Mtoto wa hayati Sokoine, Mhe: Namelok E. Sokoine (kulia), Naibu waziri wa Ardhi Mhe Goodlack Ole Medeye na mmoja wa wasimamizi wakishauriana mambo mbalimbali kwenye eneo la jukwaa kuu kabla ya kuwasili kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda.
Wananchi waliokusanyika kwenye kanisa katoliki la kumbukumbu ya hayati Sokoine wakiimba nyimbo za mila za wamaasai baada ya kukusanyika kushiriki misa hiyo. Kanisa hilo lilijengwa kwenye kijiji cha Sokoine Dakawa mkoani morogoro.
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, akiteta na Mbunge wa Mvomero Amos Makala ambaye pia alihudhuria kwenye miza hiyo takatifu ya kumwombea Hayati Edward Moringe Sokoine.
Mtoto wa Hayati Edward Moringe Sokoine, Mhe: Namelok E. Sokoine MP, kushoto na Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani bungeni Mhe: Freeman Mbowe (MP) wakifuatilia misa Takatifu ambayo iliongozwa na askofu wa kanisa hilo Jimbo la Morogoro Telesphory Mkude. Nyuma yao ni ni moja wa waandaaji kutoka Sokoine Memorial Trust, Edward Tunyon
Waziri Mkuu kushoto akishiriki miza takatifu ya Kumwombea Hayati Edward Moringe Sokoine, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dr Mary Nagu.
Mtoto wa hayati Sokoine, Mhe: Namelok E. Sokoine, akisema neno la shukurani baada ya kufanyika misa takatifu katika kanisa hilo. |
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telsphor Mkude baada ya Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye kanisa katoliki, Kigango cha Wami Sokoine jana. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na watatu kulia ni Binti wa Marehemu Soine, Namelok Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu, Mstaafu, Edward Lowassa katika Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, Marehemu Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki, Kigango cha Wami Sokoine, Morogoro jana. Watatu Kushoto ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Mhasham Telsphor Mkude akibariki sanamu ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye viwanja vya Kikagango cha Kanisa hilo katika kijiji cha Wami Sokoine , Morogoro baada ya kuongoza Ibada ya kumkumbuka kiongozi huyo.
Baadhi ya washiriki wa Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, Marehemu Edward Moringe Sokoine wakishiriki katika Ibada hiyo kwenye Kigango cha Kanisa Katoliki cha Wami Sokoine, Morogoro.
Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telsphor Mkude akiteta na Namelok Sokoine, Binti wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Marehemu Edward Moringe Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum katika ibada ya kumkumbuka kiongozi huyo iliyofanyika kwenye Kigango cha Kanisa Katoliki cha Wami Sokoine,Morogoro jana.
Je mke wa marehemu yuko wapi? Je alikuwa na watoto wangapi? Haya ni maswali ya wanafunzi as yanaweza kutoka kwenye mtihani. Huyo alikuwa miongoni mwa heroes kwanini msitujuze mambo yake?
ReplyDeleteKwanini morogoro? Nilidhani alitokea Kilimanjaro. Naomba jibu. Asante.
ReplyDeleteYaani wewe unaeuliza kwanini Morogoro, ama ulikawa hujazaliwa tulipomteza Moringe, au MVIVU, hebu google Edward Moringe Sokoine, utapata jibu.
ReplyDeleteNachokumbuka alikuwa na wake wawili
ReplyDelete,kuhusu watoto sikumbuki vizuri, ila anatokea Arusha,Monduli juu.Ukisikia mzalendo huyu jamaa alikuwa hakuna mfano. Nyerere mwenyewe alisema jamaa alikuwa super.
Morogoro kwa sababu ndipo alipopata ajali ya gari.Wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es Salaam.alizikwa nyumbani kwao Monduli.Kwa taarifa zaid soma http://www.arushatimes.co.tz/2003/42/interview.htm
ReplyDeletewanaouliza kwanini morogoro, ni kuwa ajali ilitokea morogoro. na sokoine sio wa kilimanjaro, ni wa mkoa wa arusha (kama anapotoka pamehamia manyara then other bloggers can clarify)
ReplyDeleteAlipata ajali na kufariki Morogoro ndio sabau ya kumbukumbu kufanyika huko. Kwao ni Umasaini, Arusha.
ReplyDelete