Mbunge mteule wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Leganga, ambako kulifanyika mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wa jimbo hilo leo
 Mbunge wa Arusha mjini Mh Godbless Lema akiwasili mkutanoni
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh Freeman Mbowe, akiwashirikisha wananchma na wapenzi wa chama hicho, kuitikia msemo wa ‘Peoples Power’, wakati wa mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wa jimbo la Arumeru Mashariki, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Leganga leo.
 Mbunge wa Moshi Mjini Mzee Ndesamburo akihutubia
Mistari: Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Mh Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr Sugu, akitumbiza wakati wa mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wa jimbo la Arumeru Mashariki kwa kumchagua mbunge wa Chadema, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Leganga leo. Picha na mdau Joseph Senga
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZINGINE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mfano huu unatakiwa kuigwa na watanzania wote. Hongera Arumeru mmeonyesha njia kwa watanzania!!

    ReplyDelete
  2. Ninafuraha sana watu wa Mikoani/Bara wanapoamua wanakuwa wameamua, huwezi kuwagilibu hovyo hovyo. Wote tukiamua inawezekana!

    ReplyDelete
  3. Wanamgambo wa people's power muko juu, mumefyeka hutuba za kizamani za mzee Mkapa.

    ReplyDelete
  4. Woooh cant blv ths! Mayb CCM got 2 b honest to Tanzanians how? well simmple! The 50yrs were a failer yet they got no words to sell about that number. Now the only option am seeing on CCM's table is some1 from CCM got 2 come up and say u knw wat Tanzanians " WE ARE SORRY" for the 50yrs coz everybody does mistakes then we can wrap up from there, isnt cool?. Live with it or not, is gonna take a long tym for CCM to reclaim it back n' that till CHADEMA makes a mistake.People spoke a lot n' they meant it, tired of CCM as it is right now n' so am I.

    ReplyDelete
  5. Hii ndiyo maana ya maneno yale niliyo waambia, kwamba; msiogope ninyi somesheni tu watoto wenu, hata kama hawapati kazi, kwasababu kupitia hao watu wataelewa maana ya mageuzi, na hiyo gia tuliyo ingiza wala msiitoe,kinachotakiwa sasa ni kuongeza tu mwendo kwa kukanyaga mafuta, lakini gia usibadili mpaka tutachukua nchi,maana watu wamechoka na vituko vya C.C.M.

    ReplyDelete
  6. hawa jamaa wanachukua nchi mda si mrefu

    ReplyDelete
  7. CHADEMA wanatisha. Angalia umati huo!!

    ReplyDelete
  8. Danger for CCM, I they are gone. I cannot wait for 2015 then Chadema will ask all the corrupt officials etc to account for their wealth. It is out monies they are using!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  9. Hapo hapoooooo !

    KITU , BAO LIMEZAMA KIMIANIA

    MATOKEO YA MECHI:

    CHADEMA 1 / LIVERPOOL 0

    Na Mpira umekwishaaa,

    C.C.M Chaliiiiiiii !

    C.C.M ziiiiiiiiiiiiii !

    Michuzi ziiiiiiiiiiiii !

    ReplyDelete
  10. Hotuba za matusi kama za kina Lusinde ndio zinatuangusha CCM. Pia, tuachane na watu ambao wameshachafuka kwenye jamii. Wanatuzamisha wote!

    ReplyDelete
  11. Big up Chadema.
    Siasa za matusi na kiburi cha kuwa na fesdha kmewaponza CCM.Watanzania wameanza kuamka na kujua kati ya pumba na mchele.

    ReplyDelete
  12. lakini hizo alama zao za misaraba ndio zitawafanya tusiwape nchi maana nchi yetu haina udini sasa mkileta udini dasalame mjini hampati kitu watoto wa mjini ndio wanaoweza kukupa nchi au kukukataa habari ndio hiyo.

    mtoto wa zamani wa kariakoo mjini.

    ReplyDelete
  13. Jamani sijafuatilia sana lakini je Zitto Kabwe ameonyesha ushirikiano kwenye hili zoezi? Maana naona timu nzima ya wabunge maarufu na safu ya uongozi wa Chadema upo. Kama hayupo kweli inabidi kipindi kingine aonyeshe ushirikiano. Mana chama ni ushirikiano, chama sio mtu. Umaaraufu wa mtu unatokana na chama. Kama hata onyesha ushirikiano na wanachama na viongozi wengine sisi wanachama tuta mjengea shaka. Na hizi hisia za kuanza kuropoka kuutaka urais bila kupitia taratibu za chama pia hazi onyeshi ustaarabu na ukomavu, mimi mkereketwa wa uongozi bora sioni kama anafanya jambo la busara, na wasiwasi huyu ndio atakuwa anarudisha maendeleo ya chama chetu. Ningefurahi kusikia kama alikuwa mastari wa mbele kwenye hili zoezi. Unafikir kwenye vyama si jambo zuri. nawasilisha

    ReplyDelete
  14. Hongeren chadema haya ndo mapinduzi tunayotaka

    ReplyDelete
  15. big up chadema. we are together

    ReplyDelete
  16. Zito alikuwana majukumu ya kichama kule mwanza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...