Na Mary Ayo, Arusha
SERIKALI imesema juhudi za makusudi zinatakiwa kuhakikisha kuwa wawekezaji wengi wanajikita kwenye ukataji na ung’arishaji wa vito ili kuongeza thamani ya madini hapa nchini.
Akifungua maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya madini na vito jijini Arusha jana, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliwataka wawekezaji kwenye sekta ya madini kuwekeza kwenye ukataji na ung’arishaji wa madini ili kuongeza ajira nchini na ukusanyaji kodi.
Alisema serikali ilizuia usafirishaji nje wa madini ya tanzanite yasiyoongezewa thamani ya ukubwa wa gramu moja na kuendelea ili kuwajengea uwezo watanzania waweze kukata na kung’arisha madini hapa hapa nchini.
Alisema kwa miaka mingi idadi kubwa ya madini yazalishwayo nchini yamekuwa yakisafirishwa yakiwa ghafi, na kuisababisha nchi kukosa mapato.
Waziri Ngeleja alisema mwaka jana serikali ilianzisha utaratibu wa kuhakikisha madini ya Tanzanite yanaonyesha kuwa yanatoka Tanzania yaani ‘certificate of origin’ kabla ya kuyasafirisha kuyapeleka nje ya nchi.
“Hii ndio maana tumekuja na mkakati huo kuwashawishi wawekezaji kujiingiza kwenye eneo hilo ili kukomesha utoroshaji wa madini yetu.”alisema Ngeleja.
Aliongeza kuwa hatua hii itasaidia sana kuongeza ajira kwa watu na serikali kupata mapato ya kutosha kutoka kwenye sekta ya madini.
Aliwahakikishia wawekezaji kuwa serikali itatoa leseni kwa wale watakaojiingiza kwenye eneo hilo na kutambuliwa kama wawekezaji.
Waziri huyo alisema serikali itaendelea kusisitiza uwekezaji kwenye uzalishaji wa vito hapa nchini kabla ya kusafirisha nje.
Alisema hatua hii itawekezekana kutokana na ushirikiano uliopo baina ya serikali na sekta binafsi ndani na nje ya nchi.
“Tunajitahidi kuwaalika wawekezaji kutokana na mazingira mazuri yaliyopo,” alisema na kuongeza kuwa Tanzania ina madini ya aina nyingi ambayo yanatakiwa kuchimbwa.
Maonyesho hayo yameandaliwa na Chama cha wachimba madini nchini (Tamida), na kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka nchini na nje ya nchi.
Soti kwanza mikataba ya wawekezaji wa madini nchini kisha ndio suala hilo ulilozungumzia litiliwe mkazo! Bila hivyo haina maana hata kidogo!
ReplyDeleteMikataba ya wawekezaji katika sekta ya madini ifanyiwe marekebisho,baadaye ndio litiliwe mkazo suala la vito,vinginevyo tutalia kilio cha mbwa pua juu
ReplyDeleteHuu ni utani!Inanipa wasiwasi kwamba we may be having the wrong people at the wrong places at the wrong time!Bado watanzania tunacheza na sekta ya madini.Imagine Dhahabu yote iliyopo nchini,lakini thamani ya shilingi yetu bado duni sana!Tuna ambiwa GDP au Pato la Taifa linakuwa kwa kasi sana,Kasi Gani?eti kwasababu Tunazalisha Dhahabu kwa wingi zaidi,lakini dhahabu hiyo inaishia wapi?Yameanza kutushinda,tunafikiri tunaweza kuvutia wawekezaji sasa waanze "kazi za usonara(?)",waanze kuchonga vito nchini?this is ridiculous!nani atakubali?unless hujui the ABCD'S of gold mining or Umafia wa biashara ya madini!Tuwekeze zaidi katika kujenga vyuo au Kutoa Masomo Maalum ya Ufundi Stadi katika teknolojia hii ya "usonara"na kun'garisha vito na madini mengineyo kwa vijana wetu kwa malakhi wanaomaliza Form Four plus kila mwaka! jamani acheni this Longolongo business ya kufurahisha majukwaa for personal gains!People can never agree to be fooled all the time,may be only once,period!Hatuna hata uwezo wa kusafisha dhahabu hapa nchini hadi kufikia kiwango cha ubora wa asilimia 99.99999%!All the gold is sold Raw overseas!tuna watu hapa kweli,au utani?
ReplyDeleteMikataba kwanza jamaniii...
ReplyDeleteAfu tunaomba priority kwa wawekezaji wa ndani ya nchi!!
Sawa kabisa wadau mlioshusha mada hapo juu.
ReplyDeleteNi wazi kabisa kumedhihirika udhaifu mkubwa katika sekta ya madini na jitihada zilizofanyika ni "senti hamsini tu!!"
Ukiacha sekta ya madini, kuna maeneo lukuki yamesahaulika ama ni kufumbiwa macho.
Tanzania kwa ujumla imekuwa ni nchi legelege kwa upande wa viwanda. Leo hii kuanzia korosho, kahawa, na mpaka hayo madini kwa asilimia kubwa tumekuwa tukisafirisha kama mali ghafi, halafu, kwa mfano kahawa hiyo hiyo, tunakuja kuuziwa kwa bei ya juu baada ya ku-prosesiwa.
Maneno na ahadi finyu hazitoshi. Mh Waziri anasema wawekezaji wajitokeze na watakaojiingiza kwenye eneo hilo watatambuliwa kama wawekezaji!! Leo hii mwekezaji mzawa akijitokeza anapata unafuu gani? Mbali na kodi kabla hata hajaanza biashara, kuna viunzi kibao lazima aviruke mpaka kufikia hiyo sifa ya kuitwa mwekezaji. Sasa ni wakati wa matendo hai, na itakuwa busara kama wawekezaji wa nyumbani wakipewa unafuu kwa upande wa kodi, na gharama za vitendea kazi ili kuweza kujititimua na kutoa huduma zitakazonufaisha taifa kwa ujumla.
Inasitisha kuona nchi yetu inavyomalizika kila kukicha wakati tunayo mali ghafi, madini, na wasomi kibao tu.
Wakati wa kutoa nafasi kwa wenye uwezo na sio kujuana aka kubebana umefika. Tuepuke ubinafsi na kujipendelea, tuongeze bidii katika kujenga na kuongeza mbinu za manufaa kwa wote.