wanaoteseka mnakuja kupinga ukweli wanaoteseka huko
Acheni ubaili na ubinafsi saidieni wenzenu sio kuja kuandika story za kujitetea. Katibu umetia aibu kubwaaaaaaaaa
mtu zaidi ya mmoja ni WATANZANIA. period...do you get that????
wewe uliesema ulaya lazima uwe nainsurance usidanganye watu labda ni nchi unayoishi
ReplyDeleteacheni kusema ulaya wakati mnaongelea nchi au eneo unaloishi wewe.
Pumba tupu kudanganya watu eti lazima uwe na insurance kutibiwa nasema tena labda ni huko ulipo wewe au ulipokuwepo
muongo mkubwa kusema ulaya?
siku zote mwerevu atabaki kuwa mwerevu, na mjinga atabaki kuwa mjinga iwapo hataki kujibadilisha kupitia watu.. hata siku moja mtu alioishi ulaya huwezi kumsikia anaongea pumba kama hizi ,eti unajitia ugonjwa wa uwongo ili upate malazi na kula ulaya, msemaji wa maneno hayo atakuwa mgambo, aliepita akachemsha kwa ulegevu wake. mdau ugiriki
ReplyDeleteelisante chagaboi Anonymous wa Tue Mar 13, 11:26:00 AM 2012.
ReplyDeletePANA RAHA SANA KWA AINA YAKE KTK MAISHA ASILIA NA UHALISIA KAMA:
1.Kukaa mfumo wa maisha ya Kijamii zaidi kama ilivyo nyumbani Bongo.
2.Watoto wako waka ishi maisha asilia na halisia ya Mwafrika.
3.Ukala chakula asilia na halisia kutoka shamba moja kwa moja na sio, chakula bandia kutoka ktk frizer.
4.Ukapata Sheria ya Kijamii kwa migogoro yako kifamilia na mwenza wako ikatatuliwa Kijamii ktk ukoo badala ya Mamlaka za Sheria za Majuu ambazo zinakandamiza kulingana na Utamaduni na Mila zetu za Kiafrika.
5.Ukaenda bafuni kuoga taulo huku begani, ndoo mkononi, na kopo la kuogea kwapani!,,,(unakuta muda mwingine bafunim kuna foleni huku choo ni cha 'passport size' badala ya bafu la Mvuke na sabuni za Majuu kama Jergens n.k.
6.Ukacheza Bao na Karata na na Wazee Mtaani.
7.Ukapata 'Social life' baada ya muda wa shughuli zako kuisha kwa kupata maongezi ya Vijiweni na Mitaani au Kijijini, wakati Majuu au Ughaibuni hakuna muda mchafu kama huo watu wako bizy na kufukuzana na $$$$.!
ZAIDI ZAIDI RAHA YA MAISHA ASILIA NA UASILIA YA KIAFRIKA!
Mdau hoja zako 11 ktk Maoni yako ni za kueleweka isipokuwa ukweli upo pale pale 'HATA UGHAIBUNI KUKIWA KUZURI KAMA PARADISO,,,''INGAWA SIO KWELI'' KWA KUWA HIYO HIYO MAJUU WAPO WALIO KTK PEPO NA WAPO WALIO KTK KIAMA,,,UGENINI UHAMISHONI NI UTUMWANI ,BADO INABAKI KUWA NYUMBANI NI NYUMBANI BONGO JUU, JUU, JUU!!!''
Mdau wa Tegeta Anonymous wa Tue Mar 13, 12:13:00 PM 2012
ReplyDeleteNakuunga mkono asilimia 100% ukweli ni kuwa Dunia nzima imefilisika, na kuwa kifo cha wengi Harusi na ibaki kuwa samaki mmoja akioza basi wote wameoza!
KAYU LIGOPORA ,Kiongozi Katibu wa Jumuia ya Watanzania Ugiriki elewa kuwa:
*****UKWELI NI KUWA HALI HALISI NI MBAYA DUNIANI KIFEDHA NA KIUCHUMI, HASA HIYO HIYO UGIRIKI, KAMA UWEZO ATAKUWA NAO YEYE NI AKIBA YAKE KIDOGO ALIYO NAYO YEYE PEKE YAKE, ASIJITETEE NA KUWACHANGANYA WENZAKE AMBAO WAMECHOKA*****
WEWE NI KIONGOZI ILITAKIWA USIKANUSHE HIZO HABARI, ULITAKIWA UZIFANYIE KAZI HALAFU UCHUKUE HATUA ZINAZOSTAHILI, HILO NDIO JUKUMU LA UONGOZI, INAELEKEA KATIBU WEWE NI KADA MZURI SANA WA SIASA ZA KIBONGO ZA KUPINDISHA UKWELI.
Siyo vizuri kujikaza kisabuni wakati hali ni tete kwa kutumia Matamasha ya miziki ya Matonya na Mipasho ya Khadija Kopa kama kigezo cha uwezo wa kimaisha!.
Acha Ujasiri mbaya na hatari wa namna hiyo wa kufa na tai shingoni!.
Kayu Ligopora Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Ugiriki!
ReplyDeleteHaaa wewe ni Katibu wa Jumuia au ni Kada wa Chama cha Siasa?
Ama kweli hazina iliyofichika ipo Ughaibuni, unatukumbusha Ofisa Habari wa Utawala wa IRAQ kipindi cha Raisi Saddam Abbas Hussein, akitoa uhakika ktk BBC kuwa Majeshi ya Marekani yako km 300 kuingia Baghdad wakati ukweli yakiwa km 3 tu!
Kayu Ligopora,
ReplyDeleteUnatokea kuwa 'Mwanasiasa au Kada wa Chama cha Siasa tena za Kitanzania' zaidi kuliko kuwa Katibu wa Umoja wa Watanzania huko Ughaibuni!
Jirekebishe usiwe Kisiasa bali uwe kiumakini na Kiuhalisia zaidi!
elisante chagaboi, Anonymous wa Tue Mar 13, 11:26:00 AM 2012
ReplyDeleteUmetoa Maoni yako na hoja 11 kuhusu Ubora wa Maisha ya Ughaibuni ikuwemo hiyo Ugiriki iliyokwisha filisika kimaisha,,,dhidi ya Mtu aliyefanikiwa kimaisha hapa Tanzania.
UKWELI UTABAKI KUWA:
MFANO WANA DIASPORA WAKONGWE DUNIANI NI JAMII YA WAYAHUDI WALIOTAPAKAA KONA ZOTE ZA DUNIA.
LAKINI WAKAJA BAINI KUWA LICHA YA KUWA NA KILA KITU KTK MAISHA YAO POPOTE WALIPO DUNIANI, MFANO UPENDELEO KUTOKA UN, KUWA NA FEDHA NA UWEZESHWAJI WA MABENKI N.K WALITAMBUA KUNA UMUHIMU WA KUUNGANA NA NCHI YAO YA ASILI YA AHADI.
NDIO MAANA HATA KAMA WAKIWA NJE KWA MAKAZI YA KUDUMU, IWE NA URAIA WANAJIHESABU BADO WAO NI TAIFA LA ISRAEL NA BADO WANAUNGANA NA KWAO KWA NJIA YA TAASISI ZA JUMUIA YAO AMBAZO NI ZA KUMUAMKO NA KIITIKADI.
NA WAO NDIO WAMEANZISHA MIPANGO KAMA YA DUAL , MILTIPLE CITIZENSHIP NA DIASPORA.
HIVYO NDUGU YANGU Elisante Chagaboi KWA MFANO HO WA WANA WA ISRAEL DUNIANI HAPO JUU,,,UMUHIMU WA NYUMBANI TANZANIA UPO PALE PALE HATA UFIKE NCHI YA PEPO YENYE KULIWA ASALI KWA MAZIWA.
elisante chagaboi, Anonymous Tue Mar 13, 11:26:00 AM 2012.
ReplyDeleteMdau hayo mafao 11 uliyoyataja yanapatikana wakati Uchumi ukiwa umeimarika na sio Uchumi tete unaotegemea (TENA KUFIKIRIWA KUPEWA MKOPO IKIWA NI MARA YA 3 WAKATI MARA MBILI TAYARI LAKINI HAIKUSAIDIA) Mkopo kutoka Benki ya Ulaya!.
Gharama za maisha zataka Uwezo wa Kiuchumi wa Jamii husika kitu ambacho kwa GREECE hivi sasa 'HAKUNA' !.
Wewe unaona Wazito wa Serikali ya Ugiriki na wa Umoja wa Ulaya makoti yanawawia kuwa mazito, vipara vina mwagika majasho kutafuta kuinusuru nchi ya Ugiriki na Ulaya Kiuchumi halafu wewe unadai wanao uwezo wa kuwapa watu mafao hayo 11,,,kweli Mangi maneno yako yanaenda wa wakati?
elisante chagaboi, Anonymous Tue Mar 13, 11:26:00 AM 2012.
ReplyDeleteMdau hayo mafao 11 uliyoyataja yanapatikana wakati Uchumi ukiwa umeimarika na sio Uchumi tete unaotegemea (TENA KUFIKIRIWA KUPEWA MKOPO IKIWA NI MARA YA 3 WAKATI MARA MBILI TAYARI LAKINI HAIKUSAIDIA) Mkopo kutoka Benki ya Ulaya!.
Gharama za maisha zataka Uwezo wa Kiuchumi wa Jamii husika kitu ambacho kwa GREECE hivi sasa 'HAKUNA' !.
Wewe unaona Wazito wa Serikali ya Ugiriki na wa Umoja wa Ulaya makoti yanawawia kuwa mazito, vipara vina mwagika majasho kutafuta kuinusuru nchi ya Ugiriki na Ulaya Kiuchumi halafu wewe unadai wanao uwezo wa kuwapa watu mafao hayo 11,,,kweli Mangi maneno yako yanaenda wa wakati?
Kweli nakubaliana na mdau nyie hamna muda wa kupoteza ratiba yenu ipo tight kweli kwa kutafuta $$$$.Kazi sita kwa siku 1. Asubuhi kusafisha supermarket na kubeba mabox, mchana kusafisha McDonald restaurant, usiku kukesha nyumba za wazee kubadilisha pampers!
ReplyDeleteRudini nyumbani wapendwa mtuletee hayo mliyoyaona huko. Kwa uhakika ukifika na kugombea ubunge unaupata, halafu tunaanza kwa pamoja kulijenga taifa. Unatoa maoni yako mazuri ili yafanyiwe kazi na Tanzania ipate kuwa mahali pazuri, wazazi, ndugu na jamaa wafurahie matunda yenu, nao waishi maisha mazuri kama Ugiriki.
Kayu Ligopora!
ReplyDeleteInaonekana upo busy sana na maisha yako binafsi!
Hivi unafungua TV au kufuatilia vyombo vya Habari vya Dunia huko?
Inaonekana upo nje ya Dunia ya kawaida ni kama upo Sayari nyingine!
Ugiriki imekaribia kaburini kabisa, zaidi ya (Kufikiriwa Mkopo kwa mara ya 3) Umoja wa Ulaya baadhi ya nchi Wanachama zenye Msimamo mkali kama Ujerumani, Ubelgiji na Uholanzi ZILIFIKIA KUPENDEKEZA UGIRIKI IENGULIWE NA KUTOLEWA KTK UANACHAMA WA JUMUIYA YA UMOJA WA ULAYA KWA UZEMBE WA KUSHINDWA KUSIMAMIA NA KUFIKIA MALENGO BAADA YA MIKOPO MIWILI YA AWALI WALIYOPEWA NA BENKI YA UMOJA WA ULAYA...LAKINI KWA HURUMA YA NCHI ZA SKANDINAVIA WAKATETEWA. IKIDAIWA IKIENGULIWA UCHUMI WA ULAYA UTAPATA ATHARI ZAIDI,,,BORA KULIBEBA TEJA LAO HIVYO HIVYO...
SASA LEO KAYU LIGOPORA ANATOA MSIMAMO KWA KUPINGA TAARIFA YA KIFO CHA KIMAISHA UGIRIKI,,,EBO!
Mdau wa Fri Mar 16, 02:30:00 PM 2012 hapo juu,
ReplyDeleteWalahi wacheni nichekeeeee!
''Ugiriki imekafribia kaburini kabisa''
Labda Kayu Ligopora akiwa usingizini totoro atakuja zinduka Ugiriki imeshazama Kaburini yupo gizani na huku mchanga umefinikwa!
Sijui ndio atafufuka atoke aamini maneno na ndio aamue kurudi Tanzania?
Ugiriki ina kiama cha maisha zaidi ya:
ReplyDelete1.Tanzania ilivyokuwa ktk vita ya Uganda mwaka 1978-1979 Wananchi walipotangaziwa wafunge mikanda kwa miezi 18 ya shida!
2.Ni afadhali ya Libya ilivyopigika na kupondeka kwa Makombora ya NATO ktk Wimbi la Vita vya Mapinduzi ya mwaka jana 2011!
3.Somalia yenye vita vya zaidi ya miaka 20 ina nafuu, kama ilivyo Mogadishu sasa ni kama Kijijini na sio Mji Mkuu wa nchi, maisha ya watu na Mifugo hadi Mogadishu mjini ili kujihakikishia Amani na Usalama dhidi ya vita wao na mifugo yao.
Mogadishu ipo kama ilivyokuwa Karne ya 12 wakati sasa tupo ktk Karne ya 21 ina nafuu.
Maandamao peke yake Ugiriki tunayaona ktk TV na uharibifu wa Waandamanaji unafanya kuwe kama Makombora ya vita yamepiga nchi!
ACHENI UBISHI MRUDI NYUMBANI MJE MFANYE UMACHINGA MIJINI AU VIJIJINI KULIMA!
Mtoa Maoni wa 41 hapo juu
ReplyDelete'UGIRIKI IMEKARIBIA KUTENGWA KUTOKA UANACHAMA WA UMOJA WA ULAYA'
Sasa ndugu zetu mliopo Ugiriki ikitengwa mafao yale 11 aliyoyasema....Mangi elisante chagaboi yatakuwepo?
Duhh inaonyesha wengi hawafuatilii mambo jinsi Dunia inavyokwenda, hata waliopo huko Majuu kukicha wanawahi Madukani kubeba Ma Box!
Mpaka Katibu wa Umoja hajui yanayojiri!...atakuja zinduka kusikia nchi imeuzwa kwa Mabepari Mabilionea wa Urusi!
Si Ugiriki baada ya kutengwa itakuwa kama nchi za Afrika tu?
Greece imelipuliwa kimakosa na Makombora ya NATO!
ReplyDeleteWalikuwa wamelenga Iran kuangamiza mitambo ya Nyuklia kwa bahati mbaya yakatua kwa Magiriki!
Wabeba Ma BOX Wabongo sasa wanatafutana!
Ama kweli katika kila kichwa cha binadamu kuna mashine inayopokea habari na kuielewa tofauti na watavyoielewa wengine. Nadhani huyu Katibu ameweka wazi kuwa KUNA SHIDA UGIRIKI ila shida hiyo haijafikia hatua ya mtu kukimbilia hospitali ili akalale na apate chakula.
ReplyDeleteSishangai kuona watu wanavyochanganya story na kuelezea mambo yasiyohusiana na topic kuu kama anavyoeleza mdau wa hapo juu akisema Greece imelipuliwa kimakosa na Makombora ya NATO! Nadhani ingependeza kama watu wangekuwa wanautumia ukumbi huu kujadili hoja kuu na kuchangia mawazo yatayoweza kuwasaidia ndugu zetu waliopo ugiriki waweze kutatua matatizo yao.MIMI NAMSAPOTI HUYU KATIBU WAO NA WALA SIONI KOSA LOLOTE ALILOFANYA
AMA KWELI DUNIA INA MAMBO NA AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE. UKIANGALIA HIZI COMMENTS UTAGUNDUA WAZI KUWA BINADAMU HATUANGALII JAMBO KWA MTAZAMO MMOJA .KILA MTU ANA MTAZAMO WAKE NA UELEWAJI WAKE.
ReplyDelete