Mhe. Mwai Kibaki, Rais wa Kenya akipokelewa na Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika mjini Arusha tarehe 28 Aprili, 2012.
Mhe. Rais Kibaki akifurahia burudani ya ngoma mara baada ya kuwasili KIA.
Mhe. Rais Kibaki akiwa na wenyeji wake Mhe. Membe (kulia) na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samwel Sitta (kushoto) mara baada ya kuwasili KIA.
Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Uganda akisalimiana na Mhe. Samwel Sitta, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki mara baada ya kuwasili KIA kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 28 Aprili, 2012.
hapa itifaki imekaaje? Raisi wa nchi kupokelewa na waziri?
ReplyDeletekwani kuna kosa watanzania bwana tusome tuache kuzungumza mambo kwa kukremu.
ReplyDeleteWamepokelewa na waziri nadhani kwasababu hii sio official state visit. Na pia, nadhani hawa wageni wetu hawawasili at the same time. Na kama huvyo, JK angekuwa KIA kwa siku nzima! Ali.
ReplyDelete