Ndugu Michuzi naomba uwakilishe ujumbe huu katika BLOG yako kwani inasomwa na wengi na inaelimisha pia hivyo naamini itaweza kusaidia watu wengine wakaepuka Ajali kama nitakayoelezea. 

Jana tarehe 29 April 2012 nilikuwa nimetokea Moshi naelekea Dar Es Salaam. ilikuwa jioni ya saa kumi na moja hivi tulikuwa tunapita kama kilomita 60 au 70 kabla ya kufika daraja la Wami. Mbele yetu katika kona kulitokea Basi lililokuwa na jina la KAMPALA COACH ambalo lilitokea Kampala likaingia barabarani kutokea upande wa pili wa barabara kitu ambacho kilisababisha Gari iliyokuwa mbele yangu aina ya NOAH nyeupe ifungu breki za ghafla na pia iingie upande mwingine kumkwepa. mimi niliyekuwa nyuma ya Noah niliweza kupunguza mwendo kwa wakati na kulipisha upande wa kulia likiwa bado halijakaa katika nafasi yake (lane). Baadaye niliambiwa kuwa walitoka nje ya barabara kununua mkaa.

Kwa kweli lilikuwa tukio ambalo lingeweza kusababisha ajali mbaya sana kwa dereveva wa Basi hilo kutojali magari mengine..kitu ambacho mimi naita uzembe wa hali ya juu.

Tuliamua kuwa tukatoe taarifa Trafic ili yule dereva apewe onyo na kuelimishwa. Kwa bahati nzuri tuliwakuta kabla ya eneo la Mandera wakanisihi nibakie pale ingawaje lengo langu ilikuwa apewe onyo na kufuatilia taarifa za Dereva huyo.

Trafic walifanya kazi yao vizuri sana. aliposimishwa dereva huyo alikiri kukatiza barabara na pia kusababisha tatizo hilo ILA cha kushangaza alikuwa mkali na kunitukana kuwa mimi sina busara na pia mimi ndie nilikuwa nikiendesha gari kwa speed!!!!!!!!. 

 Trafic walimsihi kuwa kwa hali ile alikuwa na makosa kwani yeye ndio alikuwa anaingia barabarani na hakukuwa na swala la mtu mwingine kuwa yuko speed au la. pia mimi nilikuwa nyuma ya NOAH sasa itakuwaje mimi ndie nilikuwa na speed. LAKINI KITU NINACHOTOA TAHADHARI NI hiki kifuatacho... 

Abiria walishuka chini na kuanza kusema kuwa ninawapotezea muda wanawahi Dar es Salaam. niliwasihi kuwa mimi ninashughuli zangu ila mimi ni msafiri sana katika njia hizo pia nimeendesha kwa miaka 10 uingereza bila kupata ajali.

 pia niliwaeleza kuwa nimeshuhudia ajali nyingi sana barabara zetu ambazo zinasababishwa na uzembe kama ule. nilisimamisha kwa nia njema yakuona kuwa ajali haitokei.. lakini abiria wao hawajali hayo. ila wachache walishukuru na kuomba radhi. TAHADHARI YANGU NI KUWA MADEREVA WENYE ATTITUDE KAMA HIZO NI MBAYA SANA BARABARANI. 

PIA BASI HILO lilipita kibaha bila kupima katika mizani....Trafic wanaweza kucheki.(pamoja na kuwa mimi sikubaliani na mabasi kupima ila ni sheria ambayo ilivunjwa wazi wazi.) .... na taarifa hizo nizauhakika kwani nimezipata kutoka kwa abiria ambaye kumbe alikuwa ananijua.

Sababu ya kuandika hivi nilipenda abiria wale wasome hii wakizingatia kuwa wakati mimi niko nyuma nilisimama njiani. nilishuhudia ajali pale Ruvu dararajani saa mbili usiku. walikufa abiria pale at least wawili. chanzo kwa haraka niliona gari dogo la abiria lilihamia upande wa pili. kwa kuwa mbele ya ke lilikuwa lori kubwa sio magari madogo kama yetu, yeye alibakia barabarabini wakagongana uso kwa uso. NINAAMINI KUWA WALE MAJERUHI KAMA WANGEWEZA KURUDISHA NYUMA WAKATI WANGEPENDA MTU KAMA MIMI AMSIMAMISHE DEREVA NA KUMUONYA UENDESHAJI WAKE..

MAONI YANGU.
Nalisihi jeshi la Polisi la Barabarani...Trafic waanzishe utaratibu wa kuchukua kumbukumbu ya madereva wanaolalamikiwa na malalamiko yafanyiwe kazi pia watuhamasishe kutoa malalamiko ili waweze kupunguza ajali. kama dereva mmoja analalamikiwa na watu wengi nadhani wanatakiwa wamuondoe barabarani asituulie  watu na kusababishia taifa hasanara.

mimi mdau wa barabarani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. sasa huyo dereva anasema huna busara...busara ni kufumbia macho makosa, hata yaliyokuwa ya wazi!? Watanzania bado tuna safari ndefu ya kubadilika! Tunashukuru mdau kwa kutoa taarifa...yamkini utapata japo wachache watakaoifanyia kazi!

    Mdau
    Vancouver.

    ReplyDelete
  2. Mimi nakubalia sana na huyu mdau. watanzania hatuko serious kwenye maswala ya msingi. abiria wanasema wanawahi dar kama wanauhakika wakufika na dereva mzembe kama huyu. hawa madereva wa mabasi wanatakiwa wawekwe adabu haswa kwenye overtake sheria wanzijua lakini wantumia mabavu na uwezo wao mdogo wa kufikiria.

    ReplyDelete
  3. Pole ndugu yangu..Kuna watu humu huwa wanatoa comments nzuri;Sheria tunazo,zipo lakini.....

    David V

    ReplyDelete
  4. Hongera sana kwa kuwa mvumilivu na kupoteza muda wako mwingi ili kujaribu kurekebisha mambo.

    Hao abiria wanasubiri mpaka gari lipate ajali ndiyo wapayuke eti oooh dereva alikuwa anaendesha vibaya, dereva alikuwa na anakimbia na upuuzi mwengine.

    Nakubaliana na wewe kwamba lazima hatua ichukuliwe ili tuwe na madereva wenye akili na siyo wavuta bangi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...