Tunapenda kuwatangazia wadau wote waliowahi kusoma Ifunda Technical Seconday School kwamba kutakuwa na mkutano mkubwa wa kujadili rasimu ya katiba ya umoja wetu, Constitution of Ifunda Technical Alumni Association (ITAA)
MAHALI: URAFIKI SOCIAL HALL - Ubungo
TAREHE: 29 APRIL 2012
MUDA: KUANZIA SAA 8 MCHANA
Karibu: Tujadili na kukubaliana namna nzuri ya kuchangia maendeleo ya shule yetu na kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kimaisha.
Tafadhali usikose na mjulishe kila aliyesoma Ifunda Technical Secondary School!!!!!!!!!!!!!
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na wanakamati Mr. Benson Magehema (0754710846),
Mr. Paul Kasanga (0716777949) au Eng. Norbert Leon (0713551525)
Karibuni sana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Shule kongwe sana hii,sijajua kama bado inatoa vijana 'wakali' kama zamani..Mfumo wetu wa elimu umevurugika sana miaka ya karibuni.Wakati fulani nilikuwa nafanyakazi na kampuni kubwa ya ya 'wazungu'TZ.Wazungu wale walikuwa wanapenda sana kuajiri vijana waliotoka kwenye vyuo vya FTCs,Ardhi Institute,Mzumbe ya enzi zile,IFM,nk.Walikuwa wananiambia ni wazuri(vijana) sana kwenye kazi kuliko 'graduates'.Baada ya hivi kupandishwa hadhi au kubadilishwa kuwa vyuo vikuu..Wale wazungu wakawa tena hawako 'interested' sana na wahitimu wa vyuo vile vile ambavyo vilivyopandishwa hadhi na kuwa vyuo vikuuu......

    David V

    ReplyDelete
  2. Mambo yamebadilika sana sasa. 70s na 80s Ifunda, Moshi Tech , mazengo tanga tech zilikuwa ndio kama special school. Watoto wakali wa hesabu walipelekwa kule na wakitoka wakaenda Technical College kama Dar Tech na Arusha Tech. Huko waliwekewa mizengwe(pass mark za juu sana Minimum B average) wasiende Chuo kikuu. Ndio maana David Technical College product zilikuwa kali. Inapaswa kuangaliwa hili bila mapinduzi ya ufundi maendeleo ya nchi ni ndoto.

    ReplyDelete
  3. david, suala ni maslahi hapa na wala sio hadhi au level chuo. graduates huwezi kumfananisha na FTC holder...mimi nina bahati ya kuwa navyo vyote namshukuru mungu lakin nataka pia kuwa vijana wa kutoka FTC level kwenda chuo kikuu ilikuwa ni changamoto moja kubwa sana, iliyakiwa ufaulu sana sana...

    benson magehema, my classmet ingawa ww ulikuwa electrical mm nikiwa civil,hongera sana kwa hili jaman, tunawaunga mkono ingawa sijajua mnawashirikishaje wale walio mbali kama mm ktk hili nikimaanisha ambao kwa sababu moja au nyingine hawtaweza kufika hapo siku hiyo.
    ahsante

    by eng. hanti
    loptz@yahoo.co.uk

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...