Basi la daladala linalofanya safari kati ya Ubungo na Tegeta, Dar es Salaam, likisimamishwa ili liungane kwenye mgomo ulioitishwa na madereva na makondakta wa daladala hizo leo kupinga kitendo cha kulipishwa tozo nyingi katika kituo cha daladala cha Ubungo Tanesco.
Daladala zinazofanya safari kati ya Ubungo-Tegeta, Dar es Salaam, zikiwa zimeegeshwa katika kituo cha njia panda ya kwenda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana, baada ya madereva na makondakta kugoma wakidai kulipishwa tozo nyingi katika Kituo cha Daladala cha Ubungo na kutojua fedha hizo zinakopelekwa. Kwa siku hulipa kwanza sh. 1,500 na 500 halafu kila linapofika kupakia abiria hulipishwa sh 400. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Mmoja wa madereva wa zaidi ya daladala 100 zilizogoma, akijielezea unyanyasaji huo
Daladala ikisimamishwa kuungana na wenzao waliogoma
Abiria wakiwa wamekata tamaa ya kupata usafiri wakati Daladala zinazofanya safari kati ya Ubungo-Tegeta, Dar es Salaam, madereva na makondakta wake kugoma wakidai kulipishwa tozo nyingi katika Kituo cha Daladala cha Ubungo na kutojua fedha hizo zinakopelekwa. Kwa siku hulipa kwanza sh. 1,500 na 500 halafu kila linapofika kupakia abiria hulipishwa sh. 400. (PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)
Abiria wanateseka lakini kama itasaidia kuondoa ufisadi/rushwa wamefanya jambo la maana.
ReplyDeleteRais alishasema wakigoma wenye daladala tutembee, shida iwapi? Wagome mpaka mwisho...au nao wanataka mtu ajiuzulu?
ReplyDelete