MAREHEMU MWALIMU MUNGUATOSHA KALEBI TEMU
Leo tarehe 29/04/2012 umetimia miaka miwili tangu Mungu alipomuita baba yetu katika makao ya milele. Japo hayupo pamoja nasi kimwili, lakini bado yuko nasi mioyoni mwetu. Tunakumbuka upendo, ukarimu na ucheshi wake, pamoja na mafundisho, maonyo na maelekezo aliyokuwa akitupa. Tunamshukuru Mungu kwa uvumilivu na ujasiri aliotupa tangu baba alipotutoka.
Unaendela kukumbukwa na mke wako Santa, watoto wako na wenzi wao, dada zako, mdogo wako, shemeji zako, wajukuu, vitukuu, marafiki na wanaukoo wote.
“BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE”
Bila shaka huyu Mzee ni kaka yake aliyekuwa Ofisa wa cheo cha juu wa Polisi hapa nchini, Melkizedeck Kaleb Temu, na ambaye baadaye aliishi Rhodesia kufundisha askari Polisi mara tu baada ya uhuru. Afisa huyo baadae aliamua kuchukuwa uraia wa huko. Poleni wana familia,
ReplyDelete