Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Diamond akizikonga nyoyo za mashabiki wake kwa moja ya nyimbo zake usiku huu,kwenye hafla ya jioni ya washiriki wa Kongamano la Makatibu Muhtasi nchini,iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
Mwanamuziki Mkongwe wa Bendi ya The Kilimanjaro a.k.a Wana Njenje,Nyota Waziri (kulia) akiimba nyimbo yake ya Gere wakati wa hafla ya jioni ya washiriki wa Kongamano la Makatibu Muhtasi nchini,iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. mnakaribia JUNI mnaanza makongamano mtumie fedha mhakikishe zinaisha kabla ya bajeti.....nchi kama imelaniwa hii, haijui vipaumbele wala muda gani wa kufanya kitu gani.bora tu liende.Makongamano na semina elekezi hayaishi lakini na mambo ndio yanazidi kwenda kombo.

    ReplyDelete
  2. Hizi ndio zile za Madrassa za kuchakaza Kanzu na Vibandiko kuchanika huku Dufu nyingi,,,lakini Uelewa wa Imani chini.

    Semina na Makongamano mengi ukiwauliza wahudhuriaji baada ya wiki chache mbele kila kitu 'walicho elekezwa' wameshasahau!

    Hii ndio hali halisi ya Mambo ktk Tanzania yetu!

    ReplyDelete
  3. Hii kazi ya ukatibu muhtasi ni fani ya 'wadada' tu?

    David V

    ReplyDelete
  4. Ni fani ya wakaka pia ila ndio hivyo tena kinakaka hawachangamkii angalau nursing wanakwenda siku hizi

    ReplyDelete
  5. kukonga NYONYO duuh....

    ReplyDelete
  6. Ndio kazi ya katibu muhtasi ya kina dada tu. Wewe ungependa katibu muhtasi wako awe Dume David V? Hao wanafanya zaidi ya kazi.

    ReplyDelete
  7. Ni wadada tu kutoka na mfumo dume wa kiutawala uliokuwepo zamani. Maana mabosi wengi walikuwa wanaume. Madada hawa pamoja na kufanya kazi nyingine za ofisi, huwa wanawahudumia mabosi kwa kuwaandalia chai, kuwatengeneza vizuri kola ya shati au tai, wakati mwingine huwarusha roho bosi zao.

    Mojawapo ya mafundisho, huambiwa na walimu wao, kuwa katibu muhtasi ni mke wa pili wa bosi.

    Sasa wapi na wapi mkaka awe mke wa pili wa bosi?

    Kwa sasa akina kaka tutaanza kuwaona, kwa kuwa siku hizi mabosi si wanaume tu.

    ReplyDelete
  8. Huyu mwana blog anayezungumzia kuchakaza kanzu na kupiga dufu jingi hapa inahusika vipi katika mada ya masekretary. Una hakika kama hao uwasemao imani zao ni pungufu/ziko chini?

    Hawa ndio wachafua hewa unaowasema sasa. Hii ni platform ya kuzungumzia imani za watu ukilinganisha na uelewa wa hawa makatibu muhtasi?

    ReplyDelete
  9. Nimekupata.Lakini hao unaosema wanafanya 'zaidi ya kazi' kumbuka kwamba wengine wameolewa wana ndoa zao...huoni kwamba kwa kuwahisi hivyo unaleta picha mbaya kwa waume zao(akina dada walioolewa) na jamii kwa ujumla?....Tafakari!

    David V

    ReplyDelete
  10. David V huo nido ukweli. Wewe unapooa kama mamaa ni katibu muhtasari basi umejitolea huo ni ukweli ambao haupingiki. Msome mdau hapo juu "Sat Apr 28, 09:45:00 PM 2012" anakwambia kwenye mitaala yao ya shule "Mojawapo ya mafundisho, huambiwa na walimu wao, kuwa katibu muhtasi ni mke wa pili wa bosi." Sasa tafakari wewe hapo.

    ReplyDelete
  11. Wewe ndiye mchafuaji hali ya hewa. Huo ni msemo tu "kuchakaza kanzu....." na hata "kanzu mpya, shehe yuleyule" katika kupendezesha lugha yetu sadifu. Kwenye blog ni burudani tu. Wewe unaanza kulitazama hilo ki-udini na kuchochea hisia za watu. Tuache sisi wa-tz sasa hivi adui yetu ni mmoja tu; ufisadi. Usitake kutupotezea target kwa ku-manipulate viadui feki kwa kuamsha hisia zako za udini

    ReplyDelete
  12. Wewe David uelewa wako mdogo sana. Ni vizuri umetoa jina lako. Bado hujajua huyu jamaa anakuambia nini? Umesoma shule gani wewe? Ulipasi kweli?

    Anzisha blog yako uandike upinzani wako kwa imani za watu uone kama kuna mtu atakutafuta.

    Mchafua hali ya hewa weee!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...