Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, ambaye hivi sasa ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Miujiza, Uponyaji,Kufunguliwa na Mafanikio, Kilontsi Mporogomyi (kulia) akicheza bao na Jumanne Mang'oli wakati wa mashindano ya mchezo huo ya maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Muungano leo kwenye Jumba la Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam. Mporogomyi alishinda. Katikati ni Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania (Shimbata), Monday Likwepa. (PICHA NA KHAMIS MUSSA)
 Baadhi ya wapenzi wa mchezo wa bao wakiwa katika mashindano hayo
                                            Watu mbalimbali wakishindana kucheza bao
Askofu Mkuu Kilontsi Mpologomyi akipongezana na jamaa aliyecheza naye bao Bw. Mang'oli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. SEKTA YA FEDHA hadi YA DINI:

    Bandugu hivi pana uhusiano kati ya Sekta ya Fedha na Dini?

    Duniani sasa mtazamo wa ki-Siasa hutumika zaidi kuwapata Viongozi badala ya Vigezo:

    Mfano ktk kinyang'anyiro cha Uraisi wa WORLD BANK majuzi Marekani imemchagua Jim Yong Kim kwa mtazamo wa Kisiasa na kumwacha Ngozi Okonjo Iweala mwenye vigezo !

    ReplyDelete
  2. Dunia inatisha huyu Kilontsi Mporogomyi ni 'Askofu Mkuu'???Je hilo Kanisa liko wapi tujiunge?

    ReplyDelete
  3. MIONGONI MWA 'SACCOS' CHACHE ZILIZOPO KTK MAISHA YETU SASA ZIPO KATIKA:

    1-DINI
    2-MICHEZO
    3-SIASA

    UKikosa Fedha hapo 1,2 au 3 tangulia mwenyewe Kaburini!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...