Katibu wa Bunge, Dr. Thomas Kashililah akitoa maelezo kuhusu Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika ambacho yeye ni Katibu Mkuu wake, kushoto kwae ni Mhe. Zitto Kabwe na Mhe. Beatrice Shellukindo. Wa kwanza kulia ni Mhe. Kaimu Balozi, Mama Nyange.
Mhe. Zitto Kabwe akiuliza swali maofisa wa Ubalozi wa Tanzania waliokuwa wakitoa maelezo kuhusu uhusiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Zambia.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mama Nyange akitoa maelezo kwa wabunge wa Tanzania walioko mjini Lusaka kuhudhuria mkutano wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA). Nyuma yake ni maafisa wa Ubalozi huo pamoja na Mhasibu Mkuu wa Bunge, Ndugu George Seni (wa kwanza kushoto). Picha na Saidi Yakubu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...