Bw. Michael Edward Kimemeta - Baba Lulu
Picha na Habari na Dixon Busagaga wa 
Globu ya Jamii, Moshi


Baba mzazi wa Muigizaji wa kike wa filami nchini   maarufu kama Lulu, ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba,  ameibuka na kueleza kushtushwa  sana na  taarifa za kifo hicho pamoja na habari kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli na kuwa anahusika na kifo chake.

Baba Lulu,  ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta(49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo,  Mkoani Kilimanjaro, kaiambia Globu ya Jamii leo huko Moshi kuwa alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu wa mtoto wake Lulu,lakini hakuamini  masikio yake baada ya kupata  taarifa za kifo hicho,  huku bintiye, anayedaiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu, anahusika.

Lulu alifikishwa mahakamani jana April 11, 2012 akikabiriwa na mashtaka ya mauaji ya  Marehemu
Steven Kanumba, ikiwa ni siku nne baada ya kifo cha msanii huyo.

Alisema kuwa Elizabeth ama Lulu alizaliwa tarehe  April 17,1995 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, na kwamba  alimaliza elimu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya  Midway  mwaka jana na kamba hivi sasa ana umri wa miaka 17.

Bw Kimemeta  alisema kuwa ni vyema polisi kuwa makini katika uchunguzi wao  kwa kuzingatia kuwa tukio hilo limejenga chuki na uhasama  baina ya Lulu na ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wa marehemu Steven Kanumba.

Alisema kuwa kilichomshtusha zaidi ni taarifa za polisi kusema kuwa kulitokea ugomvi kati ya Marehemu Steve Kanumba na Lulu,huku ikitajwa kuwa walikuwa wapenzi.

“Hatukutegemea kama Marehemu Kanumba angeweza kuwa na mahusiano y kimapenzi na binti yetu; kwanza ndiye tuliyekuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa
katika kuendeleza na kukikuza kipaji alichokuwa nacho Elizabeth”, alisema baba mtu.

“Ninaomba Wanasheria na wanaharakati wa haki za kibinadamu kuingilia suala hili na  kusaidia katika kupatikana  kwa haki dhidi ya shtaka la mauaji linalomkabili binti yangu  Elizabeth na pia naomba swala hili lisichukuliwe kishabiki ama kwa hisia bali haki ichukue mkondo wake”alisema.

Alisisitiza kuwa jamii inatakiwa kutambua mazingira ya tukio hilo,ambapo chanzo kinasemekana ni  ugomvi uliopelekea tafrani kwa Lulu kutuhumiwa kumsukuma Marehemu Kanumba kwa kile kinachodaiwa kuwa ulikuwa  wivu wa kimapepenzi na haiyumkini hakukusidua kumuua hivyo yeye anashangaa bintiye kuhusishwa moja kwa moja na mauaji.

“Ushiriki wa mwanangu kuhusu mambo ya sanaa nilikwishapata wasiwasi na mama yake mzazi alikuwa akiwasiliana na Marehemu Kanumba enzi za uihai wake ambaye alikuwa anamhakikishia usalama wa  Lulu na kusema kuwa ataendele kubaki kama mwalimu…..lakini leo nasikia  alikuwa ni mpenzi  - nilishtushwa” alisema Kimemeta.

Baba Lulu pia ameelezea kusikitishwa kwake kwa  kushindwa kuhudhuria mazishi  marehemu  Steven Kanumba  kuhofia usalama wake, na kusema  mazingira  yatakaporuhusu hata sita kufika nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba na kutoa pole.

Bw Kimemeta amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia ya Marehemu Steven Kanumba na kutoa mkono wa pole kwa msiba huo mkubwa ambao haukutarajiwa.
Kasema  kuwa Kanumba alikuwa bado ni kijana mdogo aliyeonyesha umahiri kwenye sanaa na kwamba amecha pengo kwa familia yake na Tanzania kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 50 mpaka sasa

  1. kwa kweli wazazi wa elizabeth nasikitika jinsi mlivyomlea Lulu. mwaka Jana Lulu alidanganya umma wa Watanzania kuwa ana miaka 18 lakini hamkujitokeza kukanusha ili aendelee kuwa treated kama mtoto. Leo hii anatuhumiwa na tuhuma za mahuaji ndo mnajitokeza? waswahili wanasema Samaki mkunje angali mbichi, ninyi hilo hamkulifanya. Kanumba kuwa mwalimu wa lulu hakumzuii kumpenda kama Lulu alishasema ana miaka 18 maana tayari alifaa kuandaliwa kuwa mke. Swali jingine kwa wazazi wa Lulu saa sita za usiku binti wa miaka 17 hayupo nyumbani na hayupo location labda anafanya kazi ya kuigiza, alikuwa anafanya nini? hata kama mtoto ana kipaji na kipaji chake kinaongeza pato la familia bado haizuii wazazi kutimiza wajibu wa kumlea, kumlinda na kumwongoza mtoto lakini kutokana na maswala yaliyokuwa yanaaandikwa kwenye magazeti kuhusu lulu ni wazi kuwa wazazi wa Lulu kuna wakati mlijisahau kuhusu malezi ya Lulu. tena mahusiano yake na kanumba yalimsaidia akapunguza skendo na kuandikwa magazetini.
    shime shime kwa wazazi wenzangu tuwajali na kuwalinda watoto wetu badala ya kusubiri maji yakishamwagika ndo tunajitokeza.
    Binafsi naomba haki itendeke pande zote mbili.

    ReplyDelete
  2. That's good Dad. It's never too late to protect your daughter.

    ReplyDelete
  3. Huyu jamaa alikuwa wapi siku zote maana binti yake kila siku media zinaandika habari za kuzibuka kwa lulu mbona hakusimama kama Baba mwe yaani sikujua kama baba yake yuko hai

    ReplyDelete
  4. HUYU BINTI AMEZALIWA TAREHE 17 APRILI 1995. KWA MAANA HIYO UMRI WAKE SASA HIVI NI MIAKA 16!

    ReplyDelete
  5. Ukweli ni kwamba haki ni vema ichukue mkondo wake, lakini hebu tuwe real,
    Nimeshtusha na kauli za baba mzazi kuhusu mahusiano ya kanumba na lulu, tabia za lulu na suala la umri.
    Media kila siku (mara kwa mara) zimekuwa zikieleza mahusiano ya kanumba na lulu.Pia tabia mbovu za lulu hasa ulevi na uasherati mpaka kuna wakati walitoa na picha zake akiwa amelewa kwenye kumbi za starehe, na wakati mwingine alihojiwa na akajibu kauli zinazosikitisha.
    Suala la umri nashindwa kuelewa maana tulimsikia lulu mwenyewe kuwa alifanya birthday ya kutimiza miaka 18,hata hivyo polishi (kamanda wa polisi kinondoni) alipohojiwa na clouds fm alisema "lulu ni mtu mzima kwani ameshatimiza miaka 18 an hana tatizo lolote la kiafya, hivyo hahitaji mtu wa kumsaidia kutoa maelezo yake polisi,na anatoa ushirikiano ktk mahojiano na wakati muafaka ukifika yatatolewa" sasa taarifa ya mahakama kuwa lulu an miaka 17, na hii tarehe ya kuzaliwa iliyotolewa na baba yake vinanikoroga sana.
    Hata hivyo wewe mzazi wa lulu ulikuwa wapi wakati mwanao akiwa bado mdogo sana tena mwanafunzi kila wakati anaripotiwa taarifa za hovyohovyo wewe baba uko kimya (maana yake ulikuwa unaona sawa)
    Jamani haki ichukue mkondo wake lakini tukumbuke pia kumtendea hayati kanumba na watanzania kwa ujumla haki.

    ReplyDelete
  6. Wazazi- wazazi wazazi..kuzaa si kazi wahenga walisema kazi kulea mwana. Baba wa eliza, kanumba hakuwa mwanaume wa kwanz kutembea na lulu au umeshtuka kwa vile alikua mwalimu wake? Umekumbuka shuka kumekucha.. mwanao alipokuwa anamaliza night clubs akiwa na miaka 13 hukua unamuona? ulikuwa wapi kuita wanaharakati wakusaidie? ntaandika hapa mpaka kesho.
    Wewe na mama yake mngemlea huyu mtoto kama mtoto na si kitega uchumi haya yasingemkuta.
    ingawaje naungana nawe kwamba tuache sheria ichukue mkondo wake.
    wanaume kuzaa si kuweka mbegu tu na malezi tusaidie

    ReplyDelete
  7. Ivi huyu baba alikuwa wapi siku zote kujitokeza kwenye vyombo vya habari na dola kuomba msaada juu ya tabia mbovu za binti yake au alikuwa na yeye anakatiwa bakshishi na mwanae.

    Haki itatendeka wala asiwe na shaka kabisa kwani anae jua ukweli ni Mungu pekee na ndiye atakaye tenda haki na itaonekana dunia nzima, na asisahau kuwa kwenye vitabu vitakatifu imeandikwa kuwa ATAKAYE UWA KWA UPANGA NAYEYE ATAKUFA KWA UPANGA. Kwa sasa Kanumba ni marehemu hivyo hatakuwa na jinsi yakujitetea mahakamani na ukweli au haki tunayoiongelea inaweza ikapindishwa ila ni kwa akili na macho ya kibinadamu ila mbele za Mungu haki na utetezi utakuwepo na DAMU YA MTU haikimbiwi.

    Nawaasa wazazi wa Lulu waache kulumbana na jamii kwa kutaka kujieleza kwa mapana nawashauri waongee na Mwenyezi Mungu tu ndio msaada pekee kwao.

    ReplyDelete
  8. Baba Liz, uwe unapitia pitia habari basi hasa zinazomhusu mwanao, hata kama zimeandikwa kwenye yale magazeti yetu...mwanao alifanya pati ya kutimiza miaka kumi 19

    ReplyDelete
  9. haki itatendeka na ukweli lulu ndie aliyekuwa na marehemu mpaka kifo kinamkuta, na kuwa mpenzi wale halina kipinga mizi hata lulu mwenyewe anaelewa ndo wa kumuuliza so mnasema hivyo nyinyi kwa kuwa wa kwenu yu hai lkn angekua hayupo sidhani kama mngechukulia poa kiasi hicho.

    ReplyDelete
  10. Baba mtu aseme tu anaomba msamaha kwa lilotokea, kwani ni bahati mbaya, lakini leo hii akianza na mada kuwa lulu ana miaka 17 tuu, mbona lulu alipotangaza gazetini ana miaka 18 yeye kama mzazi alinyamaza! eti lulu ni mdogo, mtoto gani mdogo mwenye kujenga zinga la jumba!! alikuwa na mahusiano na mijibaba, mbona walikaa kimnya kama wazazi! amlaumu mkewe, kwani alijua yote ya mwanaye, naye kwa sababu lulu ndo mtafutaji alikaa kimnya, kama yeye kama baba hakujua basi tanzania ilijua. asilete vigezo, ilihali mwelekeo wa mwanae ulikuwa wa kiutu uzima, na si kitoto kama anavyomtetea! kwa usemi wake ni kwamba Marehemu kafanya kosa kutembea na underage, kha, wakati uma wote unajua huyu lulu si mtoto mwenzetu, ni mtu mzima!!! Cmon now baba Lulu, dont go that side!

    ReplyDelete
  11. Mimi jamani bado sijamwelewa huyu baba lulu of course pamoja na mama lulu. Kama wazazi walijua kabisa mtoto wao hajatimiza miaka 18 lakini mambo aliyokuwa anafanya Lulu ni mazito kwa nini hawakuomba msaada kwa hao wanaharakati ili kumnasua huyo mtoto mpaka imefikia hivi ilivyo sasa hivi? Angalau ingeonyesha kuwa walifanya juhudi fulani hata kama ilivyo isingefanikiwa maana. Simhukumu Lulu kwani na me ni mzazi lakini ndugu zangu wote ni mashahidi nguo alizokuwa anavaa huyu binti, kumbi za starehe alizokuwa anaonekana, mabwana aliokuwa anasemekana kuwa nao n.k hivi kweli ni sawa kwa mtoto ambaye hajatimiza miaka 18? Mimi nilifikiri kama wazazi inawezekana walishindwa kulitatua hilo mapema basi walipaswa kuomba huo msaada mapema kwa serikali au hao wanaharakati na si mpaka hali imefikia hivi. Swali langu ni kuwa wakati huu msaada wa wanaharakati sijui utasaidia nini maana kweli anaweza kushinda hiyo kesi akatoka gerezani(na ndivyo ninavyoomba) lakini kisaikologia huyo mtoto anasaidiwaje ili aweze kukabiliana na changamoto atakazokumbana nazo katika jamii. ME NAONA NI KAMA MACHOZI YALIYOCHELEWA.

    ReplyDelete
  12. kwanza ushtakiwe ww kwa kushindwa kuitunza familia mpk mtt anakumbwa na mikasa mikubwa km hii, ulikuwa wapi miaka yote hiyo mtt km huyu aanze majukum makubwa km haya ww upo?sijawahi kumsikia huyu mtt akikutaja km kwl upo we mzee huoni haya? wanaume km nyie inabidi iwekwe sheria mkipatikana tu ni kifungo kwanza alaaa!!!!!

    ReplyDelete
  13. Pole sana mzee ila jaribu kujiweka pia kwenye nafasi na mama na baba kanumba je ungelichukuliaje hili swala? heri kanumba angeumia na kutoka salama ila kafa... Mimi pia ni mzazi naona una tatizo kubwa sana lakini saa zingine kukubali watoto wetu wana makosa ni vizuri.

    Mdau Canada

    RIP Kanumba

    ReplyDelete
  14. MICHUZI SALAAM ALEIKUM KAKA....!
    NIMEFURAHI KUPATA MUDA MWINGINE NIWEZE KUTOA YANGU YALIYO MOYONI INGAWA WENGI HUMU NA LABDA HATA WEWE BINAFSI TUTATOFAUTIANA. LAKINI NAJUA NITAJAJILIBU KUWA WAZI NA MKWELI. KWANZA NIMEFURAHI BABA LULU KAJITOKEZA NA KUMBE LULU HAYUKO PEKE YAKE. PENGINE JAMII INGEJIULIZA NI VIPI NDUGU YETU KANUMBA ALIKUWA ANA TEMBEA NA MTOTO MDOGO WA MIAKA 17 WAKATI YEYE ALITAKIWA KUWA KAMA KAKA YAKE? HAYA LAKINI KUBWA ZAIDI NI PALE RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO ANAPO TOKA OFISINI NA KUINGIA MITAANI KUOMBOLEZA KIFO CHA KANUMBA, TENA MBALI YA HAPO WAZIRI MKUU KAENDA NA BILA KUISHIA HAPO KAMTUMA MPAKA VICE PRESIDENT KWENDA KWENYE MSIBA KAMA MSIMAMIZI WA MAZISHI!! SASA KWELI HAKI ITATENDEKA KWA LULU JAMANI? RAIS ANATOA MCHANGO WA SHS. MILLION KUMI? GIVE ME A BREAK TEN MILLION SHILLINGS WAKATI NCHI HAINA DAWA SHULE HAZINA MADAWATI USAFIRI WA WATOTO WETU MBOVU UMEME HAKUNA KIKWETE ANATOA MILLIONI KUMI ZA MCHANGO? HAYA MAREHEMU NAMKUBARI ALIKUWA MTU MZURI LAKINI KIFO KIMESABABISHWA NA NGONO TENA YA MTOTO MDOGO WA MIAKA KUMI NA SABA? RAIS ANATOA MILLIONI KUMI ANATUMA VICE PRESIDENT KWENDA KUSIMAMIA MAZISHI? COME ON PEOPLE HIVI HAKUKUA NA SHUGHURI ZINGINE ZA KIMAENDELEO ZA KUSAIDIA JAMII? SHILINGI NGAPI ZILITOTEWA KWA WAFIWA WA MABOMU YA MBAGALA, SHILINGI NGAPI ZILITOLEWA KWA WAFIWA WA MGOMO WA MADAKTARI, SHILINGI NGAPI ZIMETOLEWA KWA WATU WALIOKUFA KWA KUTAPELIWA NA BABU WA LOLIONDO? MHESHIMIWA KIKWETE ULITAKIWA KUFANYA KAMA UNAVYOFANYA SIKU ZOTE NYINGI TU ANDIKA UJUMBE KUPITIA VIJANA WAKO SIYO IKULU YOTE KUHAMIA NYUMBANI KWA MAREHEMU. HII INA CHANGIA KUTO PATIKANA HAKI KWA LULU. KWANZA KUNA TETESI BAADHI YA WANA SIASA WALIKUWA WANATEMBEA NA HUYO MTOTO WA MIAKA 17 TUNATAKA KUWAJUA NA WAJIUZURU NYADHIFA ZAO. ASANTE KAKA MICHUZI AGAIN NIMEAMUA KUTOFAUTIANA NA WENZANGU WOTE NINA IMANI HII NI BLOGU YA JAMII NA HAYO NI MAWAZO YANGU BINAFSI.KIUKWELI SERIKARI YA JAKAYA IMENISIKITISHA SANA. FIKIRIA OBAMA NA IKULU YOTE INGEENDA KWENYE MSIBA WA MICHAEL JACKSON AMA WHITNEY HOUSTON NA OBAMA KUTOA $10,000? TENA KWA KIKWETE MBAYA ZAIDI TUNAAMBIWA LULU NI MSICHANA WA MIAKA 17, WAME GOMBANA NA KANUMBA KUHUSU SIMU YA MWANAUME MWINGINE NA KANUMBA KAKASIRIKA LULU KAMSUKUMA KWA SELF DEFENSE BAHATI MBAYA KANUMBA KAFARIKI LAKINI HABARI TUNAZOSIKIA HATA LULU ANA MAJERAHA YA KUONESHA KULIKUWA NA PURUKUSHANI? MWACHENI HUYO MTOTO HANA MAKOSA KABISA TUJIFUNZE WATU WAZIMA KU DATE VITOTO VIDOGO TABIA SIYO NZURI. MICHUZI THANKS FOR GIVING ME TIME .

    ReplyDelete
  15. Haya sasa habari ndio hiyo, he baba wa Lulu kumbe yupo heeee kumbeeee! Michuzi Blog Pongezi kubwa! sante sana ninyi ndio wa ukweli katika mahabari mambo mengi nimeyafahamu kupitia hii blog na kuelimika (imenifundisha mengi!)

    Sasa huu ugomvi inawezekana marehemu alitaka kumbaka Lulu! Kumbe Lulu mtoto mdogo sana huyu, miaka 17 tu! Mwalimu kamgeuka mwanafunzi wake, ingekuwa vipi mwalimu angeshtakiwa kwa kosa la kubaka. Kiukweli ngoja tuone majibu ya sheria dhidi ya tuhuma hizi za mauaji zinazomkabili mtoto Lulu(Elizabeth Maiko)Mungu atubariki.

    ReplyDelete
  16. Pole sana baba Lulu, uliyosema ni ya kweli na naamini sheria itachukuwa mkondo wake sawasawa, tunaungana na wewe kulaani watu wanaoshabikia bila kujua nini hasa kilichotokea. Mungu awape njia wanaoratibu hiyo kesi ili haki itendeke barabara.

    ReplyDelete
  17. Total confusion mara kwenye gazeti la mwananchi baba huyo anasema Lulu ana miaka 16 hapa tunaambiwa tena ana miaka 17 tuamini lipi!!

    Kwa wazazi wa Lulu mnatakiwa kuwa responsible kwa hali aliyofikia binti wenu. Mnawezaje kumpa uhuru mkubwa binti huyo angali bado mdogo kiasi hicho na kumkabidhi mikononi mwa kijana kuwa mwalimu wake!! Nadhani hamkuwa serious na malezi ya huyu binti. Anyway labda bado mtakuwa hamjachelewa mnaweza kuchukua hatua kumrudisha huyu binti kwenye mstari maana anakoelekea siko kabisaaaa. Wazazi muungane ili mumlee huyu mtoto pamoja maana malezi kwa njia ya simu si maelezi hayo. Ni ushauri tu ndugu tusimpoteze huyu binti.

    ReplyDelete
  18. Tunaomba haki itumike binti bado yupo chini ya umli wa 18 tunaomba Ray nae afikishwe mahakamani na wengine wote waliosaini nae mkataba bila ya kuomba vyeti vyake vya kuzaliwa ili kujua ana umli gani

    ReplyDelete
  19. Kifo cha msanii huyu kinasikitisha lakini haki ni lazima itendeke.

    Pigania haki za binti yako usiogope chochote mamilioni ya watanzania walio kimya, wasioonekana kwenye TVs wako nyuma yako.

    Common sense imewatoka polisi kutokana na umaarafu wa marehemu.

    Hii sio kesi ya mauaji, labda kua bila kukusudia. Na kama kweli Liz alikuwa na majeraha, marehemu alikuwa na whisky chumbani,na alimchukua Liz toka nje ya nyumba alikokuwa akiongea kwenye simu na kumuingiza chumbani na kufunga mlango!

    Hakuna kesi hapo, lakini polisi na vyombo vya sheria vinalazimika kuonekana vinafanya haki kwa wapenzi wa marehemu na mkuu wa nchi na waziri mkuu wake.

    Pigania haki ya Liz, kwani haki inaonekana inapindishwa.

    Sufa

    ReplyDelete
  20. BABA WA LULU HIVI UPO????? POLE SANA MZEE MTOTO WAKO ATAKUWA FREE TU COZ HAKUNA KITU KITAKACHOMFANYA AWE NA HATIA MAREHEM SIKU ZAKE ZILIKUWA ZIMESHAFIKA ILI KUWA INASUBIRIWA SABABU,,, ILA MZEE WANGU SIKU ZOTE HIZO ULIKUWA WAP??? WAKAT MTOTO WAKO ANAFANYA MADUDU YOTE YALE,, KUNA SIKU UCKU WA KAMA SAA SABA NILIMKTA MTOTO WAKO MZALENDO PUB HANA WAS WAS MBONA SIJAWAH KUCKIA HATA SIKU MOJA UNA KEMEA VITENDO VYA BINT YAKO??? KUNA MTU MZIMA MMOJA ALIMFATA AKAMUULIZA WEWE MTOT USIKU HUU WATOTO WOTE WAMELALA UNAFANYA NINI??? JIBU ALILOTOA YULE MTOTO NI AIBU ALIMJIBU MTOTO WA KWAKO MIMI MTU MZIMA MWENZIO,, FUNZO KWA WAZAZ WOTE MSILEE WATOTO KAMA MAYAI SABABU YULE MTOTO MLIMUACHA FREE SANA..

    ReplyDelete
  21. Hahahahahahahahaah Hii familia wote wasanii, na michuzi usiibanie hii

    ReplyDelete
  22. inasikitisha sana huyu mtoto alianza mambo ya ngono mapema sana, na sasa mambo ya kasema ati kumbe ana miaka 17??? wakati mwenyewe kaongea wazi zaidi ya mara kama tatu na interview rasmi katoa kudhibitisha kuwa yeye in mwanamke ana miaka 18, hata wanaume wote waliokuwa nae kimapenzi pamoja na yule mmbunge, huyu marehemu, na kadhalika hawastaili kulaumiwa maana hawakujua alidanganya umri wake kwa anasa,
    baba yake anaonekana ni mtu mwenyewe hiyana na ameongea ya maana na naamini sasa kila mtu ataamini kweli ana miaka 17, na sio utata uliokuwepo awali hadi watu kuhisi labda wanajaribu kubadili kushusha miaka yake ili apunguziwe adhabu na kupewa kifungo cha watoto.
    baba yake mzazi anayeishi moshi amehakiki kuwa mwanae ana miaka 17.
    anaonekana mzee poa sana huyu laiti huyu mtoto anguishing na kukua Katika mazingira ya baba yake mzazi asingekuwa hivi,
    mola amlaze pema peponi marehemu kanumba na kama alivyosema baba yake elizabith hapa, tuwe na subra na kuiachia sheria ichukue mkondo wake.

    ReplyDelete
  23. mi naona huyu jamaa anyamaze tu maana kama ni kulea basi keshashindwa na kama aliiachia dunia imlelee mwanae basi asubiri.

    ReplyDelete
  24. Pole baba Lulu. Una wakati mgumu katika kipindi hiki.Ni msiba mkubwa kwa waTZ na pia kwa Lulu pia yuko katika wakati mgumu mpaka. Kwa kila binadamu yoyote angekuwa hivyo. Walikuwa wapenzi kwa vyovyote Lulu hasingechukua hatua ya kumuua mpenzi wake tungoje tu uamuzi wa mahakama.

    ReplyDelete
  25. Nakuelewa sna baba. Mimi pia ni baba na najaribu kujiweke katika nafasi ya yako na napata ugumu sana. Mungu ni mkubwa na haki itatendeka hata kama kuna watakaoweka ushabiki.
    Pole sana na nimekuwa nikifanya maombi ili huyu binti aliyeingia matatani baada ya kupotoshwa aweze kushinda huu mtihani.
    Naamini atashinda na atajifunza jambo hapo. Tupo pamoja Baba Lulu na mimi kwa nafasi yangu kama nitakuwa na mchango niko tayari.
    Mdau wa Mwanza.

    ReplyDelete
  26. Mambo ya mahakama hayaingiliwi na tu walawanaharakati.kuwa mpole baba

    ReplyDelete
  27. Hawa wazazi wanatakiwa walaaniwe kwa malezi mabaya ya mtoto. watu wote wanaomfahamu LULU wanajua kwamba ameanza mapenzi muda mrefu na kama umri anaousema baba ni sahihi basi ni wazi wazazi wake walikuwa mbali naye au walibariki aliyokuwa akiyafanya.

    ReplyDelete
  28. Hivi kweli hawa wazazi wa LULU...walimlea mtoto wao kwa kumtakia mema hapa duniani au walimlea tu kiutandawazi nasema hivi cozi alipohojiwa na yule dada wa kipindi cha MKASI kwa kauli yake HOT LULU alikua anaenda disco akiwa mdogo na walinzi walikua wanampitisha kwa kua alikua star akiwa yeye na marafiki zake..na pia miaka alisema 18....leo hii limemkuta la kumkuta anasema ana 17...akumbuke binaadamu anauwezo wa kumuongopea binaadamu wezake lakini kamwe huwezi kumuongopea MUNGU...sasa swali linakuja kwenu wadau woote wa MICHUZI BLOG...JE HUYU LULU alikua na wazazi na kama alikua nao walikua wapi? na je TZ kuna wizara ya WATOTO...nakuna ngos za kulinda watoto...ni mm mdau wenu macho 10.

    ReplyDelete
  29. kazi ipo miaka 16 mara 17 mara 18 tushike lipi

    ReplyDelete
  30. swala la 'single parenting' yafaa litafakariwe kama tatizo la kitaifa.

    ReplyDelete
  31. hivi baba lulu upo? je ulikuwa unaona maovu yote aliyokuwa anafanya mwanao? acha hili lililotokea la kanumba? siamini km wewwe ni baba kweli mwenye mmapenzi na mtoto wako

    ReplyDelete
  32. Samahani sana Mzee Michael, lakini ukweli ni kwamba kama mwanao atatambulika kua anamakosa nakufungwa maisha, angalau utaweza kumtembelea jela, kumuona na kuongea nae, lakini wazazi wa Kanumba, watamuona wapi kijana wao?? Kwakweli nashindwa sana kuamini kwamba familia yako ilikua haijui kama binti yako wa miaka "KUMI NA SABA" anauhusiano wa kimapenzi na Kanumba,kama karibu Tanzania nzima ilijua na pengine hata nje wa Tanzania inakuaje nyie mlikua hamjui? Or was it just ok because things were ok but now its not ok because she is involved? I honestly pray for the justice to be served for Kanumba family na watanzania kwa ujumla. She didnt only take their son but she took Tanzanian's son! Sheria ya nchi na ya Mungu inasema kwamba kila mtu atavuna anachokipanda. Unagombana na mtu na panga au silaha mkononi matokeo yake yatakua yapi? Km unashika silaha mkononi sidhani km unaamisha ugomvi uishe. Am sorry but as young as she is she needs to face justice, this for all others to know no one is above the law, if she didnt like it she should have seek for help, as simple as that! So tafadhali acheni kusema hayo oooh ni mtoto, if she knew how to go around and get herself involve with things or people above her age then she should go through all she need to through just like any other person! Am sorry but It
    HURT so much to see mtu ame strive kujijenga na kujenga nchi then he has been taken away just like that!! WHY? and for WHAT??

    ReplyDelete
  33. makubwa haya tena leo baba lulu kajitokeza hadharani........ haya yetu macho

    ReplyDelete
  34. Inasikitisha kuona majonzi walioachiwa wazazi wa pande zote mbili. By the end of the day, nadhani itakuwa bora kutouliza maswali mengi zaidi kwani muhusika mmoja tayari hayupo kutoa majibu, so majibu mengi yatakayotolewa yatakuwa ya upande mmoja.

    Baba umesema sawa. Umeongea kiungwana. Ila chonde usijiulize kama hawa wawili walikuwa wapenzi kwani jibu la hilo wanalo wao wawili na Mungu. Inawezekana kabisa walikuwa hivyo kwa marehemu alikuwa mwanaume, na bintiyo ni mwanamke. So you see, it is very posssible after all mapenzi huanzapo wakutanapo wawili (tena siku hizi hata jinsia za aina moja poa pia). So chonde baba, inawezekana na vile vile unaweza wewe usiambiwe kwani labda ndoo walikuwa wanaanza.

    It is sad pia tunaposikia umri wa bintiyo unabadilika kila siku. Leo she tells us she is 18, mara pwaaa kawa 17, kesho tutaambiwa she is 7 if not 8. Hapa inaonyesha jinsi binti naye (tena kwenye interview kibao anasema I am 18, I can make my own decisions, I can do this and that) anavyoweza fanya au sema lolote atakalo akidhania ni sawa, kumbe mbeleni anajiingiza kwenye shida zaidi. Chonde mfundeni umuhimu wa kusema ukweli hata kama hataki ulimwengu ujuwe, laa basi awe ananyamaza tu!

    Nakushauri kama mzazi, huu si wakati wa kuongea sana, acha hata 40 ipite walau. Cha msigi familia yako yaweza endelea mwombea marehemu na binti ambaye yupo selo sasa!

    ReplyDelete
  35. HAKUNA WA KUMBEBESHA HUU MSALABA NI MAMA MZAZI WA LULU TU HIVI NDIO ALIVYOTAKA MWANAE AWE.

    ReplyDelete
  36. Pole Baba Elizabeth hufahamu hata kuhesabu umri wa mtoto wako? Ni miaka 16 atakapofika april 17 2012 ataingia miaka 17.Muachie Mwenyezi Mungu ndio muamzi wa kweli.

    ReplyDelete
  37. Jamani tuongee yoote tunayoweza kuongea kama wanadamu. ukweli wote ni mungu peke yake ndiye anayeju. Nina umri wa miaka 40 sasa sijawahu kusikia marahemeu ameshinda kesi. Hivyo mi nawaomba watanzania wote msimba umeishatokea maisha mengine yaendelee, vyombo vinavyohusika ndivyo vitakavyoamua kuhukumu kibinadamu lakini mungu ndiye atakayetoa hukumu sahihi. sisi wote tunaongea tu hatuwezi kufanya lolote.

    Halafu wazazi na sisi tuwe wakweli. Mimi nimefundisha perfect vision ambapo lulu alisoma akaishia katikati wala hata Form four sijui kama alipata cheti na ni karibia miaka minne to mitano. Sasa baba yake lulu anaposema lulu kamaliza form four mwaka jana midway namshangaa sana, labda kama alisoma kama private candidate sikatati lakini lulu alikuwa mwanafunzi wangu perfect vision miaka kama minne imepita.

    Tuachane na kifo cha kanumba, mungu ndiye yote. Hapa mi naona kikubwa ni wazazzi wa lulu kukaa na mtoto wao na kumfundisha maadili kama watoto wengine. Tuseme ukweli Lulu ni mtoto ambaye kwa mtu aliyesoma Perfect vision anamjua jinsi alivyokuwa anasumbua vichwa vya watu. Sijui kama kweli kalelewa na wazazi wote wawili lakini ni mtoto ambaye ni tatizo. Nashauri wazazi wake akitoka wakae naye chini lasivyo, sasa hivi amepata kesi hiyo but baadaye haitakuwa kesi kwake itakuwa ni umauti. Kwa ujumla aachana na maswala ya wanaume kuna siku watamuua mwenyewe.

    Poleni wazazi wote kwa yaliyotoke. Mungu wape faraja katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  38. Pole sana baba Lulu kwa yote. Nina kuomba kitu kimoja tu mzingatie kama family, acheni kuongea uongo mbele ya vyombo vya habari mnazidi kumchukiza Mungu. Taarifa za umri wa Lulu kuwa ni miaka 17 na si vinginevyo mngekuja nazo mara Lulu alipofanyiwa interview na salama, na kukiri yeye ana miaka 18, hapo ndipo mlipopaswa kutoka kwenye vyombo vya habari na kukanusha uongo wa binti yenu. Au alipofanyiwa party kubwa ya kutimiza miaka 18 pale pia mngejitokeza kukanusha na si leo. Ushauri wa bure mrudieni Mungu na mkabidhi kesi ya Lulu mikononi mwake, na si mnavyofanya sasa. Mnatufanya wananchi tuone kuwa uongo na tabia mbovu za Lulu kapata kwa wazazi! Unaongelea chuki kwa Lulu, hakuna mwenye chuki naye bali tunataka asaidiwe matatizo yake ya kisaikolojia. Ameanza kutumika na wanaume angali mdogo sana na hii imemwaribu kisaikolojia. Acha binti asaidiwe. Endelea kumwombea mwanao na acheni hii tabia ya kutoka kwenye vyombo vya habari wakati kesi inaendelea.

    ReplyDelete
  39. Najua km mzazi lazima utoe maoni uliyotoa,walakini wether umeua kwa kukusudia murder,or kwa kutokusudia yani manslaughter,lazima kunakuwa na na kesi ya kujibu.Sijui kwa age ya Lulu na sheria bongo zinasemaje though

    ReplyDelete
  40. Poleni sana wazazi wa Lulu kwa janga hili lililowakuta..poleni pia na kifo cha Kanumba.Siku zote kifo hupangwa na Mwenyezi Mungu,haya mengine ni sababu tu za kidunia.Nawapa pole sana kwa mtihani huu mlopewa na Mwenyezi Mungu kukipanga kifo cha Kanumba wakati yuko na bint yenu!Sasa mimi sielewi Allahu Ya'allam,,hapo ni kumuumbua Kanumba kutoka na mwanafunzi wake?au bint kama huyo aliyeshindikana apate fundisho?Na haya mapenzi yao watanzania waliyajuwa,au huwo ndo ulikuwa mwanza na mwisho wa kujuwa uhusiano wao?,,Kama ilikuwa haijulika basi kweli wasanii mna siri sana,maana niliona wenyewe kwa wenyewe katika mahojiano wanasema wao kwa wao wanalalana kama wanyama.

    Kwanza nakulaumu wewe baba mtu,mtoto ni baba na mama,,hasa hasa baba ukiwa around mtoto anakuwa anaogopa sana kuliko akiwa na mama peke yake.Haya ndio matokeo ya baba mtu kuwa mbali na wanae,,Hivi unajitokeza sasa hivi maji yameisha mwagika hayazoleki,,ingawa si haki kumshikilia Lulu kwa tuhuma ya mauwaji,na ninamatumaini ataachiwa tu,Lakini Je? hili doa mtalifutaje katika familia yenu?na haswa huyo bint katika kichwa chake nadhani haitamtoka mpaka uzeeni mwake!

    Baba Lulu ungeweza kuangalia mfano mzuri kutoka kwa akina Michuzi,wako busy na blog na kusafiri lakini wanapata muda wa kuwapitia mabint zao shuleni,,(maana siku moja niliona Issah yuko shuleni kwa bint yake kuangalia maendeleo yake.Wewe Baba Lulu uko Moshi Lulu Dar,,Unategemea nini sasa.

    Pia namlaumu sana Mama Lulu,,Siku zote ulikuwa unajuwa kuwa mtoto wako ni mtundu wa kupitiliza,Je ulichukua hatua gani kumdhibiti na hiyo hali,,ukilinganisha umri wake,miaka hiyo ni ya purukushani katika maisha,,Mimi sikatai kuanza usanii akiwa na umri mdogo,,ni jambo jema sana..lakini nahisi wakati huwo ndo ungeanza kumchunga sana wewe mama mtu,,maana alikuwa ni mdogo mno,kuliko kumkabidhi kwa vijana wakulelee,na wakati hawana undugu nae,,,Ulitegemea nini mama Lulu?Na kwa kuwa hii habari ya kifo imetokea,kama isingetokea si ungeendelea kupokea pesa unakula na kumruhusu atoke usiku wa manane kama hapo alipo kubwa na hili janga?

    Najuwa kwa Lulu hii ilikuwa si tukio la kwanza la ajabu,,kitu kilichonistua mimi,kama mwezi umepita nilitumiwa picha na ndugu yangu mmoja akaniambia kuwa,,angalia watoto wadogo walipofikia Tanzania,,Nilistuka kuona picha ya Lulu uchi wa mnyama kapigiwa hotelini,,machozi yalinitoka nilihisi kama ni mwanangu wa kuzaa,,kwa kuwa namkumbuka zamani,,tunamuona katika TV ni katoto kadogo nakasifia kuwa haka katoto kanajuwa kuect sana,,Inasikitisha mno kuona Baba mtu mzima unampeleka hotelini bint mdogo mdogo kama huyo,,kisha unaamua kumpiga picha kisha unazituma katika website,,kwa kweli iliniuma sana,,

    Mwisho nasema hivi,,Hiki kitendo kilichomtokea Lulu ni fundisho kwa kina mama wote wenye watoto wa kike,,na pia ni fundisho kwa akina Baba,na pia ni fundisho kwa watu wote wanaofanya vitendo vichafu kwa siri,,Watu tukumbuke kwamba Kwa Mwenyezi Mungu hakuna siri,,na nawasihi watu wote wenye watoto au ndugu au hao mabint wenyewe,,tusicheke au kufurahiya hili tukio,,kumbuka leo kwangu kesho kwako,,inaweza kuwa bora ya huyo Lulu alisukuma tu,,ikaja wa kwako akauwa kabisa kwa kukusudia,,

    Tunaomba Bint huyu aachiwe kwani hiyo iliyotokea ni bahati mbaya,wangapi wameuwa kwa kukusudia na wameachiwa itakuwa hii,tena walikuwa wapenzi ni wivu tu!

    Michuzi usiibane hii
    Ahlam UK

    ReplyDelete
  41. Alah! Kumbe ni Lulu Kimemeta ni wa miaka 18-1.

    Kifo cha Kanu tunajifunza tabia za wasanii nyuma ya pazia jeusi. Na Kama kioo cha jamii ndio hichi basi kimeshavunjika na hakuna wa kukirejesha tena. kilichobaki ni Kumuombea duwa njema.

    ReplyDelete
  42. Wale wanaodai Kanumba kaanguka na kufa peke yake wanatufanye tuanze kufikiria mengine zaidi.

    Kwanza mimi sijawahi kuona mtuhumiwa anatetewa na serikali yote.

    Mara Lulu ni mdogo, Mara walikuwa wanapigana na hakuna kesi ya m"murder" kwa wanaopigana.

    Hao wanaomtetea Lulu wanamteteaje huku wanalaumu wanaomhukumu?

    Huyu msichana ni mtu mzima kwa kila hali. Kwa nini alikimbia ikiwa hakuwa na hatia yoyote?

    Wale Wa"zito" anaohusishwa nao inakuwaje?

    Ni uchambuzi tu.

    Ikiwa hahusiki Mungu amtetee

    ReplyDelete
  43. Kumbe Lulu ni Mchaga!

    ReplyDelete
  44. yaa mzee pole sana ni unajisikia vibaya kwa mwanao (binti wa miaka 17 recently) amehusishwa na mauaji tena na mapenzi chini ya umri. nakuomba mzazi mwenzangu uwe karibu na mwanao na hawa akina mama huwa wanaharibu watoto. je una habari kuwa ile simu ya mwisho aliyopigiwa Lulu ilitoka kwa mheshimiwa flani?

    ReplyDelete
  45. Jamani Ankal, hivi kumbe Lulu ana baba yake? Ni kwa nini huyu baba asifunguliwe mashitaka kwa kutofanya kazi ya malezi kwa mwanae ambayo yamempelekea kumuingiiza katika matatizo makubwa. Mimi nimeanza kusikia matendo machafu ya Lulu toka miaka 4 nyuma,ina maana alikuwa na miaka 12-13, sijasikia mzazi yeyote akikemea ujinga huo. Leo huyo baba anataka kumbebesha mzigo marehemu Kanumba wakati walimpatia akuze kipaji, na yeye kweli alitii na kuendelea kukuza kipaji cha mapenzi kwa Lulu ikiwa pamoja na kumdhibiti kuwa na wanaume wengi. Mimi nashauri hao wanaharakati wakijitokeza waanze na kufungua mashitaka dhidi ya wazazi wa Lulu, pili ndo waangalie uwezekano wa kumsaidia huyo lulu kama upo. Hili litakuwa fundisho hata kwa wazazi wengine wanaofanya watoto wao kama vitega uchumi. Wakiletewa pesa na mtoto hawaulizi alikotoa, wala hawaiti wanaharakati kuwasaidia. Leo binti kashitakiwa mnaomba wanaharakati wawasaidie na kuomba haki itendeke, aliyewaambia haki haitatendeka ni nani? Hata kama akiwa na miaka 17,siyo sababu ya msingi ya yeye kutohusiswa na mauaji, kwanza wamfungulie kesi zingine kama kudanganya umri ili kupata driving licence,kwenda club,kunywa pombe,kudanganya bank ili amiliki a/c mwenyewe etc. Kesho kutwa atakuwa na 18 kwa mujibu wa baba yake.

    ReplyDelete
  46. Asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu. Na mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Hivyo baba Lulu pole sana, hiyo ndio faida ya malezi mliyoyafanya kwa huyo binti yenu.Hata kama angekuwa na miaka 12 sheria ingemkamata tu.

    ReplyDelete
  47. kama mzazi inaumiza sana lkn kwa suala la lulu jamani tunashindwa kuanzia wapi mana huyu mtoto ilifika mahali watu wanauliza kweli ana wazazi? tabia mbaya na chafu zisizostahili zote anazo huyu mtoto hakusikia la muazini wala mnadi swala sasa mama kabla hujasaidiwa na wanaharakati je ulishawahi kupeleka suala la mwanao na tabia zake huko? sbb wakati mwingine wazazi tunachangia tabia za mtoto huyu lulu angekanywa mapema haya yote yasingemkuta sbb hata hiko kifo siyo yeye alisababisha ni uwepo wake tuu, ila ndio tujifunze kama wazazi siyo kushadadia matendo ya watoto wetu sbb wanatuletea sukari na unga wa kula basi hata anapoharibikiwa hatumsemi,hata kama hakusikia lkn hata siku moja mama lulu sijawahi kumsikia anakemea tabia za mtoto wake,hayasasa ngoma ikilia sana hupasuka tunaanzia wapi? kiusalama huyu lulu aachwe kwanza gerezani mpk hasira za wananchi ziishe maana watamfanyia kitu mbaya tukaja kulaumu baadae. na pia ni fundisho kwake na kwa wazazi wote wanaoendekeza watoto wao, kweli anai anaweza amini mtoto wa miaka 17 kutenda aliyoyatenda lulu mpk kifo cha kanumba? hapo kumbuka huyo lulu alishapelekwaga polisi alivotoka mama mtu alipiga vigelegele akarudishwa so mama cha msingi tuombe mungu akutie nguvu na huruma za watanzania na kumuombea msamaha siyo kuzungumza zungumza nadhani unawajua waandishi wetu. Pole baba kwa kushindwa kulea.Yamekufika,uza nyumba yake kimara ili mlipe mwanasheria tu,hakuna mwanaharakati, tumeweka mgomo kwa Lulu

    ReplyDelete
  48. kwanza ungewashitaki hao 'vijogoo' kwa kuwa Lulu bado alikuwa under 18 (minor) akikota na marehemu. ni suala zito kisheria.
    mdau

    ReplyDelete
  49. Mmhh mi sijawahi kusikia mchaga aliyeacha mke mjini yeye akawa vijijini

    ReplyDelete
  50. Pole sana baba Elizabeti, mungu ataifariji familia yako na ila ya bwana Kanumba kwa Rehma zake.
    Naomba nikufahamishe kitu kimoja tu wewe omba Mungu wako haki itendeke, nchi hii haina wanaharakati bali ina wanamikakati, haki za binadamu maana yake ukitaka kumjua mlevi mmwagie pombe yake, ukitaka kumjua shetani mchokoze kiti chake na ukitaka kuwajuwa wanamikakati kachokoze Chadema, hapo ndio utakapoona haki ikipiganiwa shurti kwa watu kutaka kuvua nguo mabarabarani.
    Yaani hili swala la Lulu ni la kijamii kabisa na linagusa moja kwa moja haki za binadamu, ustawi wa jamii, uandishi wa habari n.k. Tawla kwa mfano wangekuwa mstari wambele kumkinga Lulu haswa kwa vile bado ni mdogo amepata matatizo kama haya wasikubali jamii kumhukumu kwa kupitia magazeti, kituo cha haki za binadamu, kuhakikisha haki yake ya msingi ya kisheria(presumption of innocence) inalindwa hakuna, wako kimya, wangoja watu wazima na akili zao wagome kazi, kwa tamaa na ushabiki siokuwa na maana ndio uwasikie hao wanaojidai wanaharakati wakiita waandishi wa habari midende ya shingo ikiwatoka wakielezea mikakati yao. Baba hangaika kivyako, wako wasamaria wema watukufuata, wako wazandiki utawaona, na jiepushe baba kuingia kwenye makundi ya siasa, haswa wanaopenda kubadilisha vyeti k.m vile vya ndoa, vya kuzaliwa, vya ubatizo, kuwa mkweli na muwazi ndipo haki itakapo tendeka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...