Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi katika sherehe kuwapongeza wananchi,Wilaya na Mikoa,kwa kuuza sana zao hilo huko katika Uwanja wa Jamhuri Hall Wete Pemba leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha Afya Chimba,Jimbo la Tumbe,alipokuwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya jamii katika Mkoa wa Kaskazini Pemba leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenykiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi cheti Hamad Sais Hamad,akiwa ni muuzaji Bora wa zao la karafuu kwa mwaka 2012,katika sherehe za kuwapongeza wananchi walioshiriki na kuuza sana zao hilo huko katika Uwanja wa Jamhuri Hall Wete Pemba leo.
Baadhi ya wananchi wa Chimba Kaskazini Pemba,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza nao wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha Afya katika Shehia hiyo leo,akiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya jamii katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kushoto) akifuatana na Katibu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Afani Othman Maalim,pamoja na ujumbe aliofuatana nao katika ziara ya kutembelea Bonde la Ukele,kukagua Tuta la kuzuia Maji Chumvi,katika Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba,akiwa katikamziara ya kuangalia maendeleo ya jamii katika Wilaya hiyo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Afani Othman Maalim, alipotembelea Bonde la Ukele,kukagua Tuta la kuzuia Maji Chumvi,katika Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba,akiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya jamii katika Wilaya hiyo leo.(Picha na Ramadhan Othman,Pemba.)
Mbona watu wengi hivyo au ndio...??
ReplyDelete