Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo,Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, kuhusu maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM iliyokutana leo mjini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine imeridhia Rais Kikwete kuvunja Baraza la Mawqaziri.

Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.

Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.

Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.

2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.

Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.

Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. BADO MNAPOTEZA MUDA HILO BARAZA LILITAKIWA LIVUNJWE TANGU LILIPOTEULIWA.FANYENI KAZI ACHENI POROJO ZA MAAGIZO,MIKAKATI AHADI,KUSHUGHULIKIA....HIZO LUGHA ZISHAPITWA NA WAKATI NENDENI NA KASI YA WANANCHI MNABAKI NYUMA WENYEWE VIONGOZI WANANCHI WAKO KESHO NYIE BADO MNA JANA YENU.

    ReplyDelete
  2. KULIVUNJA SIO SOLUTION, SOLUTION NI KUTAIFISHA MALI ZOTE ZA WIZI ZILIZOPATIKANA KWA HUJUMA YA HAO WAHESHIMIWA. TUNATOA UJUMBE GANI KWA WANANCHI--->KWAMBA: INGIA MADARAKANI, IBA, FUKUZWA, KAZI KWISHA. HIVYO HATA HAO WAPYA HAWATAKUWA NA WOGA WATAFUATA MKONDO HUO-HUO. MAONI YANGU NI HAO WAHUJUMU WA NCHI WAWAJIBISHWA KWA: KUTAIFISHWA MALI ILI ZIRUDISHWE MIKONONI MWA SERIKALI (WANANCHI), PILI HATUA ZA KISHERIA ZA MAHAKAMA ZICHUKULIWE KAMA NI KUTUPWA LUPANGO NA IWE HIVYO. SISI WANANCHI SASA TUNAANGALIA TUONE UAMUZI WA RAIS TULIEMCHAGUA NATUMAINI HATATUANGUSHA.

    ReplyDelete
  3. Lazima wawajibishwe wafilisiwe mali zao walizo zipata kwa njia ya udanganyifu wizi wa mali za umma vitega uchumi vyao vilivyo patikana kwa njia ya wizi hiyo ipo wazi

    ReplyDelete
  4. Jamani hata sisi wananchi tunao uwezo wa kuwawajibisha. Wananchi mna uwezo wa kujikusanya na kuwafungulia mashitaka hao wahujumu uchumi. Ilimradi tu ushahidi muwe nao wa kutosha

    ReplyDelete
  5. Rais hao bahadhi ya mawaziri ndiyo wanakuanguasha..ebu waondoe mara moja,wataifishwe hizo mali zao zote walizochuma kwenye ufisadi.

    David V

    ReplyDelete
  6. Katika kipindi hiki tunamuombea Mhe. Rais hekima na busara. Aidha twaiombea nchi yetu amani na utulivu.

    ReplyDelete
  7. I think there should be a well stated law on those bandits. They should not be allowed to save the government in anyway. Let them go the village and build Ujamaa villages perhaps. Or else enjoy the money that they have been stilling. It makes me so sad and not to see how Tanzania can move forward.

    ReplyDelete
  8. Cha muhimu ni ADHABU KALI kutolewa kwa 'MAWAZIRI WEZI' waliopatikana kufuatia kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri!

    ReplyDelete
  9. Wananchi hawavutiwi na wingi na urefu wa Vikao vya juu.

    Hamu ya Wananchi ni kuona Adhabu kali inatolewa kwa Wizi wa Mawaziri walioufanya kupelekea wao kuachishwa kazi!

    ReplyDelete
  10. waondolewe kabisa sio kuwapangia sehemu nyingine wakaibe kama mwanzo.Tumechoka na viongozi kama hao ,hawaitakii mema nchi yetu kila siku tunaonekana wachanga ,kumbe kuna viongozi wameshakuwa wakubwa hawako kwenye uchanga tena

    ReplyDelete
  11. Madaktari wetu wanadai maslahi walau mazuri kiasi;;serikali inakuwa haina pesa kumbe kuna wachache wanazidokoa..Hawa nao ni wauaji kwa namna moja au nyingine

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...