Kiongozi wa Brahma Kumaris Raja Yoga Centre Jijini Dar es Salaam,Sista Dhaerti Patel (kulia) akizungumza na vyombo vya habari kuhusu kuwepo kwa sherehe za Jubilei ya Miaka 75 ya Brahma Kumaris Yoga inayotaraji kufanyika siku ya jumamosi katika ukumbi wa Russian Cultural Club jijini Dar Es Salaam.Kushoto ni Sista Lalita Patel toka Jumuiya ya Brahima Kumaris Raja Yoga iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam
Sister Lalita Patel toka Jumuiya ya Brahima Kumaris Raja Yoga iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam, akizungumza na waandishi wa habari.

Na Pascal Mayalla.

Jumuiya ya Brahima Kumaris Raja Yoga Centre, inayojishughulisha na Meditation (Kutulia na Kutafakari), itaadhimisha Jubilei ya Miaka 75 kwa kufanya mhadhara kwa umma utakaoendeshwa na bingwa wa Meditation, Sister Charadhali kutoka nchini Urusi, siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Russian Cultural Club jijini Dar Es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kituo cha Brahma Kumaris Raja Yoga Center cha Upanga Jijini Dar es Salaam, Sister Dhaerti Patel, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho hayo, alipokutana nao kituo hapo Upanga jijini Dar es Salaam.

Sister Dhaerti amesema, maadhimisho hayo yatahusisha mhadhara wa namna ya kufanya meditation, utaohutubiwa na bingwa wa meditation kutoka nchini Urusi, Sister Chakradhari kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 2:00 usiku katika ukumbi wa jumba la utamaduni la Urusi lililopo mkabala na Hospitali ya Agha Khan ambapo hakuna kiingilio.

Sister Dhaerti ametoa wito kwa Watanzania wa rangi zote, dini zote, rika zote na jinsia zote kujitokeza kwa wingi ili kufahamu kuhusu meditation na jinsi itaklavyowasaiodia kimaisha, na kusisitiza kuwa meditation haina dini, bali huwasaidia zaiodi watu kuwa karibu kabisa na muumba wao.

Aklifafanua kuhusu maadhimisho hayo, Msaidizi wa Sister Dhaerti aitwae Sister, Lalita Patel, amesema Jumuiya hiyo yenye vituo zaidi ya 8,500 duniani kote, ilianzishwa nchini India miaka 75 iliyopita na imekuwepo Tanzania kwa zaidi ya miaka 25 lengo kuu likiwa ni kuwaelimisha watu jinsi kufanya meditation ili kuboresha maisha yao bila gharama zozote.

Mmoja wa wafuasi wa meditation, Bibi. Leonada Peter Kissima, ametoa ushuhuda wa jinsi meditation inavyomsaidia katika maisha ya kila siku ikiwemo kuwa na uwezo wa kutokasirika, kutofanya makosa mbalimbali, kupata uwezo wa kuboresha maisha yake ya kiroho na kujikuta unapata mafanikio makubwa kwenye maisha ikiwemo kufanikiwa kuboresha kipato na kuishi maisha bora.

Maadhimisho hayo, pia yatahutubiwa na mabingwa mbalimbali wa meditation na kuwashuhidia Watanzania waliopata mafanikio baasda ya kupata mafunzo ya meditation kwenye kituo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...