Katibu mkuu wa baraza la wazee wa timu ya YANGA katikati mzee Ibrahimu Akilimali akiongea na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya klabu ya Yanga jijini Dar es salaam juu ya ombi la wazee wa klabu hiyo kwa TFF kuwapunguzia adhabu wachezaji wa timu hiyo walioadhibiwa na TFF kutokana na utovu wa nidhamu walionyesha katika mechi kati ya Yanga na Azam baada ya kumpioga mwamuzi wa mchezo huo
Makamu mwenyekiti wa baraza la wazee wa Yanga Bw.Hashim Hasan akisisitiza jambo katika mkutano huo
)Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria katika mkutano huo wa wazee wa yanga wa kwanza kushoto ni Bw Omari katanga wa radio one stirio akifuatilia kwa umakini katika mkutano huo
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Wazee wangu, nafahamu jinsi gani mlivyo na moyo wa huruma kwa vijana waliofungiwa. Hii inaonyesha ni jinsi gani mnavyojali mpira wa miguu. Lakini mpira una sheria zake. Kila kosa linalofanywa na waamuzi, wachezaji, waalimu na hata wamiliki wa timu, lina adhabu zake. Katika adhabu zote zinazohusiana na mpira wa miguu, hakuna ngumi. Tayari hawa vijana wenu wameshasamehewa. Vinginevyo ilikuwa wafunguliwe mashtaka na kama wakipatikana na hatia, basi wangetumikia kifngo kisichopungua miaka miwili. Nafikiri ni vizuri waendelee kutumikia adhabu waliyopata ili iwe fundisho kwao na kwa wachezaji wengine. Wachezaji wanaruhusiwa kumzonga mwamuzi lakini siyo kumpiga. Kama tunapenda mpira wa miguu, basi ni lazima tunzingatie sheria zake. Pia kama tunapenda kuvunja sheria lakini hatupendi adhabe zake, basi tukubali kuwa mpira umetushinda. Hata kama mwamuzi alifanya kosa la kutisha, hakutakiwa kupigwa ngumi. Ni hayo tu wazee wangu.

    ReplyDelete
  2. Hawa wazee mbona hawajalaani kitendo cha kihuni walichofanya wachezaji? Busara zao zingewatuma kwanza kulaani kuliko kuibuka tu na kuwaombea msamaa. Kutolaani maana yake ni kuwaunga mkono wachezaji sasa sijui mtu anayeunga mkono uhuni kama anastahili kusikilizwa.

    ReplyDelete
  3. Masikini Mzee heri alikolala. Yanga imeingiliwa.

    ReplyDelete
  4. kwanza mm naona wangeongezewa adhabu hasa yule kijana aliyefungiwa mwaka 1 pamoja na cannavaro..wapuuzi sana hawa..mim kwa kusema ukweli ni mpenzi wa simba wa msimamo wa kati tu lakin napenda haki zaidi kuliko hio simba..nilipenda sana mpira zamani kuliko sasa...lakini huyo kijana aliyempiga refa,nasema si kwa vile simpenda kwa sababu ni wa timu pinzani,hapana ni kwa sababu hana adabu kwa asilimia 100 nadhani..TFF wakae upya na kumwongezea adhabu pamoja na faini kabisa.
    upande mwingine, TFF pia wasiishie kusema wanampongeza tu kapteni wa timu ya yanga kwa kuwasihi wenzake waache fujo..inapaswa apewe na yeye pongezi ya chochote na si maneno matupu kwa maneno matupu hayavunji mfupa jamani..apewe hongera ya kiasi chochote cha fedha kwa mfano ili iwe motisha kwa yeye binafsi na wengine siku za usoni...kama hilo haliwezekani basi na hawa wengine wasipewe adhabu ya faini ila wafungiwe tu

    huo ni mtazamo wangu tu
    hsm

    ReplyDelete
  5. Hivi baraza la wazee wa Yanga ni chombo halali na kina uwakilishi wake moja kwa moja TFF? Huu ni ukurupukaji, Nadhani hili baraza linatambulika ndani ya klabu yao tu na halina nguvu ya kisheria ya kuagiza TFF. Kikubwa wanachoweza kukifanya ni kuushauri uongozi wa timu yao na wao ndio wanaoweza kuongea na TFF? Hivi ukiwa mzee ndo wa kutumika kuhalalisha makosa na kupindisha sheria? Tatizo la Tanzania saivi kila kitu wanaiga kutoka kwenye siasa. Shame on you Yanga

    ReplyDelete
  6. mtoa maoni huyo wa kwanza na penda kukupongeza kwa lugha ya heshima uliyoa waelezea wazee wetu pia na maelezo yako . Kiukweli vitendo walivyo fanya hao wanaojiita wachezaji kinasikitisha , hasa kwa jamii ikiwa wao kama kioo adhabu waliopewa inawafaa kwani itawaumiza kiuchumi na itawafanya wakumbuke nidhamu

    ReplyDelete
  7. Nakubaliana na mdau aliyesema kuwa wazee hawa walipaswa kwanza kulaani uhuni uliopindukia uliofanywa na wachezaji wa Yanga kabla ya kuomba wapunguziwe adhabu pamoja na kwamba adhabu waliopewa bado ni ndogo kulingana na makosa waliofanya.

    ReplyDelete
  8. kejeli kejeli 2, yeboyebo mnalo mwaka huu!

    Mnakua kama Boom FC au Ashanti khaa!

    ReplyDelete
  9. Mi naona timu nzima na mashabiki wao wangepewa adhabu ya kutotumia Uwanja wa Taifa kwa msimu mzima maana wametuharibia hata sehemu za kukaa timu gani ina mashabiki kama wanachama wa Al-Shababu? au kwasababu hizo nguo zenu zina rangi ya chama tawala basi mnaona na nci hii mmeitawala nyanja zote?adhabu haitoshi TFF waongezeeni zaid na zaid!

    ReplyDelete
  10. Nyie wazee shukuruni kuwa hao wahuni mnaowatetea wamepewa adhabu ndogo. Mwasika pamoja na kufungiwa mwaka mmoja alitakiwa kufunguliwa shitaka la kushambulia (assault) ambalo lingempeleka jela si chini ya miaka miwili. Kwa wale wanaokumbuka, Eric Cantona alihukumiwa kifungo jela baada ya kumtwanga shabiki wa timu pinzani mwaka 1995. Adhabu hiyo ilifutwa baada ya Cantona kukata rufaa. Hii ni mbali ya adhabu ya kufungiwa miezi minane na FA. Baadaye Fifa iliifanya adhabu hiyo kuwa ni ya dunia nzima ikimaanisha kuwa Cantona hakuweza kuikwepa kwa kuhamia klabu ya nchi nyingine. Manchester United tayari ilishamfungia Cantona miezi minne na kumpiga faini ya pauni 20,000. Huku ndiko kusimamia sheria za mchezo na kudumisha nidhamu, lakini Bongo tunatetea ujambazi katika soka halafu tunategemea tufanye vizuri katika michuano ya kimataifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...