Mwili wa Marehemu kanumba ukiingizwa chumba cha maiti Muhimbili usiku wa kuamkia leo
 Swahiba mkubwa wa Marehemu Kanumba, Ray Kigosi, akiusindikiza mwili ndani
Marafiki wa karibu. Picha na Spoti Starehe
 Mamia ya waombolezaji wa kada zote wanamiminika nyumbani kwa msanii nyota aliyetutoka usiku wa kuamkia leo Steven Kanumba, ambako wakati mipango ya mazishi ikiendelea polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo chake chenye utata. Tamko rasmi halijatoka nasi tunaomboleza huku tukifuatia kwa karibu. Tuvute subira wadau.

Habari za awali ambazo kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni Afande Kenyela amesema kuwa Kanumba alikuwa na kutoelewana kati yake na Mpenzi wake ambazo taarifa za awali zinasema waligombana na Kanumba alisukumwa na kugonga kichwa chini na mpenzi wake ambaye ametambuliwa kwa jina moja la Lulu.
Habari ambazo bado haijazithibitisha zinasema kuwa Kanumba alikuwa akioga ili atoke na ndipo aliposikia mpenzi wake akiongea na simu na mtu mwingine alipotoka kumuuliza ndipo mzozo kati yao ukaanza na katika hali ya kusumunana Kanumba alisukumwa akaanguka na kugonga kichwa chini.
Afande Kenyela alisema alipigiwa simu na ndugu wa Kanumba ambaye walikuwa wakiishi pamoja na Kanumba na walipofika Pale walikuta tayari ameshakata roho ila bado inasubiriwa ripoti ya daktari.
Kamanda Kenyela pia amesema kuwa mpenzi wak
e Maerehemu Kanumba anashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi. Lulu ambaye naye anag’aa kwenye tasnia ya Filamu amekuwa akigonga vichwa vya habari vya magazeti ya “udaku” kutokana na skendo za mara kwa mara za mahusiano ya kimapenzi, ni majuzi tu mwanadada huyu ametimiza miaka 18 tangu kuzaliwa.

Aidha nyumbani kwa marehemu Sinza kumejaa ndugu jamaa na marafiki kiasi barabara ya kwenda Lion kupitia Madukani inapitika kwa taabu.
Kanumba ambaye alizaliwa mwaka 1984 amefanikiwa kuzikonga nyoyo za mashabiki wa tasnia ya movie za Tanzania si tu kwa Tanzania bali hata nje ya nchi pia. Kwa mashabiki wa filamu za kibongo Kanumba alikuwa ni namba moja na kwa kiasi kikubwa aliweza kuweka viwango kwani alikuwa anafaa kwa kila kona kuanzia kuigiza mpaka kuvaa na adamu ya maisha tofauti na ma Super Star wengine hivyo kuwavutia watu wa rika lote. Kanumba anamaliza kipindi chake cha miaka 28 akiwa ameacha kumbukumbu ambayo itaishi kwa muda mrefu.
 Chanzo: Spoti na Starehe 


 Huzuni imetanda kila mahali


 Mmoja wa viongozi wa chama cha wasanii akieleza jambo
MC akitoa matangazo haya na yale


REST IN PEACE STEVEN KANUMBA 1984-2012
We have received the death of Steve Kanumba with shock and consternation.
Steve has been a constant visitor at ZIFF, a keen supporter and has won Awards at ZIFF both in 2010 and 2011.
Steve Kanumba was the most famous of all Tanzania film stars of the Bongo Movies. His is a household name loved and cherished by millions in Tanzania but even many more millions in Burundi, DRC Congo, Rwanda, Zambia, Kenya, Uganda and Nigeria. But what distinguished him from the rest was his affable and amiable character. His reputation and character went in tandem and those of us who knew him were amazed by his liveliness, humour, creativity and filial love. He made and starred in not less than 100 films over the last 10 years. We join all others in mourning this creative son of Africa.
- Martin Mhando

A poem for you my dear friend Steven.
ULALE PEMA PEPONI STEVEN KANUMBA
Ulikuwa mtu mbele ya watu, ukajivika tabasamu cheko na bashasha,
Ulikuwa wa mwanzo na jemadari, kuona mbele na safari kuongoza,
Ulikuwa wa mwisho kununa, ulipokisimangwa kwa kero na ujuvi,
Wewe ulishika panga, ukaingia mwituni na njia kutupasulia!

Eh jiti kuu la mwituni, ndege wema na wabaya watamiapo,
Eh mzizi ulotambaa, ukagusa nyika na bahari kwa pamoja,
Eh mbuyu wa thamani, dawa poa na sumu kali zote zipo,
Eh wimbo wa pozeo, jua la kuchea na na mwezi wa kuchwea.

Nikwambe nini jabali, ulobeba tasnia,
Nikusifuje kwa hili, mbinguni wakasikia,
Leo dunia hulali, Pepo yakutazamia,
Ugone mpheho Steven, Umbudo nakukumbuka.
by Moyo wa Simba
In January, in the foto below, he joined us at the Mini ZIFF festival in Zanzibar. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. I never knew the guy,but he must have been a really likeable chap, what a sad loss, RIP young man, and as for Lulu you will have to live with this for the rest of your life, umeua bila kukusudia, me thinks.

    ReplyDelete
  2. Tujuze sababu, nasikia baada ya kifo lulu alikimbia eneo la tukio. Kale katoto kale?

    Ankali vipi hujaenda Obay Police, please tujuze ya kule au hosp/muhimbili

    ReplyDelete
  3. Yaani siwezi kuamini kuwa Steven Kanumba amefariki! Aklikuja kututembelea mwaka 2007 tulivyokuwa tunashuti ikle simema, Bongoland 2. Nilikuwa nawasiliana naye mara kwa mara. Ilikuwa ndotoyangu kuigiza sinema naye. Na huyo Lulu aka. Elizabeth Michael aligiza kama msichana muuza chapati katika sinema hiyo.

    REST IN PEACE STEVEN KANUMBA!

    ReplyDelete
  4. Rest in peace ndugu/rafiki yetu. Mungu amekupenda zaidi.

    ReplyDelete
  5. Watanzania tumepoteza rasilimali muhimu (human capital) katika kuitangaza tazania na kukukuza utamaduni uliotukuka wa watanzania nje na ndani ya nchi. Dunia ilitujua kupitia balozi wetu mahili kanumba. Mungu ailaze mhali pema peponi - amen . Teophory mbilinyi - mbezi beach

    ReplyDelete
  6. RIP Steven Kanumba, lakini we need to know the truth behind his untimely death. I find this explanation of "alisukumwa akaanguka na kugonga kichwa chini" dubious and very hard to believe. Tuwape muda wachunguzi wafanye uchunguzi wao na kutuambia nini hasa kimesababisha kifo cha Steve.

    Mdau,
    Dar

    ReplyDelete
  7. I would like to send my condolences to the parents, relatives and friends of Mr. Kanumba. May God grant you patient; remember WE ARE FROM GOD AND UNTO HIM WE SHALL RETURN. Nonetheless, judging by the pictures in here, it appears to me that so many of us have been caught in the materialism trap to the extent that when we receive news such as this, we tend to be shocked to the core. Oh! GOD GUIDE US TO REALISE AND HAVE CONVICTION ALL THE TIME THAT TO YOU WE SHALL RETURN AND DEATH IS CERTAINTY.

    Mdau, Ughaibuni

    ReplyDelete
  8. It is very sad .. great lost Tanzania. RIP Kanumba.

    ReplyDelete
  9. OMG!What a loss....gone to soon. Rest in Peace Kanumba..

    ReplyDelete
  10. may his soul rest in perfect peace... amen and for u lulu im sorry but u will live with this for the rest of ur life..and of course u will be charged for manslauther.

    ReplyDelete
  11. hii sehemu ni crime scene. uchunguzi utafanywaje?

    ReplyDelete
  12. Mungu amweke pema peponi. Ni kijana mbichi, tutamkubuka daima. Mungu awape nguvu wafiwa. Nasi wengine tujipe subira wakati uchunguzi unaendelea, tuepuke kutoa hukumu kabla ya kupata taarifa ya uchunguzi ingawaje Afande Kenyela keshachemsha kwenye mahojiano.

    ReplyDelete
  13. Lulu has something we want to know. i think there is more to just falling and hitting his head. am so shocked and touched by Kanumba's sudden death. my heartfelt condolences to the family. May his soul rest in eternal peace

    ReplyDelete
  14. Lulu has something we want to know. i think there is more to just falling and hitting his head. am so shocked and touched by Kanumba's sudden death. my heartfelt condolences to the family. May his soul rest in eternal peace

    ReplyDelete
  15. I'm so shocked about kanumba's death...Rest in Peace brother...you were a star!...much respect!
    as for lulu...dah...pole mwaya...i'm guessing hukujua this was going to happen,ila uache utundu mdogo wangu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...