habari kazi brother michuzi.


Nimepata email ndogo kutoka kwa kijana mmoja anaetaka kutembelea tanzania na ameniuliza masuali haya mawili:-


How much should i expect to pay for a taxi from dar es salaam airport to city centre? 
How safe is Mafia street, should i avoid to go there?


Nimeshindwa kumjibu kwani ni muda mrefu kidogo sikufika tanzania bara na kwa hivyo sielewi hali ilivyo huko kwa sasa. kuna yeyote anaeweza kunipa majibu?


ahsanteni
Mdau Zenji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Jibu si unalo tayari!!??? Mjibu kwamba 'HUJUI' kwani muda mrefu hujafika Tanzania bara, na huelewi hali ilivyo sasa. Majibu utakayopata kutoka kutoka kwa watu wengine si yako, na hayana uhakika, na utakapompa majibu hayo utakuwa unasema uongo maana ki ukweli HUJUI. AKipata matatizo lawama zote utapata wewe, maana utakuwa umetoa majibu ambayo si yako. Yeye anataka kujua kwa kusikia kutoka kwako, na wewe HUJUI. Tatizo la watanzania tulio wengi HATUTAKI KUSEMA KWAMBA HATUJUI KITU, tunataka kulazimisha na kuwaonyesha watu wengine kwamba tunajua - hakuna dhambi kwa kusema SIJUI.

    ReplyDelete
  2. Kutoka DIA mpaka City centre ni 30,000/=. Mafia ni salama kama anataka kutembelea Mafia tunamkaribisha. Tanzania yote ni nchi ya amani na ukarimu. Pamoja na hayo akiwa Tanzania nivyema mahali popote unapokwenda ukiwa ni mgeni apate maelekezo kutoka kwenye nyumba ya kufikia wageni alitakapofikia.

    ReplyDelete
  3. taxi ni kama 10,000 hv au zaidi kidogo eqv. $10. Sehemu zote za city center ni salama labda itokee tu kwa bahati mbaya-ni vizuri tu akawa mwangalifu kuanzia pale airport na hata huyo taxi driva amwangalie maana sa nyengine anaweza akatumiwa. kwa ujumla dar ni salama kama lilivyo jina lake amani tu tofauti na nairobery.

    ReplyDelete
  4. Mdau Zenji,

    Hahahahaha,

    Mweleze Mgeni wako aje Tanzania hakuna wasiwasi wowote kwa kuwa Bongo Tambarale!

    MAJIBU YA MASWALI YA MGENI:

    1.Usafiri wa Taxi kwa sisi wenyewe ni kama Tshs. 10,000 au Tshs. 20,000 hivi sasa yeye Mgeni anaweza pigwa kidogo zaidi ya hapo.

    2.Asiwe na wasiwasi na jina 'MAFIA STREET' na aje afike hadi Mtaani hapo, kwa sisi Bongo haimaanishi kama kule Italy zaidi ya atakuta 'KIDUKA CHA JUICE' CHA MDAU MWENZETU ANAYETUMA MAONI humu ktk Blogu, wala hakuna dalili yeyote ya Ugaidi au Uhalifu zaidi ni labda wasiwasi wa Mateja wachache wadokozi.

    ReplyDelete
  5. Kuhusiana na Gharama za tax kutoka Eapoti hadi mjini anatakiwa kuwa na kitu kama dollar 25 hivi, au Tsh equivalent to that amount. Kwa maana pale tax zake bei huwa juu kidogo. Mfano mimi nikiwa sina mzigo mkubwa, I would rather tembea kwa miguu mpaka njia panda pale maeneo ya Karakata. Pale unaweza kupata tax hata kwa Tsh 10,000 tu mpaka town au ukachukua bajaj, lakini hii ni kwa wazoefu.

    Na kuhusiana na mtaa wa Mafia street ni mtaa salama sana tu, hauna uhusiano wowote na kundi la katili la Mafia la nchi Itali, mtaa huo ulipewa jina hilo katika kukienzi tu kisiwa chetu cha Utalii cha Mafia. Ila tahadhari za kiusalama za kawaida ni muhimu kuchukuliwa hususan ukiwa mitaa ya Kariakoo.
    Kwa ufupi hali ya Usalama Tanzania imeimarika sana. Hakuna tena matukio matukio ya Uhalifu.

    Mwambie akaribie Tanzania.

    Khamis JK.
    0765 519658

    ReplyDelete
  6. A taxi to the city centre from the airport would cost between 25,000 and 30,000 Tanzanian Shillings. Mafia street is in Kariakoo and considered to be safe during day time. It's a busy business area full of people of [Tanzanian and non Tanzanian traders from Rwanda, Burundi, DRC, Comoro and upcountry regions]. But, just like in any other areas of Dar es Salaam precaution is always important and don't show that you are a stranger to the area.

    ReplyDelete
  7. Ndugu mdau

    NAULI ZA TAXI

    Viwango vya nauli za taxi toka airport mpaka town vimeandikwa kwenye ubao wa taxi drivers na pia hata ukiwauliza watakuambia bila kificho, ila haizidi Tshs. 30,000

    Lakini pia anaweza kupanda daladala kama si lazima kuchukua taxi na nauli ni Tshs.350 mpaka Kariakoo au Posta

    MAFIA STREET

    Kama yalivyo maeneo yote ya kariakoo, Mafia street iko safe usitegemee mtu kupigwa kisu, risasi au kudhuriwa kwa aina yoyote ile ila kikubwa ni wezi wa mifukoni na sio tu Mtaa wa Mafia ila kariakoo yote, na hii ni kutokana na wingi wa watu

    ReplyDelete
  8. Ahhh wapi !

    Asiwe na Presha.

    1.Aje hivyo hivyo kichwa kichwa atakutana na Madereva wa Teksi Vishoka ,wakiona jamaa ni Mzungu, ohhh watampiga ndefu,,,hapa haponi mtu !

    2.Mtaa wa Mafia-Kariakoo hakuna Ujambazi wala wala asiogope aende tu akifika la zaidi atakikuta ''Kiduka cha Juisi''

    ReplyDelete
  9. Mdau Zenji:

    Kama unavyoelewa Bongo hatuna 'Pricing system' kwa mfano unamwita Chinga anauza kitu anaanzia Shs. 40,000/= unatakiwa na wewe useme unaweza mshusha ukakipata kwa Shs. 4,000/= tu !,,,Hii ina maana hata bei inatoka kulingana na Muulizaji alivyo ukionekana Bosi Bosi basi Chinga anaanzia juu zaidi, kwa hiyo huyo Mzungu anaweza fika Uwanja wa Ndege kwa Gharama ya Kawaida ya Teksi ni Tsh.20,000/= sasa Jamaa Mashanta na Ma Dei waka wa Teski wanaweza kumpiga hata Tshs. 200,000/= (Laki mbili) kama asipopata maelekezo , la zaidi mtumie hizi habari na ukiweza mpe Exchange rate kati ya Ths. na US$.

    Aidha suala la 'Mafia' mtoe wasiwasi kwa Bongo ni Kisiwa kimoja wanakaa Wavuvi tena wachovu kweli, sio Mafia ile ya Italy ya Biashara za Madawa na Maujambazi !
    Kwa hapa Dar wamelipata jina 'Mafia Street' kwa ajili ya Kisiwa hiki Bahari ya Hindi wala hakuna uhusiano wowote na huko Ubayani Italy !

    ReplyDelete
  10. Hahaha Mdau Zenji,

    Niache nicheke !

    Mfano wa woga wa 'Mafia Street'

    Nakumbuka pana matukio mawili yalijiri kama hapa chini:

    1.Jamaa Maalim Mmoja (Mwalimu wa Dini ya Kiislam) alisafiri mikoa ya Kusini Lindi hadi Mtwara akafika Kijiji kimoja akapewa mtu wa kumshindikiza ili afike aendako, akamuuliza mwenyeji leo tunaanza safafri tutalala wapi ,Mwenyeji akasema tutaondoka Hapa Newala tutakwenda kulala 'NANGURUWE' !, yule Maalim akastuka akasema hapana sitkubali kwenda kulala 'Nanguruwe' akiwa hajui ya kuwa Nanguruwe ni jina la Kijiji.

    2.Mwingine alitoka Bara akaja huko Zenji akamuulizia mwenyeji wake yupo wpai akaambiwa akitaka amuone aende huko 'MCHAMBAWIMA' ndio atamkuta mwenyeji wake, jamaa wa bara akasema hapana siwezi kwenda huko !

    Sasa huyo Mgeni anafikiri na kuhusisha 'Mafia Street' na wale Wahalifu Genge la Maharamia wa biashara ya Madawa ya kulevya huko Italia.

    ReplyDelete
  11. Asalaleee,

    Jamaa yako usipomwelekeza vizuri au kwenda kumpokea Airport siku hiyo akifika atawapa watu hela ya kula kwa aina kibao za Ganji:

    -Ganji kusikia,
    -Ganji kuona,
    -Ganji panga,

    Jamaa atadakwa na Shanta wa Taksi atatajiwa bei ya JUU kabisa !, halafu atapelekwa kwenye teksi, Dereva atapewa panga lake, waliosikia watapewa zao na walioona watapewa zao, hata kama ulipita njia ukikakamaa na wewe unapata za Mzungu !

    Mtaa wa Mafia aje ila awe Makini na Mateja wa Kariakoo tu hakuna lingiza

    Hii ndio Bongo Tambarale !

    ReplyDelete
  12. mwambie nauli ya taxi ni sehemu ndogo tu ya nauli atakayotumia kutoka kwao kuja tanzania, kuhusu usalama mafia street, mwambie ni salama sana kiasi kwamba sisi wakazi wa mafia tukitaka kwenda kwao hatuulizia hali ya usalama ya kwao ingawa kwao si salama ndio maana ana wasiwasi kama kwetu (mafia street) kuna usalama

    ReplyDelete
  13. Kama wewe ni Mtanzania kujua mambo hayo si lazima uwe nchini, hata ukiwa mahali popote kama wewe ni mzalendo hayo yote waweza kumjibu. Sasa hivi dunia ni kama kijiji utandawazi ni mwingi hivyo kujua kinachoendelea nyumbani ni rahisi sana.

    Jitahidi kufuatilia mambo yanavyoenda nyumbani kwako.

    ReplyDelete
  14. Ohhh,

    Huyo jamaa Mgeni wako Mdau wa Zenji atapokewa kama Raisi !

    MAFIA kwa Bongo ni Kisiwa cha watu tena wapo choka mbaya tu, wala hakuna ujambazi wala nini.

    Airport pana Vishoka wana njaa balaa na akifanya mchezo ataibiwa sana tu.

    Wewe fanya utafute muda utoke huko Zenji uje Dar kumpokea ama sivyo itakula kwake !

    ReplyDelete
  15. Mgeni atapokewa kama Mpira wa Kona!

    Mwenye Deni kwa baba mwenye nyumba wake atalipa jioni hiyo Mzungu akiingia Bongo.

    Hapo ndio ataona 'Ari ya kazi' kwa Vijana wa Uwanja wa Ndege Dar Es Salaam.

    Mweleze Mzungu kuwa Mfia street ni mtaa mbovu tu hapa Dar tofauti na jina lilivyo linavyotisha !

    ReplyDelete
  16. Mzungu wako atapokelewa na Mawakala wa Dar Airport kama Bwana Harusi!

    Watu wana njaa balaa pale na hata ukiibiwa hakuna Msaada wowote.

    ReplyDelete
  17. 1.Airport to City Centre only 50,000 equivalent to Usd 30.
    2. Mafia street has got nothing to do with Mafia gang so it is safe as the whole Dar is let him don't be worried because of that name.

    Please he/she most welcome to TANZANIA. as we love guests.

    ReplyDelete
  18. Aiport mpaka Dar City Centre ni TZS 30,000. Kuhusu usalama mtaa wa Mafia ni hivi,kama ilivyo sehemu nyingi za mjini duniani, ni vizuri ukawa na mwenyeji wako. Muda wa mchana sio mbaya lakini usiku ni vizuri ukachua tahadhari. Hakuna garantii ya miezi 12...... ha ha ha. Nawasilisha mdau.

    ReplyDelete
  19. For safety he should be prepared to pay around 30,000 or rather $20 , the price is factor or fuel price which changes after every 2 weeks.
    What is so specific with Mafia Street, he should have a company when going to places unfamiliar to him

    ReplyDelete
  20. Jamani huyo mtu anataka kweli kuja au hiyo ni vichekesho tu,,au na wewe mdau umeamua tu kuandika?kwani wewe si umwambie Hiyo Mafia street ni jina tu haiusiani na mafia yoyote?,,kwani yeye anandugu mafia street,,
    Hata ukamwambia bei ya kutoka Dar Airport to mjini ndo utakuwa na Tax siku hiyo?Na akifika bei ikawa imepanda
    Hiyo joke sijaipenda ni ya kitoto mno.

    Ahlam UK

    ReplyDelete
  21. halow mdau mimi naitwa nurdin hua na kwa kifupi najishugulisha na shughuli nyingi zina jikita na utalii kwa kiasi fulani so kama unahitaji msaada wa huyo mtu wako ninajua hoteli za bei nafuu na hata KUTOKA AIRPORT na ukiwa na shida yoyote kwa hiyo naweka namba yangu kwa ajili ya mawasiliano ha chini ili tuwasiliane kwa zaidi 0713 287020 asante

    ReplyDelete
  22. kutoka airport mpaka center ni elfu 30, yaani dola 20. tz ni safe na asiogope kuja, na wewe uliyeomba utumiwe hii post yako fanya ufike tz bara sio kupiga box tu huko

    ReplyDelete
  23. Asante mdau Zenji, kwanza kabisa hongera na nakuomba daima usisite kuitangaza nchi yako, Daressalaam inajulikana kama bandari salama, rangi zote za watu zipo hapa na wanaishi kwa amani ile mbaya, mwambie achukue taxi kutoka airport hadi Magomeni Mapipa, afikie hotel ya Pacific ipo barabarani kabisa karibu na kanisa la KKT hii ni morogoro road, ,hapa akisha weka mizigo yake hotelini, mlo wake wa kwanza aende seaboys restaurant,kwa $ 2 atakula samaki sato, au kuku wa kuchoma, au pilau yaani kama yuko kwako labda zaidi ya kwao-maana huku bongo chakula chote ni fresh. Hapo seaboys ni kituo cha taxi pia na ni center ya mji hivyo ataweza kwenda popote pale bila shida yoyote, ile-Hoteli ya Pacific ni safi na ni cheap $20 kwa siku ni chumba safi chenye A/C . kisha taxi kutoka uwanja wa ndege hadi magomeni ni elfu 20 hivi yaani $ 15 au 10. haya mwambie aje, na kama anapenda kujimwaga ,basi kuna bar inasifa zote Congo bar ,hapa atakutana na madadazzzii watamtoa uchovu wa kiuno-Bongo we achatu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...