Mashujaa watatu kati ya wanne wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar waliobeba vibuyu na chungu wakati wa tendo la kuchanganya udongo wa bara na visiwani lililofanywa na Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Amani Karume katika picha hii hapa chini miaka 48 iliyopita. 


Toka kushoto juu ni Bi Sifaeli Shuma aliyebeba kibuyu kilichokuwa na udongo  wa Tanganyika na kumkabidhi Mwalimu. Anayefuata ni Bw Omar Hassan Mzee aliyebeba chungu kikubwa ambacho ndicho kilichobeba udongo wa Tanganyika na Zanzibar ambao ulipochanganywa tu ndipo Muungano ukawa umezaliwa, na  kulia ni Bi Khadija Rajab Abbas, aliyebeba kibuyu chenye udongo wa Zanzibar. Mara zoezi hilo lilipokamilika ndipo jina Tanzania likaanza kutumika rasmi. Picha ndogo ya kati inaonesha waasisi wa Muungano wakipita mitaani kusherehekea siku hiyo ya kihistoria, huku wananchi wakiwa wamejipanga barabarani jijini Dar es salaam kuwashangilia wakitokea uwanja wa Uhuru.
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete leo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika madhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika katika uwanja wa Uhuru Dar es Salam. 

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es Salam jana,Bi.Mwamtumu Mahiza alisema kuwa sherehe hizo zitaanza majira ya saa mbili asubuhi ambapo milango ya uwanja huo itafunguliwa kuanzia saa 12 asubuhi. 

 ''Sherehe hizi za kiistoria za Muungano zilizo asisiwa na waasisi wetu Baba wa Taifa Julius Nyerere na Hayati Habeid Amani Karume zinatarajia kufana"alisema Bi Mahiza, akiongeza kuwa  viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali watahudhuria  katika sherehe hizo akiwemo Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Mohamed Shein.  

Alisema kuwa katika kipindi cha miaka 48 Serikali imepata mafanikio makubwa ya kujivunia  katika nyanja mbalimbali zikiwemo za maendeleo ya jamii,uchumi,siasa ulinzi,usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa. Kauli mbiu ya mwaka huu ni miaka 48 ya Muungano  shiriki kikamilifu katika sensa na mchakato wa mabadiliko ya katiba. 

''Sherehe hizi zitapambwa na gwaride ,halaiki na ngoma kutoka mikoa mbalimbali Tanzania,ambapo pia aliwaomba  SUMATRA na wamiliki wa vyombo vya usafiri kuelekeza magari yao katika kuelekea uwanja wa Uhuru ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa Dar es Salaam"alisema. 

Aliwaomba watanzania kudumisha Muungano kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho wache kusikia maneno ya mitaani kwa kuwa viongozi waliopita wasisi wetu waliomba tudumishe muungano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Mbona alichanganya pekee yake?

    ReplyDelete
  2. MUUNGANO JUUUUU:

    ASIYETAKA MUUNGANO NI MVIVU NA MZEMBE:

    MARA ZOTE UKISIKIA MTU HATAKI MUUNGANO UJUE ANA KATI YA HAYA HAPA:

    1.HANA KAZI (KWA UZEMBE WAKE MWENYEWE)
    2.MVIVU NA GOIGOI (KILA KITU ANASUBIRI SERIKALI IMFANYIE KILA KITU)
    3.MUDA MWINGI WA MAISHA YEKE AMEUTUMIA AKILEWA NA AKIFANYA ANASA SASA FAINALI UZEENI AMEBAKI MASIKINI ANALAUMU CHAMA NA SERIKALI!

    FAIDA YA MUUNGANO:
    ZANZIBAR-NI VISIWA VIWILI NA MIKOA MITANO (5) TU KAMA SIKOSEI
    TANZANIA BARA-MIKOA ZAIDI YA 32
    SASA WAZANZIBARI HAMUONI NI FAIDA MKIWA RAIA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MNAYO NAFASI YA KUJIVINJARI KWENYE MIKOA 5+32=37 MIKOA ZAIDI YA 37 HIYO?

    KAMA MAISHA YAMEKATAA UKIWA VISIWANI KWA NINI USIJE MIKOA YA BARA UTAFUTE MAISHA YAKO WAKATI ''FURSA'' HIYO NA ''NEEMA'' HIYO UNAYO UKIWA KAMA RAIA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA?

    TUJIULIZE WANDUGU ZETU WAZANZIBARI YAANI WAUNGUJA NA WAPEMBA WALIOPO TANZANIA BARA WAKIFANYA SHUGHULI ZAO NA KUZIKAMATA FEDHA VILIVYO, JE WANAHANGAIKA NA KUUKATAA AU KUPINGA MUUNGANO?

    ReplyDelete
  3. Mday wa libeneke naomba uangalie jina la huyo mtu wa kwanza ni mama Sifael Shuma kama ninavyomfahamu na sio Choma, kama inafaa kurekebisha hapo

    ReplyDelete
  4. ndio hatuutaki mungano mnatunyonya hata kama kisiwa chetu kidogo na kina sehemu ndogo na hizo comment zako ulizotoa hapo juu wewe mdau wa kwanza hazina nguvu yeyote,watu tunapiga kazi ile mbaya na tumejieneleza ile mbaya.leo huu ufe huu mungano na utatuona kama tutaishindwa nchi yetu tizama picha mtu mmoja tu anachanganya mchanga wee acha watu si mazuzu tena tumeshaamka ndo maana tupo bara tunafanya biashara

    ReplyDelete
  5. waznz na wapemba majority wako uk na nchi nyingine za ulaya wakidai wao n wakimbizi sasa wewe unaejidai unapiga kazi ipi na wapi na mansema mnanyonywa kwa kipi hata kuenendeleza zao la karafuu ambalo lilikuwa likiwatoa meshindwa kumbukeni bara kila kitu kipo, mafuta, madini, bandari, mbuga za wanyama, milima kwa ukweli kumekamilika sasa sijui huko tunchowanyonya ni kipi????

    ReplyDelete
  6. si kiengezo kikubwa kuwa uk au nchi nyingine za ulaya unaweza kuwepo hapo hapo na mimi ebwana eeh niko dar nachuma napeleka kwetu na nataka muungano ufee na zao la karafu hebu tuachiyeni wenyewe serikali isingiliye kati muona kama tutashindwa mnajifanya mnatusaidia kumbe mnatuibiya na kutukomoa kisa muungano kuna siku utavunjika huu muungano,
    sina haja ya kumwanga mtama hapa lakini aliye na macho na masikia anajua hilo.
    mnakuja bandarini kila jioni kuchukua mapato yetu na pesa za karafuu zetu wee acha hizoo bado dogo dogo wewe

    ReplyDelete
  7. Mdau Anonymous wa Fri Apr 27, 05:58:00 PM 2012

    Dunia ya sasa yenye hali 'tete' ya Kiuchumi huwezi kuendesha nchi kwa kutegemea zao moja la Kilimo (Karafuu) kwa sababu kuu hizi mbili:

    (1.)Mabadiliko ya hali ya hewa na Tabia nchi:
    (Mvua za mashaka + ukame + kubadilika kwa majira ya hali ya hewa) havitoi nafasi kwa uhakika wa ufanisi ktk mazao na mavuno ya kilimo hivyo Kilimo hakina Uhakika kuwa mhimili wa Kiuchumi kwa jamii ni sawa na kukalia kuti kavu.

    (2.)Hali tete katika Soko la Dunia:
    Kwa bidhaa za mazao pia kufuatia kuyumba kwa Uchumi Duniani zimekuwa ktk wakati mgumu zaidi ya aina zingine za bidhaa ktk soko la dunia( bei za mazao ya kilimo zimekuwa zikidorora ,ushindani ukikua, huku mashariti na taratibu za hali ya bidhaa ziniongezwa na kutoa nafasi ngumu kwa nchi wazalishaji kunufaika na bidhaa zao kwa mauzo.

    UKAE UKIJUA YA KUWA SERIKALI YAKO YA VISIWANI IMEKUWA IKIBEBWA (KIBAJETI NA KIUWEZO KUMUDU GHARAMA ZA UENDESHAJI) NA SERIKALI YA MUUNGANO KUTOKANA NA CHANGAMOTO HIZO MBILI HAPO JUU !

    NI MOJA KWA MOJA KUWA UNAUTEGEMEA NA KUUHITAJI SANA MUUNGANO!.

    KWA HIYO KWA SABABU HIZO KUU HAPO JUU HUWEZI WALA KUTHUBUTU KUUVUNJA MUUNGANO!

    ReplyDelete
  8. BARUA KWENDA VISIWANI KWA WAPINGA MUUNGANO:

    Huwezi kupanda juu ya mti ukiwa na shoka mkononi halafu ukawa upo juu ya mti ukachagua tawi moja (unalolitegemea ukiwa juu ya mti)ukaelekea ukawa katikati ukageuka uanze kukata tawi lilikotokea!

    Kama utafanya ukiwa mzima na akili timamu itakuwa ni masihara tu na utasitisha zoezi lako!

    KAMA UTAFANYA (kama Taahira/ Kichaa) UTAMBUE KUWA UTASHUKA MZIMA MZIMA NA TAWI LA MTI HADI CHINI,,,KIASI KUWA YANAWEZA KUTOKEA MOJA KATI YA HAYA MAWILI:

    (1.)UNAWEZA KUITWA MAREHEMU

    AU KAMA UTANUSURIKA,

    (2.)WATU WENYE AKILI TIMAMU (KAMA MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD) WATAKUZOA KAMA FURUSHI LILILOZAGAA CHINI HALAFU WATAKUWAHISHA HOSPITALI KWA MATIBABU BAADA YA KUVUNJIKA NYONGA AU KIUNGO CHAKO CHOCHOTE MUHIMU.

    WAPINGA MUUNGANO MMEELEWA HADITHI HII?

    ReplyDelete
  9. Anonymous wa Thu Apr 26, 06:01:00 PM 2012

    ....Wewe huutaki Muungano halafu wewe usiyeutaka huo Muungano umeamka upo Bara unafanya Biashara!....

    ''CHANGU CHANGU, CHAKO PIA CHANGU''

    KWELI WAZANZIBARI HAMNAZO!

    Una akili au huna akili?, sasa huoni kuwa nafasi ya wewe kuja kufanya biashara Bara ndio faida ya Muungano?

    Kwa nini usidendelee na biashara zako hukohuko kwenu Zanzibari?

    ReplyDelete
  10. Wazanzibari mmechelewa sana kuvunja Muungano!

    Kama ni hivyo Maalim Seif Shariff Hamad ameingia muda mrefu ktk Serikali ya Mseto kwa nini hajafanikisha kuvunja muungano wakati ndio yalikuwa madai yake makubwa?

    Au kama yeye Maalim Seif anachelewa kwa nini wewe mlalamikaji usiuvunje muungano?

    Nafikiri Maalim asingechukua hata wiki moja kumaliza kazi hiyo tokea aingie Ofisini.

    Je, Anangoja nini?

    ReplyDelete
  11. Wewe Mzanzibari wa Thu Apr 26, 06:01:00 PM 2012

    Utaendelea kutawaliwa na SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA hutaki unataka.

    La zaidi utakufa wewe zako zikifika, Muungano utaucha ukizidi kushamiri!

    ReplyDelete
  12. Mzanji Anonymous ...Thu Apr 26, 06:01:00 PM 2012

    Mnapata Uhuru mkubwa na Neema kwa kupitia Muungano!
    (1.)Mnalewa pombe kwa uhuru kabisa mkiwa Bara, kwenu mnalewa kwa 'siri'

    (2.)Wengi mnavuta, neema hiyo mnaipata mkiwa Bara tu.

    (3.)Mnapata Mademua huku Bara,,,mnatugongea sana tu, neema hiyo kwenu adimu!,,,huko kwenu watu wanagongana kwa 'siri' wakati mwingine watu wanapiga jinsia moja!, unaona balaa lenu hili?

    Angalia kule kwenu hamkutaki kabisa, mnadai hamuutaki Muungano lakini mnapenda kuishi Bara, sasa wapi na wapi?

    SI MNAONA NEEMA ZA BARA HIZO KUPITIA MUUNGANO?

    ReplyDelete
  13. Ninyi Wazanzibari ndio wahitaji wakubwa wa Muungano!

    Sisi tunawabeba na la zaidi tunatumia Ustaarabu kuwa haipendezi mrudi kwenu halafu muwe mnakuja huku kwa kutumia Paasport na kuishi kwa vibali!

    ReplyDelete
  14. Wazanzibari starehe na maisha mnayapata mkiwa Bara!

    Kwenu ni GEREZANI kila kitu kwa siri hadi dishi bovu kabisa mnakula wali kwa mchele 'chereko chereko' , mtu akipika wali nyama 'kitoweo' cha kulenga, mchuzi chukuchuku hauna masalo!

    Starehe zingine ndio kama Mdau alivyoshusha juu hapa ametuchambulia kwenye Jamvi kuwa starehe fulani fulani Wazenji mnazipatia huku nchi kavu sio.

    Mbaya zaidI msituletee mpango wenu wa 'jinsia moja' (msituletee us..ge wenu huku) sisi sio biashara yetu hiyo, huku kwetu kama ni Pombe mtakunywa muwezavyo, mtavuta saaana na Mademu wapo lakini hizo zenu huko huko kwenu!

    KARIBUNI TANZANIA BARA MSTAREHE!

    ReplyDelete
  15. Mtoa maoni wa kwanza:

    ....Mbona alichanganya peke yake?....

    Wewe ulitaka achanganye na nani? ,na baba yako?

    Au ulitaka achanganye na watu wa Kisiwa chote cha Zzanzibar?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...