Rais Dkt. Jakaya Kikwete akitangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi na Waziri wa Sheria na Katiba Mama Celina Kombani.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakitoka chumba cha mikutano Ikulu baada ya Rais kutangaza wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakimsubiri Rais Kikwete kuja kutangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo Ikulu jijini dar es salaam.
Rais Kikwete akitoa ufafanuzi kuhusu Tume ya mabadiliko ya Katiba aliyoitangaza, akisisitiza kwamba tarehe ya kuanza kazi itatangazwa rasmi mara baada ya wajumbe wote kujulishwa uteuzi wao na baadae kuapishwa. Ila kisheria tume inatakiwa iwe imekamiliosha kazi ndani ya miezi 18.
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
(Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83,
Toleo la 2012, Vifungu 5, 6 na 7)
______________________________
UONGOZI WA JUU
1. | Mhe. Jaji Joseph Sinde WARIOBA | - Mwenyekiti |
2. | Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino RAMADHANI | - Makamu Mwenyekiti |
WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - BARA
1. | Prof. Mwesiga L. BAREGU | |
2. | Nd. Riziki Shahari MNGWALI | |
3. | Dr. Edmund Adrian Sengodo MVUNGI | |
4. | Nd. Richard Shadrack LYIMO | |
5. | Nd. John J. NKOLO | |
6. | Alhaj Said EL- MAAMRY | |
7. | Nd. Jesca Sydney MKUCHU | |
8. | Prof. Palamagamba J. KABUDI | |
9. | Nd. Humphrey POLEPOLE | |
10. | Nd. Yahya MSULWA | |
11. | Nd. Esther P. MKWIZU | |
12. | Nd. Maria Malingumu KASHONDA | |
13. | Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb) | |
14. | Nd. Mwantumu Jasmine MALALE | |
15. | Nd. Joseph BUTIKU | |
WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - ZANZIBAR
1. | Dkt. Salim Ahmed SALIM | |
2. | Nd. Fatma Said ALI | |
3. | Nd. Omar Sheha MUSSA | |
4. | Mhe. Raya Suleiman HAMAD | |
5. | Nd. Awadh Ali SAID | |
6. | Nd. Ussi Khamis HAJI | |
7. | Nd. Salma MAOULIDI | |
8. | Nd. Nassor Khamis MOHAMMED | |
9. | Nd. Simai Mohamed SAID | |
10. | Nd. Muhammed Yussuf MSHAMBA | |
11. | Nd. Kibibi Mwinyi HASSAN | |
12. | Nd. Suleiman Omar ALI | |
13. | Nd. Salama Kombo AHMED | |
14. | Nd. Abubakar Mohammed ALI | |
15. | Nd. Ally Abdullah Ally SALEH | |
UONGOZI WA SEKRETARIETI
1. | Nd. Assaa Ahmad RASHID | - Katibu |
2. | Nd. Casmir Sumba KYUKI | - Naibu Katibu |
Leo ni Ijumaa Kuu siyo siku ya Kazi
ReplyDeleteSerikali KUU (IKULU),Hospitali zote, Idara ya Usalama na Polisi hazina LIKIZO WALA SIKUKUU !
ReplyDeletekikwete (my president)umefanya kama inavyotakiwa lakini tukiangalia umri wa hao wakuu wa hiyo tume mbona umekwenda sana huoni kama hicho kitakua ni kikwazo hebu angalia wanatutengeneze katiba au wanatuachia usia tafadhali mkuu wangu hebu penyeza vijana kwa wingi
ReplyDeleteUmesahau, ndege na meli mabasi na daladala zote zinatembea au na wao waende kulala sikukuu. Nyumbani mama lazima apike chakula, petrol station zifungwe na zenyewe na umeme uzimwe, Tanesco wasifanye kazi na nyumba yako ikiungua fire wasifike maana ni sikukuu. Nakwambia ukumbi una wajinga kuliko werevu.
ReplyDeletewatu hawa ni wengi sana hakuna na haja ya kuwa na timu ya wanzibari na watanzania bara kwanini tusiunde timu ya watanzania tuangalie katiba yetu namuunga mkono aliosema wazee amejazaa wazee watupu yaani jamani hakuna watu wengine tanzania hii wenye zaidi ya hawa ambao tumewasikia tangu tukiwa vidudu?
ReplyDelete