Ndugu Michuzi, mimi ni mdau mkubwa wa blogu ya jamii ambaye hunihabarisha sana mambo ya nyumbani huku nilipo. Pamoja na hayo habari kubwa siku hizi ni masuala ya siasa nacampaign zisizoisha. Chama cha kimoja cha nguvu ya uma, kinakujaa juu sana katika kuipa changamoto ya chama tawala. Swali la kizushi, hivi campaign hazina kikomo ama muda maalum ambapo watanzania wakakaa kufanya kazi na kuendeleza maisha yao? Jee panapofanyika maandamano ambayo hatimaye vijana huumia hali kadhalika kukamatwa na polisi nani anafaidika? Hoja haziwezi jadiliwa kwa mikutano tuu bila fujo? Kila tafrija, msiba, sherehe na mikutano jee nilazima tuwe kisiasa zaidi kwa mavazi na hoja? Maamuzi ya Mahakama, tume ya uchaguzi au matokeo lazima yazue fujo na kudaiwa ni hujuma. 
Serikali inamapungufu makubwa, na hoja za upinzani ni za msingi sana lakini hatuoni tuna changanya za kuzorotesha maendeleo ya jamii kwa mikwaruzo ya kila siku?

Mungu ibariki Tanzania. 
Tudumishe sifa yetu ya Amani.
Mdau U.K

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kwanza nimpongeze mtoa mada kwa fikra kuntu. Leo baada ya kuona katika blogu hii kwamba Lema kavuliwa ubunge na kwamba kuna uwezekano uchaguzi mdogo ukaitishwa tena nilipata fikra kama za mtoa mada, kuna haja ya katiba kua na misingi inayoeleweka kuhusu uchaguzi. Chaguzi ndogo zinapoteza muda mwingi, pesa nyingi pamoja na kuleta fujo zigine zisizo na maana.

    ReplyDelete
  2. Mada ni nyeti:

    Matatizo yapo pande zote mbili kuwa,

    1.Mtawaliwa wakiwemo Wapinzani na Wananchi kwa ujumla kuchukulia mabmo kwa pupa na jazba bila kufuata taratibu.

    2.Mtawala kutumia Mabavu na nguvu ya ziada ama kuchelea kutoa mwelekeo wa jambo bila sababu za msingi.

    Inatakiwa tujirekebishe kwa pande zote mbili ili mambo yaende sawa.

    ReplyDelete
  3. na pia tofautisha harakati na kampeni

    ReplyDelete
  4. Si Bure.............

    ReplyDelete
  5. Arusha bila mbunge inawezekana bana... si lazima uchaguzi tena au kisheria ikoje hiyo? Ni kweli siasa zinatuchosha sanaa!!

    ReplyDelete
  6. Wametumwa hao. Akashifiwe Lowassa wewe ukafungue kesi wapi na wapi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...