Mkurugenzi mtendaji wa New Habari Corporation Bw. Hussein Bashe (kushoto) akimpigia simu mshindi wa zawadi ya gari aina ya Vitz kwenye shindano la Jishindie mchongo Bw. Kassim Ramadhani mkazi wa eneo la Kunduchi mtongani jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (kulia) na Meneja mauzo wa kampuni hiyo Bw. Godbless Urassa (katikati).
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na mhariri mtendaji wa kampuni ya New Habari Corporation wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa, na The African Bw. Prince Bagenda (katikati) mara baada ya kuwasili katika ofisi za kampuni hiyo kushuhudia utoaji wa zawadi mbalimbali likiwemo gari lenye thamani ya shilingi milioni 8 kwa wasomaji walioshiriki bahati na sibu ya Jishindie Mchongo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kutembelea chumba cha habari cha New Habari Corporation wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa, na The African . Kutoka kulia ni Bw. Prince Bagenda mhariri mtendaji na Mkurugenzi mtendaji Bw. Hussein Bashe.
Mratibu wa shindano la Jishindie mchongo lililowahusisha wasomaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa na The African Bw. Essu Ogunde akichanganya karatasi zilizojazwa na wasomaji tayari kwa kuchagua mshindi wa zawadi ya gari aina ya Vitz lenye thamani ya shilingi milioni 8 leo jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (katikati) na Mkurugenzi mtendaji Bw. Hussein Bashe.
Wafanyakazi wa New Habari Corporation wakifuatilia kwa makini fainali za shindano hilo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akiangalia gari atakayokabidhiwa mshindi shindano la Jishindie Mchongo lililoandaliwa na kampuni ya New Habari Corporation wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa, na The African leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...