Daraja la juu linalounganisha barabara za kwenda Market Street na inayotoka Eastlegh likiwa katika matenezo na kampuni ya Kichina ambayo inajenga madaraja hayo karibu katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Nairobi hii ni katika tatizo la kukabiliana na msongamano wa magari.Madaraja haya na jinsi nchi ya kenya inavyojitahidi kujenga madaraja haya kupunguza msongamano, Tanzania inatakiwa kuchukua changamoto kujenga madaraja hayo kama ambavyo Waziri wa Ujenzi Bw. John Pombe Magufuri, akisisitiza kwamba madaraja hayo yatajengwa, tusubiri tuone lakini kujengwa ni muhimu sana.Picha na Mashaka Mhando wa Globu ya Jamii,Nairobi
Home
Unlabelled
Watani wa Jadi walivyotupiga bao la kisigino kwa kuweka ma Fly over kila kona
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Huhh wajameni hizi Fly Over gani...???
ReplyDeleteHivi kweli unaweza kutengeneza Fly Overs wakati 'Ground Roads" are dirty and hugly like this..??!! kama barabara zenyewe za chini ziko hivi, why should you build the Fly Overs..???
Wenzetu wanajenga "Ground Roads" zinaimalika kwanza, the 'Fly Overs"
It doesnt make sense to me.
Kenya haina Dhahabu au Almasi au Tanzanite lakini inatuzidi karibu vitu vingi vya kimaendeleo! Nyerere alisema uchumi mnao lakini mnaukalia! Uchumi huu ulianza kukaliwa tangu enzi za Nyerere hadi sasa hakuna mabadiriko sana. Rushwa kwa sanaaaa, takrima kwa juu juu zaidi jeuri ya fisadizzzzzz!
ReplyDeleteAnonymous wa kwanza,
ReplyDeleteAngalau wa Kenya wanajaribu....! Au unazungumzia wivu.....? Au wewe hauko dar na kuona adha za usafiri...? Jamani lazima kifanyike kitu Dar ni Jehanam kwa usafiri...
Unaweza kutambua akili ya mtu kotokana na anachokiandika. huyo mchangiaji wa kwanza ameandika utumbo so najua akili yake pia inafanana hivyo. Na ninamshauri pia ahudhurie darasa la lugha!!
ReplyDeletehawa ndio wanatumia kodi zao inavyotakiwa,sio hapa kwetu siasa kila kitu na makundi hovyooo!
ReplyDeletesijui hana macho ya kuangalia kama ujenzi unaendelea au anatanguliza chuki kabla ya kufungua macho.
ReplyDeleteHeri ni kwa wao wafanyao kwa vitendo!
ReplyDeletehebu tembelea hapa pia
ReplyDeletewww.konzacity.co.ke
BIG UP KENYAAAAAA!!!!!!!!
ReplyDeletewabongo ni wivu umetujaa,Angalau KEnya inajaribu maendeleo ya njia.TUige tusione aibu,mazuri kuigwa SI ajabu.Nawakilisha hoja!
huyo anonymous wa kwanza ameshindwa kutofautisha vitu hivi viwili..kuimarika kimiundo mbinu (kuwa na miundombinu ya kutosha) na kutatua matatizo ya usafir hasa hasa foleni na hususan kwenye makutano ya barabara.
ReplyDeleteni mtazamo tu
ahsante
hsm
BIG UP KENYAAAAAA!!!!!!!!
ReplyDeletewabongo ni wivu umetujaa,Angalau KEnya inajaribu maendeleo ya njia.TUige tusione aibu,mazuri kuigwa SI ajabu.Nawakilisha hoja!
twende east twende west,wenzetu ni watu wa kuona mbali muda mrefu.wanapiga airport taveta,wanaanza kujenga reli nchi nzima standard gauge,wanajenga bandari mppya,wanaimarisha barabara nchi nzima achilia hizo flyovers,wana mipango mizuri ya uendelezaji miji tuliokaa nrb ni mashahidi,barabara zao sio mbaya kama anon wa kwanza anavyosema kwani hata dar kuna barabara za ovyo nyingi.UKIZINGATIA UKWELI KWAMBA WAO HAWANA RESOURCES KAMA SISI NA WAMETUZIDI KWENYE KARIBU SECTOR ZOTE UKIONDOA LABDA SEKTA YA MAJUNGU NA KUWANGIANA.WANA AKILI BWANA.SIE TUTAISHIA KULALAMIKA KWENYE MABAR TU
ReplyDeleteNiliwahi kwenda Swaziland na nilikuta wanajenga fly overs Tz.sijui kunani TZ!
ReplyDeleteSiasa ni mbaya sana hapa kwetu
Mdau hapo juu ameponda kuwa ground road ni mbovu. Ukiangalia vizuri utaona hizo fly over bado zinajengwa kwa hiyo ground road sitakuwa sawa baada ya fly over kukamilika. Penye ukweli tusifie jamani, wenzetu wanahitaji pongezi kwa maamuzi magumu yenye manufaa kwa nchi yao. Legacy ya Kibaki inaonekana hata akiondoka kesho. Swali 2015 inakaribia wetu ataacha legacy gani? Hiyo no changamoto ambayo siyo ya kuipuuza.
ReplyDeleteAdha ya usafiri itaisha kama kutakuwa na usafiri wa uhakika, siyo FLYOVERS. Usafiri ukiimarika magari tutapaki na kupanda hizo Icarus Kumbakumba. Nani anapenda kuweka mafuta elfu 15 au 20 kwa siku!Ila wakubwa wetu wanafikiria miradi ya wao kula; FLYOVERS na DART. UPUUZI MTUPU!
ReplyDeleteNdio. At least Wakenya wamejaribu. Sisi Bongo tumebaki kupiga domo tu na kuota ndoto za Alinacha.
ReplyDeleteNi ndoto za Mwenda Wazimu kupata maendeleo ya barabara za juu au hata za chini kama:-
ReplyDelete1.Watu nchini wanashirikiana na Wageni kuiba na kuhujumu mali za nchi!
2.Watu nchini wanaiba Mabilioni na kuweka fedha ktk Mabenki nje ya nchi!
3.Watendaji wanasaini Mikataba mibovu isiyo na Maslahi kwa nchi!,
DUNIA NZIMA KILA NCHI IMESHA FILISIKA KWA MATATIZO YA KIUCHUMI NA KIFEDHA, HAKUNA PA KUKIMBILIA KUOMBA MIKOPO WALA MISAADA!
Je, Tutegemee nani atupe fedha kwa maendeleo ya nchi yetu kama siyo kuzipata kwa rasilimali zetu wenyewe kuzitumia kwa faida na tija na uendeshaji wetu wenyewe?
Ktk suala la maendeleo nchini hatuwezi kufika popote kama:-
ReplyDelete1.Hatuwajibishani kwa Uzembe,Wizi na Ufisadi.
2.Hatuadhibiani kwa kukiuka taratibu za utendaji na makosa kama ya wizi, uzembe na ufisadi.
Ili tuweze kuwa na maendeleo ni wakati umefika sasa kuwapiga risasi Mafisadi waliothibitika na wakwamishaji ,Wapinga maendeleo na maadui wa maendeleo!
IDARA YA USALAMA WA TAIFA NI MUHIMU SASA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU NA KUFANYA MATEKELEZO ILI KUINUSURU NCHI DHIDI YA MAFISADI NA WAPINGA MAENDELEO, AMA SIVYO NCHI ITAZAMA KABISA.
NCHI ZOTE ZILIZOENDELEA MFANO, MAREKANI, ITALY NA UINGEREZA KTK KARNE YA 15 AU 16 HIVI WALIWAPIGA RISASI MABEBERU WAPINGA MAENDELEO WAKAWAACHA MABEPARI WENYE FAIDA ILI KUPATA MAENDELEO NA SASA WAMEPIGA HATUA.
UKICHEZA NA NYANI DAIMA UTAVUNA MABUA, UKICHEZA NA FISI UTABAKI NA MIFUPA MITUPU BILA NYAMA!
yeps wa bongo kazi yetu ni kukaribisha ufisadi tu ndiyo expertise yetu.siyo Kenya tu nchi nyingi Africa yetu hawana tulichonacho ki resources wanajiendeleza, sisi tupigie tu madebe ufisadi.
ReplyDeletewenzetu wanaendelea kwasasbabu kwanza wanaongozwa kwa kutumia elimu tofauti na bongo viongozi hawajiamini ushirikina kwa sana then upeo wa viongozi bongo still ni finyu sana ccm ukiwa mkweli unalogwa au unauwawa so kuendelea ni vigumu sana. mfano mzuri angalia the way wanavyo oparate bandari ya dar unashusha mzigo unalipia kila kitu then unaambiwa baada ya miezi mitatu au sita ndo unatoa mzigo bandari ya mombasa ukishusha tu mzigo unalipia then unaondoka kuna kazi ya ziada inatakiwa kufanyika katika hii tz umasikini wa kifikra unatokana na ccm tukiikataa ccm tmeikataa rushwa .umasikini. ufisadi
ReplyDeletemdau wa juu kabisa unachonga utumbo au matapishi maana huo uchafu uliouona sio uchafu bali ni ujenzi unaendelea
ReplyDeletehuwezi kujenga sehemu na ikawa safi kabla hujamaliza wacha ushamba wako hawa jamaa wakenya wanastahili sifa za hali ya juu
watanzania viongozi wetu watabaki kunufaisha familia zao tu
serikali wakiamua kuchukua kila mihela ya kiongozi alieiba basi tunajenga mpaka metro za chini ya ardhi maana kila fisadi hakosi mabilioni ya wizi.
watanzania endeleeni kula vumbi kudadadadeki mnakubali wenyewe kugawa kura kwa mafisadi kwa kilo za sukari na khanga.
Kinachonifadhaisha zaidi ni kwamba Wakenya wamebadilisha kabisa miondombinu jijini Nairobi na sehemu nyingine za nchi hiyo katika kipindi cha miaka minne tu. Sisi huu ni mwaka wa kumi sasa tunazungumzia flyovers na mradi wa mabasi yaendayo kasi lakini hakuna kinachoendelea.
ReplyDeleteKuondoa tatizo la usafiri Dar ni kitu kidogo sasa wala hakuhitaji kujenga ma "flyover". Weka bei kubwa ya parking hapo maeneo ya katikati ya mji. Weka "toll charge ukiingia katikati ya mji". Ruhusu gari za abiria, maofisi na mabasi tu kuingia katikati ya mji. Jenga mji mwengine maeneo ya mbali na katikati ya mji.
ReplyDeleteWadau wenzangu, nawaomba sana tuzidi kutafakari.. je ni kweli fly-overs ni suruhisho la foleni?? or more traffics? Nimetembea sana duniani na swala la foleni liko pale pale....hata ndani ya Wash.DC!!! ambazo huendana na muda wa kwenda makazini na kutoka makazini, Kwa upande wangu naona cha kufanya ni kusambaza Huduma za jamii ili ziwafikie wengi sio wazifuate--(hii in uhusianao na kukuwa kwa miji). dar fly overs maeneo gani mjini!!!! mtabomoa maghorofa kuapata space!! Tuachieni Old dar na jengeni hizo fly-overs nje ya mji kama mbezi, bagamoyo nk! sio kila huduma lzm watu waje city center!!! Hapo kwa watani zetu nilikuwepo last week, Foleni ni mara tano ya Dar!! pamoja na hizo fly overs!! ... nimewasilisha ktk kuwekana sawa tu!!
ReplyDeleteKusema ukweli foleni ya Bongo ni kama Jehanamu. Wazo langu serikali ingeboresha bara bara za pembeni, kama kuweka lami, nadhani zingesadia sana kupunguza magari kwenye main road. Vile vile namuunga mkono (Anony. wa Tue Mar 13, 08:36:00 AM 2012)anayesema tunaitaji usafiri wa jamii kwani nayo itapunguza magari njiani na kutusave gharama ya mafuta.
ReplyDeleteMtlekibishaje nchi yenu wakati ufisadi unaongoza, mnafikiri mchezo kurekebisha, nyie mkage hivyo,hivyo kwa kuendekeza ufisadi, na kuto kuleta maendeleo katika nchi yenu,
ReplyDeleteKulinga na upepo wa Siasa za Kiufisadi nchini ujenzi wa barabara za juu kama hizi utafanikiwa kama utaelekezwa ktk moja Majimbo ya vipaumbele kama haya:
ReplyDelete1.Kule Monduli Umasaini,
Ili ng'ombe wa Wamasai wasigongwe na magari njia zipite juu.
2.Upande wa Ukerewe kisiwani Daraja kuvuka Ziwa Victoria, liwe juu ili samaki ktika maji wasisumbuliwe na mapanga ya boti na moshi wa injini.
3.Ziwa Magharibi kule Bukoba,
Ili wale Nshomire 'Wasomi' waione BK kwa chini wakiwa juu kwa juu kadiri wanavyosafiri kwenda nyumbani.
4.Meneo ya kanda ya kati pale Igunga Tabora,
Ili Wahindi wachache kanda ya kati wanaohesabika kama 'Wazungu' waione nchi wakisafiri juu kwa juu.
5.Kanda ya Kaskazini kule Upareni.
Ili wale Washana na Wasuya walio juu sana kiufahari kuliko watu wengine nchini waione nchi wakiwa safarini nyumbani.
Fly overs au Njia za juu kama hizi zinajengwa kwa Mamlaka kukusanya mauzo ya Madini kama Almasi, Dhahabu,Uranium,Tanzanite, Gas asilia na vinginevyo ambavyo vipo nchini sio kuwaachia Mafisadi wachache wanaohesabika na kujulikana kwa majina na familia zao na sio Kujengewa kwa kutegemea Msaada wa Wahisani kutoka nje ya nchi ambao wote wamesifiliska Kiuchumi na Kifedha!
ReplyDeleteHuwezi ukalewa pombe Mshahara wako wote kila mwisho wa mwezi,,,,,halafu Ukamtegema Mdhamini nje akuvishe nguo, akujengee nyumba na akulishe maisha yote!
ReplyDeleteNakubaliana na wadau wote isipokuwa mdau wa kwanza, wenzetu wamejaribu japo. Katika hoja zetu, tunatoa malalmiko lakini hatushauri nini kifanyike katika kutatua tatizo la foleni mjini.
ReplyDeleteNingeweza kumshauri Rais katika ishu ya kupunguza foleni, ningemshauri wizara zote zitawanywe nchi nzima nazile nyeti ndiyo zibaki Dar. Mfano, Wizara ya Elimu inande Mtwara au Lindi, Kilimo na Chakula Rukwa, Mbeya au Iringa. Wizara ya Afya Dodoma. Rais aifanye kama amri, asiyeripoti ktk mkoa alio pangiwa anakuwa kajifukuzisha kazi, vijana kibao hawana kazi wamemaliza chuo watajaza nafasi.
Wazo langu ni kwamba, sioni kwanini wizara zote ziwe Dar na mioa mingine hawana hata moja. Zinapo hamia mikoani, mbaenki na huduma zingine zitafungua matawi mengi mikoani nakufanya watu wahamie huko na kupungua from Dar. Kasi ya wathamiaji kuingia dar kutoka mikoani itapungua kama sio kuisha kabisa. Mnaweza kujipangia, kila mwaka zinahama wizara tano to up country.
Tatizo la foleni za Dar ni kuwa, wote tunaingia mjini kwenye wizara na idara mbalimabli mda mmoja na wote tunaondoka mda mmoja.
Kibanga Msese
Idadi ya Majambazi wa Kiuchumi nchini haitoi nafasi kwa maendeleo ya sekta zote ikiwemo ujenzi na miuondombinu kama hii,,,ikijengwa inakuwa na viwango vya chini kama Barabara ya Kilwa ,Bandari Kurasini-hadi Mbagala,,,tunabaki idadi kubwa ya ndoto na mipango ya viganjani kama DART, Daraja la Kigamboni na ''Air Mbuni'' yaani Air Tanzania.
ReplyDeleteSisi ni mabingwa wa mipango na sera nzuri ila inapokuja utekelezaji hapo sasa ndio utawajua watanzania nadhani hiyo thika road ina hizo flyovers na barabara njia nne urefu wa zaidi ya kilometa 34 baada ya hapo ni barabara mbili umbali wa kilometa nyingine 100 yaani uanzie pale ubungo hadi chalinze dual carriage road na hakuna njia panda au keepleft terminal three utapeli tayari umeshastukiwa na wachina wenyewe wakatupiga mkwara tusije wachafua kwenye deal zetu za kiajabu ajabu nenda mwenyewe utakuwata wameshatoa hata lile bango, yaani wachina ndio wanatuonea huruma kwamba tulitaka kutengeneza lipumba nyingine schupid!
ReplyDeleteILI KWENDA NA KASI YA MAENDELEO NA ULINGANISHI KTK ENEO LETU LA AFRIKA YA MASHARIKI, NI WAKATI SASA BUNDUKI ZIWEPO MEZANI WAKATI WA VIKAO ILI KUWAJIBISHANA BADALA YA MABIRIKA YA CHAI ,VITAFUNIO NA CHUPA ZA VINYWAJI.
ReplyDeleteBILA YA WATU KUWA 'FIRED' WAKATI WA VIKAO ITAKUWA NI MZAHA NA TUKIFANYA MCHEZO TUTAKUWA WA MWISHO KIMAENDELEO TUTAPITWA NA BURUNDI AU MALAWI!
Huyo jamaa hajawahi kufika hata huko kenya
ReplyDeleteKenya wanajua wanachokifanya siyo sisi watanzania tumekalia uswahili tu na majungu majungu. Wewe anon wa kwanza umeshindwa kuelewa barabara ikijengwa na iliyomalizika? naona una shida fulani.....au ndiyo mmoja wa hao tunaowaita waosha kinywa? SHAME ON YOU.
ReplyDelete