Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo (kushoto) akitia saini kwenye hundi yenye thamani ya sh. mil. 100 alizotoa msaada kwa Chadema, baada ya kufurahishwa na ushindi wa chama hicho katika Jimbo la Arumeru Mashariki Jumapili. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa chama hicho, Antony Komu. Hafla hiyo imefanyika leo nyumbani kwa Sabodo Upanga, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa (kulia), akimshukuru mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo baada ya chama hicho kupatiwa msaada wa sh. mil. 100, kwa kufurahishwa na ushindi wa Chadema katika uchaguzi uliofanyika  Jimbo la Arumeru Mashariki, Arusha Jumapili. Hafla hiyo ilifanyika, Dar es Salaam
Picha na Kamanda Mwaikenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. I am tempted to call this man "The father of Democracy". Congratulations to you Mr. Sabodo for your individual efforts to see democracy thrive in Tanzania.

    God Bless You!

    ReplyDelete
  2. Hii ndio Siasa ya Tija , sio kuegemea kwenye Chama kimmoja tu.

    Sabodo yeye ni CCM lakini ni mfano mzuri wa Demokrasia kwa sababu Demokrasia ndio msingi wa Maendeleo!

    ReplyDelete
  3. zitawatokea puani hizo hamumjui muhindi nini. Halafu Mzee Slaa mkono wake umeathirika nini, I kind of notice it bein in that position during the campaign.

    ReplyDelete
  4. Hivi CHADEMA chama kinachopenda demokrasia kilitoa fomu za kugombea ubunge Afrika Mashariki? Eti bwana Komu???

    ReplyDelete
  5. Hizo hela 100 Milioni ni za Maendeleo ya Siasa na sio kujengea Ma Bar na ma Pubs ,,,sawa Chadema?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...