Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni (Sefue wa pili kushoto), akifatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Umoja wa Mataifa, Bwana J.Haule (wa pili kulia) watahudhuria vikao vya Maafisa waandamizi wa nchi za Jumuiya za Madola mjini London. Leo walipata nafasi ya kutembelea ofisi za ubalozi wa Tanzania chini Uingereza. Pichani wakiwa pamoja na Balozi Peter Kallaghe (shoto), na Naibu Balozi Chabaka Kilumanga,
Aidha Mhe. Balozi Sefue, atapata nafasi ya kufanya mazungumzo na Maafisa wa Taasisi ya Smart Partneship movement kuhusu maandalizi ya kikao kijacho kinachotarajia kufanyika Tanzania 2013.
Mheshimiwa Balozi, Ombeni Sefue, akiweka saini kwenye Kitabu cha wageni kwenye Ofisi za ubalozi wa Tanzania, London, akiwa na mwenyeji wake Balozi Peter Kallaghe. Picha na Rashidi Dilunga wa Ubalozi wa Tanzania, Uingereza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...