Na Mary Ayo,Arusha

MKUU wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo  amewataka wananchi wa mkoa huo kutoa taarifa sahii na kwa wakati katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 26 mwaka huu ili kuiwezesha serikali kurahisisha mpango wa miaka mitano na malengo ya millennia ifikapo 2015.

Mulongo aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa sensa ya watu na makazi ya uhamasishaji juu ya maandalizi ya sensa itakayofanyika nchini kote tarehe 26 agost mwaka huu.

Alisema kuwa sensa ya watu na makazi ndio chanzo pekee ambacho kinaweza kutoa taarifa sahii kuhusiana na rasilimali hivyo ni vema wananchi wakatoa taarifa hizo kwa umakini na weledi  ili serikali iweze kuchukua hatua za utekelezaji.

Aidha ameitaka jamii kutowaficha wale wote wenye ulemavu bali wahakikishe kuwa wanatoa takwimu zao kwa kuwa nao ni watu muhimu katika jamii na wana haki ya kuishi.

“Naombeni ndugu zangu kundi la walemavu ni watu muhimu sana muhakikishe kuwa mnapata taarifa zao kwa usahihi kwani wengi wa wananchi huwaficha kwa kudhani ni aibu “alisema Mulongo 

Hata hivyo aliwataka wasimamizi wa sensa hiyo ambao ni walimu kuhakikisha kuwa wanasimamia kwa uaminifu na uadilifu na kuacha kutanguliza masilahi mbele.

Kwa upande wake mratibu wa sensa kwa mkoa wa Arusha Magreth Martin aliwahimiza wadau hao mambo ya kuzingatia wakati wa kuhamasisha wananchi kuwa ni tarehe ya sensa pamoja na umuhimu wa sensa kwa jamii kwa kuwa wengi wa wananchi hawatambui umuimu wake.

Aidha aliwataka wadau hao kuwaelimisha  wananchi kuwa zoezi la sensa halihusiani kabisa na hofu au imani walizo nazo na pia wawahakikishie taarifa watakazozitoa wakatii wa kujibu maswali ya sensa zitakuwa siri na zitatumika kwa maswala ya kitakwimu pekee.

Hata hivyo hii ni sensa ya tano tangu  kupatikana kwa uhuru mwaka 1961 na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Ambapo Sensa ya kwanza ilifanyika mwaka 1967 na kufuatiwa na sensa nyingine za mwaka 1978,1988 na 2002.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...