Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akipanda mti wakati wa kuadhimisha Siku ya Taifa ya Kupanda Miti mkoani Singida iliyoadhimishwa juzi.kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Misitu na Nyuki nchini,Monica Kagya
Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Ezekiel Maige akipanda mti siku hiyo mkoani Singida.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akimuangalia mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Ilengero kupanda mti katika maadhimisho ya siku ya Taifa ya Kupanda miti nchini iliyoadhimishwa Singida.
Ras wa mkoa wa Singida bw. Liana akisaidiana na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Ilengero kupanda mti katika maadhimisho ya siku ya Taifa ya Kupanda miti nchini iliyoadhimishwa Singida.
Waziri wa Maliasili na Utalii mhe. Ezekiel Maige akisaidiana na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Ilengero kupanda mti katika maadhimisho ya siku ya Taifa ya Kupanda miti nchini iliyoadhimishwa Singida.
Waziri wa Mazingira Dkt Telezya Hovusa akiweka mchanga vizuri baada ya kupanda mti kuadhimisha siku hiyo kitaifa mkoani Singida pia.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini -TFS Juma Mgoo mara baada ya kumaliza kupanda mti mkoani Singida.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hivi upandaji miti unahitaki mikeka??? Kama ni hivyo mbona hao watoto wa shule hawakupewa mkeka wakati wanapanga miti???

    Asante Mr. Juma Mgoo kwa kuonyesha mfano utakao kuwa rahisi kufanya vijijini kwa wale wasio na mikeka.

    Wenzangu mnasemaje kuhusu hilo la MIKEKA.

    ReplyDelete
  2. Miti tunapanda kwa show... Baada ya siku 10 hutosikia maendeleo ya hii miti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...