Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania lilopo Kawe Jijini  Dar es Salaam Pastor Josephat Gwajima, ambaye pia ni mwanzilishi na Kiongozi wa Glory of Christ Ministries International anatarajia kufanya Mikutano Mikubwa ndani ya Jiji la London nchini Uingereza kuanzia tarehe 29 Aprili 2012 mpaka tarehe 6 Mei 2012.

Mch. Gwajima, anapenda kuwakaribisha Watanzania wote waishio London na ataombea watu wote, wagonjwa ya kila aina, walioteswa na kuonewa na ibilisi kwa muda mrefu, wasioweza kupata watoto, watu waliobiwa na kupotea katika mazingira tata watarudishwa, wafu watafufuliwa (Isaya 42:22), watu wenye balaa na mikosi wataombewa pia.

Ili kufika katika Kanisa la Glory of Christ Ministries International lililopo London, tafadhali fuata anuani hii:

GLORY OF CHRIST MINISTRIES INTERNATIONAL
LANGHAM ROAD,
TOTTENHAM, LONDON
N15 3RB
 Kwa maelezo zaidi, wasilina nasi hapa London kwa simu zifuatazo:- 0742 753 2044 / 0742 966 7095
 Tafadhari, upatapo ujumbe huu wahabarishi, ndugu, jamaa, marafiki na wapendwa wetu wote waishio jijini London.
 ©2012-GCTC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...