MSIMAMIZI wa tume ya uchaguzi katika jimbo la Arumeru mashariki,Trasias Kagenzi amemtangaza ,Joshua Nasari (26)wa CHADEMA,kuwa mbunge mteule katika jimbo hilo baada ya kuibuka kidedea na kuwabwaga wenzake saba kutoka vyama mbalimbali vilivyoshiriki uchaguzi huo. |
Akitangaza matokeo hayo leo(jana) alfajiri ,Kagenzi alisema kuwa Nasari aliibuka mshindi kwa kupata kura 32,972 sawa na asilimia 54,na kufuatiwa na mgombea wa chama cha mapinduzi ,Sioi Sumari aliyeambulia kura 26,757 sawa na asilimia 42.
Aidha aliongeza kuwa jumla ya wapiga kura waliojiandikisha katika jimbo la uchaguzi la Arumeru mashariki walikuwa ni 127,453,waliopiga kura ni 60,696 ,kura halali zilikuwa 60,036 ,zilizoharibika ni 661.
Kagenzi alisema kuwa vyama vingine vilivyoshiriki ni AFP ambapo mgombea wake alipata kura 139,UPDP kura 18,TLP kura 18,SAU 22,NRA 35 na DP kura 77,hata hivyo alifafanua kuwa hali ya uchaguzi ilienda vizuri kwani hakukuwapo na malalamiko mengi katika kipindi cha kampeni hadi kupiga kura ,ambapo wakazi mbalimbali walijitokeza na kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
Msimamizi huyo mara baada ya kutangaza matokeo hayo alivishukuru vyama vya siasa vilivyoshiriki kinyang’anyiri hicho cha uchaguzi, akidai vimeonyesha ukomavu wa hali ya juu licha ya ya kasoro na dosari ndogo ndogo zilizojitokeza na kutoa wito kwa vya vya siasa kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la upigaji kura ili kuondoa malalamiko pindi mshindi anapotangazwa kwa madai kuwa matokeo yamechakachuliwa.
Alivitaka vyama vya siasa kuiamini tume ya uchaguzi kwani hatua ya kuchelewesha matokeo hatokei maksudi kwa lengo la kutoa ushindi wa mezani kwa vyama vingine ila kinachofanyika ni taratibu za kuhakiki masanduku ya kura pamoja na fomu za mawakala,hiyo aliwasihi wafuasi wa vyama vya siasa kuacha kuitumia lawama ofisi ya msimamizi wa uchaguzi na kutishia kumvamia kwa lengo la kushinikiza matokeo yatangazwe haraka.
‘’wafuasi wa vyama ni vema wawe wavumilivu kwani hatua ya kupiga kelele na kutaka wapatiwe matokeo haraka ,yanakuwa hayana maana kwani utaratibu wa sasa tunatumia vyombo vya kisasa katika kuhakiki matokeo kwa kutumia kompyuta ‘projector’alisema Kagenzi
Akizungumza muda mfupi baada ya kutangazwa matokeo hayo,Nasari pamoja na kuwashukuru wapiga kura wake kwa kumchagua ,aliipongeza tume ya uchaguzi kwa kusimamia vema uchaguzi huo kwani hali hiyo imeondoa malalamiko mengi na pengine yangewea kuibua machafuko na uvunjivu wa amani.
Nasari alisema kuwa kazi iliyombele yake ni kuhakikisha anarudisha fadhila kwa wapiga kuwa wake ambao wamemwamini na kuamua kumchagua kwa kuwatumikia ,ambapo alitangaza kuanza kazi mara moja ya kuchimba visima viwili katika kata Maroroni ambako kuna shida kubwa ya uhaba wa maji.
Katika hatua nyingine Nasari alitaka jeshi la polisi kuwaachia huru wafuasi wa chadema zaidi ya 70 anaoamini ni wapiga kura wake, wanaoshikiliwa katika kituo kikuu cha Arusha kutokana na vurugu zilizozuka eneo la mji mdogo wa Usa River baada ya wafuasi wa chadema kuzingira barabara na kuzuia magari kuingia eneo la kuhesabia kuwa na kusababisha kupigwa mawe na kuvunjwa vioo kwa gari la kifahari la naibu kamishina wa jeshi la polisi nchini ,Isaya Mgulu,lenye namba za usajiri T 859 BWB.
Katika vurugu hizo jeshi la polisi lililazimika kuwatawanya wafuasi hao kwa kuwafyatulia mabomu ya machozi majira saa 3 usiku hadi saa 5 ,ambapo polisi iliamua kutumia sialaha za moto na mabomu kuwatawanya wafuasi hao waliokuwa na jazba wakizuia gari la aina yoyote kupita na kwenye eneo la chumba cha majumuisho wakidai yanapitisha kura chafu kwa lengo la kuchakachua matokeo.
Polisi ilifanikiwa kuwatia mbaroni wafuasi zaidi 70 wa chadema na wanashililia katika kituo cha polisi mjini Arusha ,hadi (leo)jana asubuhi walikuwa bado wakiendelea kutoa maelezo kituoni hapo.
Kaka Joshua hongera, pili nawapongeza watu wa Arumeru kutambua umuhimu wa kuwa pamoja na kuinuana muda wa kuangalia nyuma ulishapita sasa tuende mbele maana kuna mengi hatujafanya ambayo yanatufanya wenzetu wakitembea sisi tukimbie.
ReplyDeleteAm so happy for you i know you can make it because God is with you. Wosia wangu nakujua wewe ni familia ya dini na unamjua Mungu kamwe usichanganye Mungu na chochote endelea kuwa muombaji ili kuzishinda nguvu na mishale ya adui no way u can make it bila Mungu,amini ndo umeanza mapambano na kuyashinda ni kusimama na Mungu, i will pray with you. Ni mimi Dada yako Eunice Doto-Uk
CCM INABIDI IBADILIKE MNO. NA MADILIKO YAANZIE JUU CHIBNI SIYO CHINI JUU.
ReplyDeleteHAWA-SOUND KAMA WANA MALENGO KABISA TAZAMA HATA MOTTO WAO "CCM OYEEEE" INAMAANA GANI HII? WATANZANIA WANATAKA SERA NA VIZIBITISHO HARISIA NA SI POROJO TENA, MMEKAA MADARAKANI MIAKA 50.
HUWA NIKIFIKAGA KIJINI KWA MAMA YANGU HUWA NAWATIZAMA WAKAZI WA PALE SIWAMALIZI. TANGU NAANZA KUAPATA AKILI MIAKA YA 80 NI CCM TU WANAONGOZA. BARABARA SI YA RAMI, MJI UNAKAUKA JINSI SIKU ZINAVYOENDA, UMEME SI WA UHAKIKA YAANI WANAISHI MAISHA YA TABU TUPU. LAKINI KILA WAKATI WANAPEWA AHADI HEWA MAENDELEO YANAKUJA SASA, PUMBAVU KABISA. WANAFANYA WAZEE WALE WOTE WAJINGA.
MAENDELEO GANI YANAKUJA BILA BARABARA SAFI, BILA RELI,BILA UMEME WA UHAKIKA. INAUMA SANA.
MAMA MMOJA ALIJITOLEA KUTAFUTA WAZAMINI WAKAJENGA KIZAHANATI PALE KIJIJINI MBUNGE ALIPOSIKIA ZAHANATI IMEKAMILIKA WA KWANZA KUJA KUTAKA KUIFUNGUA.
WALE WATU NADHANI WAMESAHAULIKA KABISA. MBUNGE WAO NI MAMA MMOJA AMEOLEWA NA WAZIRI MKUU WA ZAMANI AMBAYE ANATOKE MKOA WA KATIKATI YA TANZANIA. HUYO MAMA ANAMAKELELE PALE BUNGENI LAKINI MAENDELEO JIMBONI KWAKE HAIBU TUPU!!!!
NITAWASHAWISHI CHADEMA WAENDE KULE WAKALETE MABADILIKO KUWAAMSHA KUWA WASILALE WANATUMIKIA WANANCHI NA SI FAMILIA ZAO. KAMA HUWEZI KUWATUMIKIA WANAANCHI ACHIA JIMBO WATU WENGINE WAONGOZE.
NAANDIKA HAYA KWA UCHUNGU KWELIKWELI, INAUMA MNO KUONA MTU MMOJA ANAFANYA WENGINE WOTE WAJINGA. NAAMINI SIKU MOJA WATASEMA BASI IMETOSHA ITAKUWA BALAAAH.WALE WATU WANANJAA NA YEYE ANAWADANGANYA KWA KANGHA NA PILAU VITU VYA MUDA MFUPI HALAFU WANAENDELEA KUTESEKA.
MDAU MWANAMAENDELEO NA SI KADA WA CHOCHOTE CHA SIASA
Wanamgambo CHADEMA; mapanga shwaa shwaa dhidi ya Chukua Chako Mapema.
ReplyDeleteKazi iliyopo mbele yenu ni maendeleo kwa umma kama mulivyo sauti ya Umma
People's Power mbele.
Hizi hesabu za tume ya uchaguzi hua zinanikera sana hona hii hapa
ReplyDeletewaliojiandikisha ni 127,453
Waliopiga kura ni 60,696
WASIOJITOKEZA KUPIGA KURA 66,757
hii ni sawa na asilimia 52.4 ya wakazi wa Arumeru Mashariki hawajashiriki kuchagua mbunge inamaana waliojitokeza ni asilimia 47.6 tu hii sio demokrasia ambayo tume ya uchaguzi inaisimamia huku ni kufuja pesa za walipa kodi huku watu wa tume hii wakiwa hawawajibiki ipasavyo kuhamasisha wananchi ili kuleta maana halisi ya demokrasia. Nionavyo mimi huenda kuna wananchi zaidi ya 127,453 ambao hawajajiandikisha kabisa kwenye daftari.
Picha inayonijia hapa ni kwamba kwa kua sio rahisi kwa idadi kubwa ya waliojiandikisha ambao hawakujitokeza kupiga kura kua wamekufa au kuhama Aumeru ndani ya muda mfupi hivyo basi huenda Tume kwa makusudi kabisa imeamua kufinya idadi ya waliopiga kura ili kukinufaisha chama fulani ili kupunguza tofauti ya kura maana binafsi nalazimika kuamini hivyo kutokana na hii tofauti ya 52.4% kua kubwa mno
Nadhani imefika wakati Mwenyekiti wetu aanza kuongea na vijana, sio wazee!. Wazee wanatizama nyuma, with nostalgia!. Vijana wanatazama mbele with hope!
ReplyDeleteMwala Hamad
ReplyDeleteJOshua Nassari,
ReplyDeleteHongera sana dogo, nimekukubali zaidi baada ya kuona ulivyopewa mic ili uwashukuru wananchi baada ya kutangazwa rasmi mbunge wa jimbo lako.uliniacha midomo wazi kwa jinsi ulivyoshusha "verse" kwa kweli wananchi wa arumeru wamekomaa kisiasa, wamechagua kitu kwa kuona kilichopo ndani yake sio kwa sababu ya kupewa kanga/viroba.Hongera sana.