Vijana wadogo wa timu ya ngumi ya Bigright boxing wakiwa katika pozi la pamoja.na kiongozi wao Ibrahim bigright nyuma mwenye miwani na fulana nyeusi
Hawa ni vijana `A`walioanza kuimprove kiasi cha kufanya show za boxing wapo katika muelekeo mzuri wa kuwa mabondia kamili na pengine kutuletea medals na tittles in a future.aghalabu sana kusikia nchini mwetu vijana umri huuu wanapewa kipaumble katika riadha, au boxing.

Ibrahim kamwe`bigright` ambae ni local promoter wa ngumi ameamua kwa dhati kabisa kuwafundisha vijana wadogo mchezo huo. Ibrahim anasema “Mabondia wengi hapa nchini wanapigana ili mradi wanapigana hawana formula zozote,hawajui kujilinda pale wanapoelemewa,hushambulia kwa kubahatisha tu, pia hawajui sheria za mchezo wenyewe yote kutokana na kukurupukia mchezo ukubwani.

Bondia akicheza sparing kidogo anatafuta fight,na akipata fight moja au mbili basi huwezi kumkosoa kila kitu anajua yeye wakati ana mapungufu mengi na hajafikia kuitwa professional boxer.hivyo nimeamua kuwafundisha vijana wadogo ambao wanafundishika .kwani SAMAKI MKUNJE YUNGALI MMBICHI. 

Sio baadae tunailalamikia serikali.sisi tujitahidi then tuiamshe serikali itusaidie,sababu inatulazimu kujua kama serikali yetu imelala katika michezo mingine ambayo pia ndio inayoleta ushindi na sifa ulimwenguni.wenyewe wamelalia soka ambayo hawaiwezi ni kupeana matumaini tu.
Hawa vijana wa timu`B` ambao bado wanaendelea na mafundisho zaidi,ili kufikia muelekeo wa kibondia.
Vijana wa bigright boxing ambao tumezoea kuwaona maukumbini katika pozi wakiongozwa na Abdulbasit ibrahim-bigright jr , issa omar na herman shekivuli waliokaa.
Bigright akimfua mmoja wa vijana wake issa omar.Issa omar ni mmoja wa vijana wanaofanya vizuri keshacheza mara tisa na kushinda yote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kwa tinejaz sawa wajifue, lakini hawa watoto viduchu kabisa jamani si wakacheze cha ndimu, tiari- bado,etc, msije mkawadumaza bure, kama wana syllabus tofauti na wakubwa then it is ok,mfano wasipige push ups za ngumi mpaka wamefika 14 to 15 ili wasije tibua bone growth, wazee wa dojo wanajua haya.

    ReplyDelete
  2. Ankali salama, kwenye hii taarifa hujatuambia Bigright anafanyia hizo shuguli zake sehemu gani ya nchi hii, maana wapo wengine pia ambao wanavutiwa na kazi yake na wangehitaji kumtembelea na hata kutoa misaada kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanyia nchi hii.

    ReplyDelete
  3. napendda kuwapongeza waliowakusanya watoto na kuwapatia michezo ya kucheza ambapo kuna utaratibu mzuri umewekwa. HATA HIVYO...Ndugu Michuzi naomba ufkishe ujumbe wangu kuwa ninamashaka sana na swla la michezo ya ngumi kwa watoto wa umri huo. napenda sana waweze kuwasiliana na madaktari katika kuelimishana. nafahamu kuwa vichwa na ubongo wao bado haujakomaa. pia mtoto sio rahisi kukubali ameshindwa na hiyo ni ngumu kufanya assessment. Sidhani litakuwa jambo linalofaa kuona mtoto anadondoka chini kwa kupigwa ngumi ... i am very much concern. ni hayo tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...